globu ya jamii ilipokwenda vekesheni sauzi hivi karibuni iligongana na supa modo wetu millen akifanya vitu vyake na kuongea naye kwa muda mfupi kabla hajakimnbilia kazini...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. I am gonna go.....au I have to go???....kwa nini msiongee kiswahili jamani??

    ReplyDelete
  2. kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  3. HIVI KUMBE HAJUI KISWAHILI VIZURI?UNAJUA NILIJUA KUWA NI MTANZANIA KAZALIWA TANZANIA KASOMA TANZANIA.ILA KUMBE NILIKUWA NAKOSEA.DAHHHHHH!!!

    ReplyDelete
  4. maji ya chumviSeptember 16, 2009

    mbona wengine wanaitwa hawakimbii?,sasa hii nidham ni yeye tuu au anakukimbia wewe michuzi? maana naona kama alianza kubabaika.kaka michuzi watu tunapenda tutoke kwenye tv lakini waosha vinywa bwana!!!!dah hawakosi lakusema yailahi toba.

    ReplyDelete
  5. Kajongo.. unafanya mchezo.

    ReplyDelete
  6. For the first time inabidi nimtetee mtanzania mwenzangu though mimi si mtu wa kufagilia malimbukeni.
    kuna mazoea,tabia,dialect mtu unadopt kutokana na jamii unayoishi nayo. tatizo ni kwamba kuna watu wanaokuwa sincere na kuna wanaojifanya hawajui kwakuwa wanaiga.especially watu wanaokaa us wanapenda kuiga wamarekani weusi wanavyoongea na 90% unakuta si kiingereza sahihi.ukianzia tenses,nouns and kila kitu kwa ujumla but swala la kwamba eti mtu hajui kiswahili mmm...sijui labda lipo but lugha ukiiongea mpaka age of 12 huwezi kuisahau ofcourse kuna kuchanganya but ile ya kujifanya kabisa eti kuna maneno huyajui mmhh...i doubt
    n'ways kila mtu na lwake...

    ReplyDelete
  7. Asante KILO nilitaka kusema hilo Iam gonna go??? Tuongee kiswahili jamani! Anajua kiswahili vizuri tu ila si unajua tena sasa hapo ndo yupo South Africa....sasa akienda Marekani ndo itakuwaje?? Sikujuan kuwa nae ni mshamba kiasi hicho nilikuwa naumuona kuwa Miss ambaye ni bora kuliko wote lakini....

    ReplyDelete
  8. Uongo dhambi ENGLISH hajuo bado lugha inampiga chenga!!!!

    ReplyDelete
  9. Ukiskia MASHAUZI ndo hayo alonayo huyo "super modo"! Hovyoooo kwa chuzi la magozi halina ladha kabisaaaaa!

    ReplyDelete
  10. Ama kweli kutawaliwa ni zaidi ya kurogwa. Yaani tumefika sehemu tunaona ujiko kutokuongea lugha yetu asili? Na hata hiyo nyingine ambayo tumechagua nayo hatuiwezi...! Tumefika sehemu hakuna lugha tunayoweza! Tunaongea a bit of Swahili, a bit of English, a bit of our tribal language.... Bora urogwe kuliko kutawaliwa.

    ReplyDelete
  11. Hajakosea kabisa kusema AM GONNA GO, hivyo ndivyo wanavyosema wenyewe huku majuu, mdau namba moja hapo juu, nahisi uko BONGO na hujatoka majuu, that is perfect street language. NA KAMA UNAONDOKA BILA YA RUHUSA YA MTU UNAYEONGEA NAYE HUWEZI KUSEMA KUSEMA ULIVYOSEMA WEWE YAANI, I have to go, MTU UNAYESEMA NAYE ANAWEZA KUKUAMBIA no don't go. LAKINI KAMA UNATAKA KWENDA AU UNAENDA KWA POWER ZAKO UNASEMA I AM GOING NOW ambayo ime-slangiwa AM GONNA GO. upo hapo. The same as I WANNA GO = to you is I WANT TO GO

    ReplyDelete
  12. Michuzi Umeachwa soremba,Nadhani mdomo ulikua wazi kwa dakika.

    ReplyDelete
  13. Mdau uliyetoa maoni ya kwanza hapo juu, hicho ni kimarekani cheusi kwa taarifa yako, yuko sahihi sana tu. Ila pozi zake za kutafuta maneno ya kiswahili, eti ameyasahau, hapo ndipo anaponikata stimu, otherwise yuko juu.

    Mdau
    Uholanzi Kaskazini.

    ReplyDelete
  14. Michuzi,nimebandika maharage jikoni nasikia kama kaharufu,nafikiri yanaungulia.

    AM GONNA GO !!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. hahahahah eti hajui kiswahili !! what a shame!!

    ReplyDelete
  16. Huyo naye alisema kuwa "AM GONNA GO' naye kachemsha hakuna watu wanaoongea hivyo!! I wanna go hiyo ndo lugha ya mitaani. Na AM GONNA GO hivyo ni watu wasiojua kiinglish kabisa na sijui umetoa wapi manake ha mablack wa majuu hawasemi hivyo.

    ReplyDelete
  17. Wewe Michuzi kweli mchokozi yaani mtoto wa watu unamkaanga hivi hivi kutumia mafuta yake mwenyewe? Sasa kwanini usingebandika hiyo interview utakyofanya naye baadaye? Mtoto wa watu kachemsha kaweka kinumba ndani na anabidi akimbie sasa. Mimi mwenyewe hapa nimeitwa I am gonna go...

    ReplyDelete
  18. tatizo watu wanafikiri kuongea slang ya african american ni dili, lol, si dili ni ujinga, ukiongea kiswakinge mi naona ni poa tuu, kwa sababu tuna internation school kibao tu bongo kwa hiyo kila mtu anataka kutoka chicha. Bro michuzi ni ombi langu ufanye mahojiano na any one of the super star wa bongo. kwa lugha ya kiingereza kuanzia mwanzo hadi mwisho tusikie..

    ReplyDelete
  19. Never heard of I'm gonna go before nijuavyo mimi Wanugu (na mimi pia) wanasema "I gotta go"

    ReplyDelete
  20. Huyo mvinje sijui supa modo wa kibongo Milen, ngeli hajui, huwezi kusema "am gonna go", na wewe uliyemtetea na wewe boya vile vile, hujui ngeli...hajapatia wala nini kama ni ngeli ya ki-slang alitakiwa aseme "I gotta go" ambayo Michu angeitamka kama "ai gara goo"...msitufanye maboya humu, hajapatia wala nini...ila nimeinyaka cologne anayotumia...hmmm ndio maana Michu alikuwa anamsogeleaaaa...kumbeeeee! Mvinje ananukia kinyama.

    mdau
    Ashkmatit

    ReplyDelete
  21. habarini zenu,
    kuongea slain kwa hapa marekani ni dalili ya kutokuwa na Elimu...asilimia kubwa ya watu wa namna hiyo hawana shule,na pia ni njia ya kuonyesha,hata wakati wa mahojiano nani ana shule na nanani hana shule,nani ameishi kwenye mazingira ya shida na nani hapana...
    Hakuna mzungu unayemkuta anaendekeza slain,sababu slain ni lugha ya class ya chini.
    Niko hapa marekani mwaka wa kumi sasa,najua ni jinsi gani ilivyo tabu kuongea lugha bila kuchanganya.
    Profesa,Washington

    ReplyDelete
  22. Wanawake kwakujifanya wanaongea english bwana!! ah, yani huyu ninavyomuona english ya masaa mawili atakua kama Kanumba,,unajua mimi namlaumu kidoogo Mithupu ,kwasababu mtu kama huyo azungumze naye kidogo tu english msikie atakavyomwaga kisouth afrika hapa,,wala hana lolote.Mimi kwa utafiti wangu nilioufanya nchi nyingi hapa ulaya na Usa hakuna mtu from afrika anayeongea english kama mzungu au mzaliwa ndani ya english,,never.Utaongea vizuli tuu,,na usikike vizuli! lakini jinsi wenzetu kama hawa weusi wamarekani wanavyonyoosha lugha!! haipo.

    ReplyDelete
  23. SAY WHATEVER YOU WANT TO SAY MILLEN NDIO KASHATOKA HIVYO SASA HIVI NNAVYOANDIKA HII MSG YUKO KWENYE NEWYORK FASHION WEEK UNALO HILO WE KAA NA KINGEREZA CHAKO APO WEEEEEEE SHUTUUUU

    ReplyDelete
  24. Jamani wabongo huwa mnanifurahisha sana... Michuzi asante kwa shughuli! Yaani huwanacheka sana nikisoma comments za wabongo...Nasikia raha kusoma blog yako kwa kweli... keep up the good work Michuzi! Thanks

    ReplyDelete
  25. Anon wa 10.59 unamaana ya SLANG na sio SLAIN. SLAIN maana yake ppl or person no longer living. murdered etc.. lakini nakubaliana na wewe. kuongea SLANG sio dili nchi za nje sio USA tu.

    ReplyDelete
  26. IM GONNA GO,I GOTTA GO,I WANNA GO "HIZI ZOTE NI SLANG HAMNA ILIO SLANG BORA BALI INATEGEMEA TU UNAPENDELEA KUITUMIA IPI WW MWENYEWE LKN KAMWE SITAMUONA MTU HAJUI NGELI ETI KISA KATUMIA MOJAWAPO YA HIZO LA HASHA,WABONGO WENGI HAMJUI KIINGEREZA NA NDIO MAANA MNAWAJAJI SANA WENGINE HASWA WENZENU KWAVILE HAMJIAMINI.HAINIINGII AKILINI KUNAMBIA HUYO MISS ETI HAJUI NGELI WAKATI WEE UNAETURUSHIA MATE YAKO HUJAWAHI HATA KUPANDA NDEGE KELELE TU ZA DEBE TUPU.UTANIKOMVISIJE MM HADI NIKUELEWE WW UNAEISHI BONGO MAISHA YAKO YOTE KUWA UNAJUA NGELI WAKATI NAJUA WAZI HUITUMII NA KAMA HUITUMII UTAIELEWA TU LKN SIO KUIZUNGUMZA KWA UFASAHA NEVER"LUGHA YEYOTE ILE YAHITAJI KUONGELEWA ILI KUI-MASTER VENGINEVYO WIZI MTUPU.TYPICAL WATU WASIOJUA NGELI WANAPENDA KUCHALLENGE ILI WAPATE KUJIFUNZIA HUMO HUMO.KWAMFANO MM UJE UNAMBIE SIJUI NGELI WEE MMATUMBI UNAEKULA TOPE NA VUMBI HUKO BONGO WAKATI MI WAZUNGU HADI WANAZAMA MIFUKONI MWAO NA UBAHILI WAO WOTE JINSI NINAVYOWADANGANYA NA KUWAUZIA MANENO NIPATE KULA YNG KWA LUGHA HIO HIO AMBAYO WEE UNADAI SIIJUI:SASA HAPO MM NA WW NANI KADATA?????

    ReplyDelete
  27. sasa kama lugha hio hio mnayosema haijui ndio wazungu wanayowasiliana nae itakuwa ni nyie wamatumbi ndio hamuijui au wazungu wanaomuelewa ndio hawaijui vizuri????
    NI HAYO TU NANGOJEA JIBU LANGU.....

    ReplyDelete
  28. I gota go!!

    Mdau

    ReplyDelete
  29. Wow i wonder why everybody tryin to be like us (Black American). Well, the right word is I gotta go and the case is closed.
    -Mdau Mnugu wa kibongo ndani ya DC

    ReplyDelete
  30. MISEMO HIYO YOTE INATUMIKA, YAANI "I GOTTA GO" AM GONNA GO", "I WANNA GO" MANENO HAYO YOTE YANATUMIKA NA WATU WOTE WAWE WASOMI, SI WASOMI, MATAJIRI, WAZEE, WATOTO, VIPOFU NI LUGHA AMBAYO SI RASMI LAKINI NI YA KAWAIDA MITAANI, HUWEZI KUTUMIA HIYO KWA SHUGHULI ZA KIOFISI KAMA VILE KATIKA ELIMU NA MAOFISINI LAKINI KATIKA OTHER SOCIAL GATHERING YANATUMIKA NA KARIBU NA KILA MTU, NI MARA CHACHE SANA WATU WAKATUMIA ENGLISH TUIJUWAYO SISI WATANZANIA KWENYE SOCIAL GATHERING, NA WALA SI WA-AMERIKA WEUSI NI YA KILA MTU, NA HUYO PROFESA HAPO JUU NI SI MKWELI KWANI WAZAWA WENYEWE NI WACHACHE SANA WANAONGEA FASAHA NI WATU WALE TU AMBAO WAMEJIFUNA ENGLISH MASHULENI NDO TUNAONGEA SAHIHI, NA PIA HUWA HAWATUELEWI KWA VILE HAWAJAZOEA KUONGEA TUNAVYOONGEA SISI KWA KUFUATA STRUCTUREM GRAMMAR, TENSES. KWA MFANO WAZUNGU WA UK WENYEJI NI MARA CHACHE WANAMALIZA KUTAMKA NENO WAZI WAZI UKALIELEWA MPAKA UZOWEE NDO UTAWAELEWA. IN SHORT ALL WORDS ARE APPLICABLE "I WANNA GO" "I GOTTA GO" AM GONNA GO" HAYA YOTE YANATUMIKA NA YANASEHEMU ZA NA MAHALI PAKE INATEGEMEA UKO WAPI KAMA VILE IN U.K. UKISEMA MOBILE NI SIMU YA MKONONI NA U.S.A. UKISEMA MOBILE NI GARI.

    ReplyDelete
  31. Please don't force your opinions about those words down peoples'throats without a tiny bit of research, all of are English words and are acceptable, for your reference go to the dictionary of English language, " LONGMAN, DICTIONARY OF THE ENGLISH LANGUAGE, MAJOR NEW EDTION, THE MOST INFORMATIVE AND AUTHORITATIVE SINGLE-VOLUME DICTIONARY AVAILABLE, 1990, VOLUME 2, EDITOR JOHN AYTO.

    word GONNA page 678
    word GOTTA page 681
    word WANNA page 1820

    From those three page UTAPATA MAELEZO YOTE KUHUSU MANENO HAYO YAPO NA YANATUMIKA WALA SI MAKOSA, SO TUFANYE UTAFITI KABLA YA KUSEMA HATA KAMA NI PROFESA VULATA.

    ReplyDelete
  32. Dah Mdau uliye tu refer kwenye ditionary na kupa tano. Umefunga ngebe za hao waliokuwa wanajifanya kumzodoa mrembo wa watu utadhani wao wako prfect. Wabongo bwana!. Wivu tuu na roho mbaya ndiyo maana wengi wenu hamuendelei.
    CLOSE TOPIC hiyo.

    ReplyDelete
  33. Dah, haya basi sasa tuachane na lugha, mimi najua huyo binti anajua sana English na pia Swahili. Wengi wenu mlio comentr hamuwezi kumpatra.
    TUONGELEE urembo wake. Wadau mnamuonaje huyo mtoto?. Nadhani kwa uzuri anatuwakilisha vyema wabongo?. Au vipi?

    ReplyDelete
  34. Sasa wewe mdau hapo juu unasema eti wewe uliesomea mashuleni ndo unaejua english sahihi? sasa kwanini ukifika London mzungu akiongea utasubili amalizie helufi zoote? na wewe ni Kanumba mwingine,,kawaida kila lugha duniani kama unaijua vizuli sio lazima uongee helufi zoote! kama unasubili eti mpaka usikie kila helufi ingia dalasani tena halaka,lasivyo utabaki na sorry?x100,mfano wa kiswahili mtanzania halisi ambae sio wa kigoma au bukoba akiongea ,,mambo vipi?mala nyingi sio lazima atamke hiyo bo yamwisho uisikie vizuli,wa TZ kubali hizi lugha za wazungu ngumu!!

    ReplyDelete
  35. Wewe unatafsiri dictionary moja kwa moja uko wrong. Ni lazima ujue namna ya kulitumia neno katika sentence.
    Mfano:
    I wanna go: Nataka kwenda (hamna pressure)
    I'm gonna go: (I'm going to go): nitakwenda au ninakwenda lakini siyo ya kulazimisha, unaaga mfano; I'm gonna go to the store
    I gotta go: ni lazima niondoke sasahivi. Una haraka na inawezekana usitegemee majibu kutoka unayemuaga.
    Hata kwenye simu kukatiza mazungumzo utasema hivyo

    Wewe uliyetoa maneno kwenye dictionary
    Close funga
    Open fungua
    Mchezo sport
    swali: why you are not eating?
    jibu: because I'm closing and I will open in the evening. I don't have time for sporty sporty.

    Kwani hayo maneno si yako kwenye dictionary pia?

    ReplyDelete
  36. She was supposed to say I'm fixing to go

    ReplyDelete
  37. WEE KWELI JUA KALI DAH!!HIVI HUONI HATA AIBU NA HUO UKOSOAJI WAKO WA KIJUAJI WAKATI GRAMMA ERROR WEE MWENYEWE??HUWEZI KUULIZA SWALI KAMA UNAEELEZEA AU KUTOA TAARIFA, KTK KIINGEREZA KUNA NAMNA YA KUULIZA NA KUSEMA TU, KWAMFANO UMEULIZA "WHY YOU ARE NOT EATING?BADALA YA "WHY ARE YOU NOT EATING??NASIKIA KUTAPIKA NA NGELI YAKO KICHEFCHEF JUAKALI BORA UNYAMAZE TU NEXTTIME.UJUAJI MWINGI NA MAKEKE KIBAO KUMBE MAMBUMBU WAZUNGU WA RELI.

    ReplyDelete
  38. KANUMBA KALETA BALAA BILA KUFAHAMU lol lol lol ee mungu wee kwa nini nilisoma msondo mie?? fm academia mnatutesa mtima kukosea ndo kujifunza hata kwenye tangazo la omo wanasema asipochafuka atajifunzaje????????

    ReplyDelete
  39. Jua Kali yaani we misho umefunga kazi LOL!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  40. Anon wa Sept 19 03:52pm
    sorry nilisahau kusema nanukuu
    Hivyo ndivyo walivyoulizana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...