Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (katikati) akionesha mbele ya wanahabari leo tuzo iliyotolewa zawadi kwa Kiwanda cha Bia cha Mwanza kwa kuwa washindi wa uzalishaji bora wa bia katika bara zima la Afrika.
Kushoto ni Mtaalamu wa Utengenezaji Bia wa TBL, Cavin Nkya ambaye ameshika cheti cha uzalishaji bora wa bia ya Castle Lager na Kulia ni Meneja wa Ubora Kiwanda cha Bia cha Mwanza, Caroline Mhonoli aliyeshika cheti kilichoambatana na tuzo ya uzalishaji bora wa kiwanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hizi habari zenu nusu nusu wakati mwingine zinazengua kinoma.

    Hiyo tuzo maana yake nini?

    1: Imetolewa na nani au taasisi gani?

    2: Mshindano hayo yalifanyika wapi na yalishikisha kina nani au viwanda gani vingine na vya nchi gani?

    3: Walitumia vigezo gani kupima ubora (quality) Kwamba Castle Lager za Kiwanda cha Mwanza kwamba zinalevya zaidi ya Castle Lager za viwanda vingine Afrika? Au?

    4: Hivi Castle Lager haina aina moja ya formula kwa Castle Lager zote zinazozalishwa pengine popote kule?

    5: Isije ikawa tuzo hii ni kama ile tuzo iliyotolewa na wafanyakazi wa Barrick Mines kule Kahama. Yaani ni kwenda tu kununua kombe na kutengeneza cheti halafu mnapiga picha na kutuwekea kwenye globu yetu ya jamii.

    ReplyDelete
  2. Calvin Nkya, my dearest friend, ex-Tambaza na ex-Megalopollis... LOL!!

    Double D

    ReplyDelete
  3. Mnapopongezana kwa kuzalisha ulevi kwa wingi msisahau na yafuatayo nayo pia kama mna akili timamu ni lazima muyajadili:

    1. Ajari zilizosababishwa na ulevi wa madereva
    2.vifo vingi vilivyotokana na ajari hizo
    3. Vilema vya kudumu/muda kutokana na ulevi
    4. Ndoa/familia zilizovunjika sababu ya ulevi mliowauzia
    5. Watoto wa mitaani waliotokana na ndoa/familia kuvunjika sababu ya ulevi huo
    5. Uzinzi uliosababisha UKIMWI sababu wazinzi walikuwa wamelewa pombe zenu
    6. Ukosefu wa Elimu sababu baba/mlezi ni mlevi wa pombe zetu hivyo hana habari na familia
    7. Umasikini sababu ya Pombe zenu katika jamii
    8. Watoto wa zinaa/wasio na baba maalumu sababu ya ulevi
    9. Njaa - sababu badala ya kulima mazao ya chakula watu wanalima nafaka kwa ajili ya kuzalisha pombe
    10. HAYO YOTE YABADILISHE KATIKA PESA HALAFU HESABU HIYO NI HASARA LINGANISHA NA UJINGA MNAOIITA FAIDA HALAFU "WENYEWE MPIME" HUKU MKIJUA KESHO KUNA AHERA NA KILA MMOJA ATAWAJIBIKA KWA ALIYOYAFANYA!!!

    ReplyDelete
  4. Yes C. Nkya Tambaza A'level graduate year 1994. Keep it up

    ReplyDelete
  5. TUJULISHENI MASHINDANO HAYA YALIFANYIKA WAPI, LINI NA NCHI NGAPI ZILISHIRIKI NA KUWEZA KUMPATA MSHINDI MMOJA TU AMBAYE NI TANZANIA!
    USANII WA KIBIASHARA SI MZURI KWANI SASA HIVI SOKO LA BIA YA SERENGETI NI TISHIO KUBWA SANA KWA TBL.

    ReplyDelete
  6. Endeleeni kujipa moyo eti washindi wa tuzo wakati serengeti inawapeleka sokoni kishenz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...