Mashekhe wa mkoa wa Kigoma wakijumuika katika futari ya mwisho jioni ya jana iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mjini humo
Kinamama wakifurahia mashine ya kukamulia mawese iliyotolewa na kampuni ya simu ya Vodacom kwa kikundi cha kina mama cha Jacosuta wilayani Kigoma .wa pili kulia ni Manager Wa Vodacom Foundation Bw Yessaya Mwakifulefule na wa pili shoto ni Afisa Uhusiano wa Vodacom Foundation, Mwamy
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh John Mongela akiwa tayari kukabishi misaada mashine ya kukamulia mawese iliyotolewa na kampuni ya simu ya Vodacom kwa kikundi cha kina mama cha Jacosuta wilayani Kigoma .Wanaoshuhudia ni Manager Wa Vodacom Foundation Bw Yessaya Mwakifulefule na Naibu Mufti Mkuu. Pamoja na msaada huo kampuni ya simu ya Vodacom pia ilifuturisha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu mkoani kigoma.
Mh John Mongella akigawa vifaa vya shule kwa watoto yatima hao

Naibu Mufti Mkuu akipokea msaada wa vyakula vya kwa niaba ya watoto yatima kutoka kwa Manager Wa Vodacom Foundation Bw Yessaya Mwakifulefule .Pamoja na msaada huo kampuni ya simu ya Vodacom pia ilifuturisha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu mkoani kigoma.anaeshuhudia makabidhaiano ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh John Mongela

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh John Mongela akipokea msaada wa vyakula vya kwa niaba ya watoto yatima kutoka kwa Manager Wa Vodacom Foundation Bw Yessaya Mwakifulefule .Pamoja na msaada huo kampuni ya simu ya Vodacom pia ilifuturisha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu mkoani kigoma

Manager wa Vodacom foundation Yessaya Mwakifulefule Akihutubia wageeni wallikwa katika futari iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya Vodacom Kwajili ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu Mkoani Kigoma
sehemu ya kinamama wa Kigoma walioalikwa kwenye hafla hiyo
qasda ikisomwa wakati wa hafla










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. masheikh kwenye mambo ya maakuli tu huwatoi hao ona kanzu zao na vibaghalashia vyao hivyo hehe...

    ReplyDelete
  2. anony wa kwanza asante kwa kuyatoa hadharani ambayo huwa unayaficha moyoni mwako,
    na pia kutuonyesha kiwango chako cha akili na uelewa.
    Inshaallah siku moja Allah(SW)atakuongoza katika njia iliyonyooka.

    ReplyDelete
  3. AMEEN! huyo mdau wakwanza nadhani si muumini wa dini yeyote! Huna adabu wala heshima, mara ngapi tumeona masista na maaskofu wanapokea misaada au wapo kwenye tafrija na huwezi kuona mtoto wa kiislamu anadharau viongozi wa dini namna hii. Siajabu huyu mtu hata siku moja hajafunga from surise to sunset. Kwanza unazungumzia watu wliofunga! Allah tunakuomba umnusuru huyu mja wako mpotevu!

    ReplyDelete
  4. Mtuma maoni wa kwanza ulikuwa huna haja ya kuandika upuuzi wako huo wa kijinga na kitoto Tanzania ni nchi ambayo ina ushirikiano wa ajabu sana katika masuala ya dini ndio maana utakuta wakristo wanasheherekea Eid na waislamu wanasheherekea Krismas sasa kama unawachukia sana waislamu si bora unyamaze tu au kama una ubavu nenda msikitini ukawaambie wenyewe uso kwa uso halafu uone watafanyaje. Uhuni mwingine hauna maana hata kidogo sijui mwenyewe unafikiria ni sifa. Dunia hii kama huna la kusema funga kinywa chako utakuja kujikuta pabaya siku moja kwa ujanja mwingi.

    ReplyDelete
  5. Hongereni Vodacom kwa kufuturisha katika mwezi wa Ramadhani. Kwa hakika mmefuturisha sana mwezi huu. Ila sasa mbona hao Masheikh hawaondoki hapo mbele japo weshapakua?? Yani wananywea uji hapo hapo???

    ReplyDelete
  6. VODA WANGEWASAIDIA ZAIDI WANAKIGOMA KWA KUNUNUA MAFUTA YA MAWESE WAYATENGENEZAYO BADALA YA KUNUNUA TOKA KWENYE VIWANDA VIKUBWA WAKATI HUOHUO WANAWAPA MSAADA WA MASHINE YA KUKAMULIA MAWESE, WAKAMUUZIE NANI WAKATI VODA WANASHINDWA KUYANUNUA?

    ReplyDelete
  7. Binadamu kweli hajui kushukuru, akipewa kidole anataka mkono mzima!!

    Sasa Vodacom inunue mawese iyapeleke wapi na kuyafanyia nini? Yaani kisa imeamua kusaidia basi kila kitu ifanye Vodacom tu? Wewe unayesema ingenunua mawese unafanya nini? Vodacom imeshawasaidia kuweza kuyakamua, nawe saidia kwa kuyanunua, nyambaf...au kaa kimya!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...