miss TZ 2008 Nasreem Kareem alonga na globu ya jamii juu ya haya na yale...Fainali za Miss TZ 2009 zinafanyika Ijumaa hii ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo Nasreem atakabidhi taji lake kwa Vodcaom Miss TZ 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mahojiano mazuri,kila la kheri mrembo katika malengo yako.Kaka Michuzi hivi kila mtu anagombea Ubunge?Ni nini sifa za msingi katika kugombea Ubunge?

    Hawa vijana wadogo na wenye vipaji tuwahamasishe kujenga vipaji vyao kwa kwenda shule,badala ya kuwaingiza/kuwahamasisha ktk masuala ya siasa ambayo mara nyingi yanakuwa masuala ya muda mfupi.

    ReplyDelete
  2. Jamani bongo warembo interview huwa hawatrainiwiiiiiiiiii???yaani ovyo kabisaaa,ningewashauri waandaaji wa mambo ya urembo kuwafundisha warembo jinsi ya kujibu maswali...na sio tu kucheka cheka bila mpango na usista duu mwingi..Naomba kuuliza hivi kumbe Temeke na Ilala ni kanda na sio wilaya????yaani interview nyingi tu tena watu maarufu wa bongo huwa ni hati hati....watu lazima waelewe mahojiano sio tu unakurupuka na kufungua kinywa..nchi zilizoendelea huwa watu maarufu au mamiss lazima wapewe shule kabla ya kuongea na vyombo vya habari.....
    Miye langu ni hilo tu....
    Asante kaka Michuzi,nakutakia vekesheni njema...

    ReplyDelete
  3. Mimi nataka awe president!!!

    ReplyDelete
  4. michuzi namkaribisha sana aje kusoma huku udosini elimu cheap sana na kwavile aitaji makuu huku kuna mtoa sana kwa hiyo fani yake maana wadosi wanamaswali mengi sana kwahiyo yanaweza kumsaidia katk maojiano hasa akiwa diplomat leader
    pili hivi warembo mbona wanaishia kimya kimya sana atuoni hasa yale mafanikio wakishapata magari na mwaka kuisha ndio basi atuwaoni tena kusaidia jamii
    mdau

    ReplyDelete
  5. yule aliyebeba mbuzi mgongoni si ni joni mashaka

    ReplyDelete
  6. nasreem nenda na joni mashaka mkagombee ubunge, mtapata kura zetu

    ReplyDelete
  7. HAYA MAMBO NI VIPI?
    KUNA WATANZANIA TUMEISHI NJE KWA MIAKA KIBAO, LAKINI TUZUNGUMZAPO KISWAHILI CHETU KINAKUWA NYORORO WALA HATUSITISITI WALA KUCHANGANYA LUGHA.
    HIVI NI NINI HICHO KINACHOPELEKEA WATU KAMA HAWA WAIOTWAO WAREMBO KUSHINDWA KUKIMUDU KISWAHILI VIZURI?
    NI NYODO AU KUJIONA?
    AU UBWEGE WA KUIPONDA LUGHA YAO YA TAIFA?
    TENA HAWA WAKO WENGI MNO, SIJUI WANA MAANA GANI?
    INANICHUKIZA SANA BINAFSI, KWANI NINATAMANI KUONA WATZ WENZANGU, HASA WANAOTEGEMEWA KULIWAKILISHA TAIFA NJE YA NCHI, KUKIENZI KISWAHILI CHETU NA KUKITANGAZA.
    SHOMBO HILI LA UBISHOO USIO NA HEKIMA WALA TAFAKURI LITAISHA LINI?
    NI LINI KILA MTANZANIA ATAONA THAMANI YA LUGHA YETU ADHIMU KAMA WENGINE WANAVYOTHAMINI LUGHA ZAO?
    NDIO MAANA MIMI NA MASELEBRITI WENGI WA KITANZANIA MBINGU NA ARDHI.
    WENGI HAWAJUIA THAMANI YAO, NI VIBARAKA NA MABWEGE, HAWAJUI THAMANI YAO.
    ULOFA MTUPU!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  8. Wewe una sema haujaona mafanikio ngoja nikupe mafanikio.

    Anina Maieda- Kaolewa na Mzungu

    Emilly Adolf Kaolewa na Mzungu

    Shose Sinare - Kaolewa na Mzungu na kuafungua shule

    Saida Kessy - Kaolewa na tajiri

    Basila Mwanukuzi - Yuko UN huko Ethhiopia

    Hoyce Temu - Kutokanana Umiss alipata kazi na kupata scholarship kusoma USA nakuipeleka fammilia yake na Kupata kazi Standard chaterd bank na kuolewa na Tajiri wa Kizambia.

    Jaquline Ntuyabaliwe - Nusu alolewe na mtoto wa kigogo mmoja ni mrembo mwenye mvuto na sura nzuri kuliko wote ,Kwa sasa ni Mwanamziki mkubwa( Album zote nzuri na quality ya CD zake ni kubwa ) na ana miliki kampuni yale ya mambo ya vikorombwezo vya ndani ya nyumba.

    Happiness Magese - Huyu amefanikisha ndoto zake za kuwa International Model ,kwa sasa anajulikana kwa jina la Millen , yuko south Africa kikazi na amesha saini mkataba mnono na ku hamia kufanya kazi zake jijini New York ,USA

    Angela Damas - Ali maliza chuo kikuu na kupata shahada yake na kutapa kazi TIGO na sasa kaajiriwa kwenye NGO moja kama bosi

    Sylvia Bahame - Huyu Mwanadada wa kwanza katika historia ya umiss Tanzania kuweza kuwakilisha TZ akiwa kama plus size model ,yeye ali graduate Universiti na ana digirii.

    Faraja Kotta - Huyu Mrembo aliye na body la mvuto sana na smile inayo mtoa nyoka pangoni, yeye sasa ni Bosi wa shirika moja la kusaidia mambo ya UKimwi na kaolewana Mbunge Lazaro Nyalandu

    Nancy Sumari - Huyu dada aliwakilisha vema TAnznaia kwa kuweza shika taji la Miss Africa kwenye Miss world na kuingia Top 5,dada wa kiarusha , sasa hivi ni Mkurugenzi kwenye company yake ya kuandaa makongamano na matamaja pia ni muandaaji wa vipindi vya Televishen

    Wema sepetu - Huyu Mrembo ,mwene majibu mazuri na akili nyingi kwa sasa ni Msanii wa Maigizo ya filamu (Video mana hatujafika kwenye flamu) na ana nafasi nzuri sana kuweza kufanya lolote kubwa ila anahitaji uangalizi mzuri wawatu alio karibu nao.

    Richa Adhia - Huyu dada aliweka Historia kwakua Miss Tz wa kwanza mwenye asili ya Acia , dada amabye ni so Intellegent yeye ni msanii na pia ana matarajio mengie kwenye future.


    Nasreem Kareem - Huyu ndie Miss Tz wa sasa ambaye anamaliza muda wake siku chache zijazo, kwa kazi nzuri aliyo fanya akiwa kama Miss Tanzania tutegemee makubwa toka kwake na tuna mtakia kila la Kheri.





    Jamani ee Kuolewa na Mzungu ni dili kwa wengine na si dili kwa wengine ala!

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 05:05 thanks kwa kutupa positive updates za warembo wetu waliopita,nawatakia na mimi kila la kheri na mafanikio katika hizi mbio za maisha!

    ReplyDelete
  10. KUOLEWA NA MZUNGU?.....KWELI UTUMWA HAUTOMTOKA MTU MWEUSI.....NAONA WAANZISHE MISS INTELLIGENT HUKO MASHULENI ILI APATE SCHOLARSHIP... NAFASI YA MWANAMKE KTK JAMII YA KITANZANIA BADO IKO CHINI SANA

    ReplyDelete
  11. TUNATAKA FAIDA KTK JAMII SIO FAIDA ZAO BINAFSI.........

    ReplyDelete
  12. Faida nyingi zipo na sio lazima zisaidie watu wengi kwa pamoja na zipo ambazo hazionekani lakini zimefanyika .
    Mfano kamati ya Miss TZ imeweza kuwapa ajira watu wengi.
    Imeweshesha kutoa misaada kwa jamii mfano watoto yatima na mengine.
    Kikubwa ni kuweza kuwafanya wasichana kuweza kujitambua kua urembo ni kipaji na kama kipaji unaweza kukitumia kukusaidia na pia kuwasaidia walio pembeni yako.

    Kuweza kushika taji au hata kushiriki tuu kuna weza kukubadilisha maisha yako yote na unapo badilika maisha kwa mlengo mzuri lazima utakua na msaada kwa jamii kwa namna fulani , inawezakua moja kwamoja au kwa namna nyingine yeyote ,mfano mmoja ni kuajiri .

    ReplyDelete
  13. Hiv kaka michuuu,hawa warembo wa mwaka huu mbona vimeo wote?ndo waliowapa vizuri majaji? yaani mingine katunisha miziwa utandani kackia ni mashindano ya maziwa.tumechoka kununua sura cz hao ni wauza sura tuuu jamaniiiiii

    ReplyDelete
  14. Mbona mbaya hivi aliupataje umiss? Au ameharibika baada ya kuwa ameshaukwaa na mapedeshee wamemmchosha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...