wasanii mbalimbali wakiongea juu ya kifo cha medi mpakankanjia mara tu baada ya mazishi yake leo katika makaburi ya kisutu jijini dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. shuleshule tu kati ya hao wasanii kanumba peke yake kaongea maneno ya kueleweka.

    ReplyDelete
  2. KANUMBA KICHWA SEMA TUU IKIJA KINGEREZA JAMAA ANAISHIWA POINT, WE ACHA TUU. UPANDE WA MED KWELI AMEWATOA SANA WASANII WOTE HAO MPAKA VICK KAMATA NASHANGAA HAJAHOJIWA AU HAKUJA MSIBANI.

    ReplyDelete
  3. mzee wa songea(UK)September 16, 2009

    hapo ndo tunapoona nafasi wazi(gap)kati ya serikali na maendeleo ya sanaa katika nchi yetu mpaka wanatokea watu wanakuwa kama taasisi kufanya yale ambayo serikali ingeweza kufanya. kwenye nchi masikini kama ya kwetu lazima uwezo mdogo wa serikali utumike kukuza vipaji ili baadae serikali hiyohiyo ije kufaidika na maendeleo yake.sasa watakuambia wao kazi yao ni kutunga sera na kuzisimamia, hizo sera zinatungwa mpaka lini kwa nini sasa wasihamie kwenye kuzijaribu zilete faida kwa jamii!!?ningefurahi kama bajeti moja ya serikali ingetenga fungu la kuwapa uwezo hawa jamaa warecord kazi zao zikilipa watarudisha maana soko letu la sanaa bado ni changa hivyo hata wakifanya kazi nzuri hailipi na hilo sio kosa lao!!hiyo itaepusha mafisadi kujificha kwenye kuwasaidia wasanii wetu maana hawakawii kuandaa tamasha na kumualika Rais na kupeana naye mikono kumbe duu DAWA ZOTE HOSPITALI ZIKIIBIWA ANAPELEKEWA YEYE KUZINADI.

    ReplyDelete
  4. inasikitisha sana,
    hasa ukizingatia jinsi alivyoweza kuwa daraja la mafanikio kwa wengi.
    Haikuwa nyumba ya pekee tanzania/dar/sinza kwa uzuri..ila ilikuwa ni nyumba ya mtu mwenye nia safi na lengo la kuwafanya wasanii washindwe wenyewe kuvaa husika lakini wasikose stage ya kufanya kazi yao.
    ina lillah wa inna illayhi rajuun..mungu awalaze pema peponi na marehemu Amina na mwisho fadhila bado zaweza kuelekezwa kwa mwana wao Rahman..hasa wasanii, toeni fadhila zenu huko.

    ReplyDelete
  5. Wewe anon wa 11:40 vp wewe, mbona una wivu na Kanumba kiasi hicho?? kwani ulinyimwa na nani kujishughulilsha na wewe ukafanikiwa eti unaendelea kumsema kuwa ingekuwa english angechemka, unajua english au kupayuka tu. Hivi lugha ya Tanzania ni english au ni kiswahili hebu tujivunie lugha yetu, wazungu wenyewe wanachemsha kiswahili kama nini mbona hamuwacheki,kwanza ni wachache sana wanajua hata cha salam.
    Leave Kanumba alone mind your own business, it seems like you don't have anything better to do.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wafiwa. Hivi huyu Mpakanjia alikuwa na wadhifa gani? kwani inaelekea ni mtu maafuru sana Tz, na wasanii wote wanasema wamesaidiwa na yeye??

    ReplyDelete
  7. Medi my bra, wasanii wengi wanashukuru jinsi ulivyowasaidia na umeondoka peke yako, sijui maandalizi gani ulifanya but i wish ungejenga walau kisima, madrasa...zaidi ya kuwaendeleza watu ambao hawatakuwa msaada kwako siku ya hesabu.
    Waumini wenzangu wenye uwezo, jiandaeni na siku ya hesabu...sifa za ulimwengu hazitotunufaisha. Hao wasanii wote wanaosema Medi kawasaidia, hakuna ata mmoja atakae jitolea kuwalipia ada ya shule walau muhula mmoja watoto wa Medi, hii inatufundisha nini?

    ReplyDelete
  8. we pull him down je unajua yote aliyoyafanya medi wakati wa uhai wake? au sababu hakuyatangaza? mie binafsi siyajuwi yote ila hata kuwasaidia wasanii ni hisani mojawapo.
    kwa mfano wewe umeshajenga visima na madrassa ngapi? usisingizie uwezo manake hata elfu moja unayoitumia kwenye internet cafe yatosha kununua juzuu!
    tafuta mtu akusimulie mfano wa sadaka ya tajiri na yule mwanamke mjane katika agano jipya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...