
Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya rege na muziki wa dansi mwenye makao yake Oslo, Norway, Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi, kwa hivi sasa anapanga safu kali kwa ajili ya ziara ya miji sita Norway.
Ziara hiyo itakayoanza Kongsberg tarehe 23 Oktoba itamalizikia jijini Trondheim 7 Desemba. Kikosi cha Ras Nas kinachanganya wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast, Norway na USA.
Wabongo wa Norway habari ndiyo hiyo! Mwezi wa Desemba Ras Nas na bendi yake watatembelea miji ya Galle na Colombo Sri Lanka kuwasilisha Norway, (ofkozi na Tizedi) katika tamasha la muziki. Kwa habari zaidi fuatilia
Asanteni kwa kusoma habari hii.
Kongoi Productions
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...