Bro Michuzi,
Pole na kazi, vijana wako wa Jake Productions pamoja na kundi zima la BABY POWDER tulibahatika kukutana na Bolozi wa Tanzania ndani ya USA Mh. Ombeni Sefue, akiwa pamoja na mwandishi mkongwe wa vitabu Bw.Elvis Msiba (wa Willy Gamba).
Tunapenda kumshukuru Mh. Balozi kwa ukarimu wake kwani pamoja na mvua kali alichukua muda wake kutusikiliza na hata kupiga picha na sisi!! Yaani ni mtu simpo ila kichwa ile mbaya. kwa kweli hapa tuna balozi.

Tafadhali angalia Trailer II
ama tembelea
www.babypowderthemovie.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mwili umenisisimka niliposikia jina Elvis Musiba na Willy Gamba,ama kwa hakika huyu mwandishi alikuwa akitupa raha sana enzi zetu zile maana utamu wa hadithi zake ni kuzidi baadhi ya movies kibao tu nashangaa kwanini sikuhizi amekuwa kimya sana.Mdau mwenye data zake alipo huyu bwana na atuhabarishe si vibaya tukijua pia anafanya nn na je kimya chake kina mshindo au???

    ReplyDelete
  2. atleast wangevaa vizuri au balozi asinge piga picha nao.hamna heshima hapo hata kwa wazungu hamna hiyo kwa kiongozi kupia picha na pajazzzz labda sijaona.heshima hupotea.

    ReplyDelete
  3. kwani kuna ubaya gani kwa wao kuvaa hivyo. hakuna ubaya wowote kwa balozi kupiga nao picha. hii sio nchi ya talaban. MKENYA

    ReplyDelete
  4. Mzee Musiba alivutiwa na juhudi za dhati za vijana wa Baby Powder na akapendekeza Waifanye movie ya Kisasi (Willy Gamba) kuwa project inayofuatia. Mazungumzo zaidi yatafanyika na mtajulishwa! Kwa ufupi tu huyo ndio mzee Elvis Musiba na Baby Powder!

    ReplyDelete
  5. HUYO MWANDISHI ANAITWA MUSIBA NA SI MSIBA , ELIMU YETU INAUTATA KWELI.

    ReplyDelete
  6. WEWE 11:24:00 HIZO SIO PAJAZZZZ INAELEKEA UNAIGA TU. WAPO WAAFRIKA WENGI TU IKIWEMO WATANZANIA WANAOVAA NGUO ZINAZO ONESHA SEHEMU NYETI ZAIDI YA HIZI AMBAZO NI ZA KAWAIDA TU NA HAZINA UBAYA. HATA HIVYO NI VIZURI NAWE UMESHIRIKI KUTOA MAONI KWENYE BLOGU YA JAMII.

    ReplyDelete
  7. wabongo kwa kuponda bwana....
    anyways,,,,baby powder iko juu tena juu.
    i see you warda...go girl!

    ReplyDelete
  8. Waziri kavaa suti Hao WamariTZ na vichupi!!!!! au ndio maendeleo utamaduni wa kitanzania upo wapi hapo. Loh vijana wekeni heshima kwa wakubwa zenu

    ReplyDelete
  9. Balozi mwenyewe anafurahia pajazzz.

    ReplyDelete
  10. good job guys.....i can't wait for the movie to be out.wawaaa jake production.BABY POWDER is the bomb!!

    ReplyDelete
  11. HAWA KINA MAKABWELA BWANA WAKIFIKA HUKO MAJUU NDIO WANAJIFANYA KAMA WAMEZALIWA HUKO

    NDIO NINI SASA KUONYESHA UPAJA UPAJA WENYEWE UNA MADOADOA KAMA CHUI HEBU FUNIKENI HUO USAFIRI WENU WA KUPANDIA MILIMA YA KULE KWENU

    MKUU WA KITONGOJI HEBU WAWEKEE HII WAIONE KESHO WASIRUDIE KUWEKA UPAJA WAO NJE YA KADAMNASI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...