JK akikabidhi usafiri aina ya Bajaji kwa mwanamkw mlemavu Sara Mageni Sanga aliyekaa chini katika kijiji cha Lupalilo,Wilayani Makete,mkoa wa Iringa jana jioni.Pembeni ya Rais kulia ni mkuu wa mkoa wa Iringa Bwana Mohamed Abdulaziz
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 28, 2009, ametoa pikipiki aina ya Bajaj kwa mama mlemavu mmoja wa kijiji cha Lupalilo, Wilaya ya Makete, Mkoani Iringa, Bi. Sarah Mageni Sanga, ili kumsaidia usafiri.
Aidha, Rais Kikwete amemkabidhi mama huyo mjane risiti ya benki ya sh milioni mbili, ili zimsaidie katika kupanua duka lake dogo ili aweze kujipatia mahitaji yake ya maisha kwa uhakika zaidi. Fedha hizo zimewekwa kwenye akaunti yake katika Benki ya NMB.

Rais ametoa msaada huo kwa mama huyo wakati aliposimama kwenye kijiji hicho cha Lupalilo jioni ya leo, akiwa njiani kwenda mjini Makete, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mkoa wa Iringa. Ziara hiyo ya siku nne inamalizika kesho, Alhamisi, Oktoba 22, 2009.

Bi. Sanga ametokwa na machozi wakati anapokea msaada huo wa Rais mbele ya umati wa wanakijiji wenzake pamoja na watoto wake wawili akimwambia Rais Kikwete:
“Mungu akubariki na akujalie uendelee kuwa na moyo wa namna hii, ili uweze kuwasaidia wengine wenye ulemavu na wajane kama mimi.”
Mama huyo amefiwa na ndugu zake wote pamoja na mume wake, na hivyo pamoja na ulemavu wake wa miguu, anaishi na watoto wote wa ndugu zake ambao anawatunza.

Anaishi na watoto sita, wawili wa kwake na wanne wa marehemu ndugu zake. Mtoto wake wa kwanza yuko kidato cha tatu na wa pili yuko darasa la saba na wote wawili ni watoto wa kike.

Akimkabidhi mama huyo msaada huo mbele ya duka lake dogo, Rais Kikwete amesema kuwa alipata habari za mama huyo wiki iliyopita kwenye Kipindi Maalum kiitwacho Sharaja kwenye Televisheni ya Taifa ya TBC1.

“Niliangalia kipindi kile, nimwona mama huyu anatembea kwa kutambaa na nikasikia jinsi ndugu zake wote walivyofariki kwa maradhi haya, na nikawaelekeza washauri wangu kuniandalia msaada huu. Kwa kuwa nilijua nakuja huku, niliamua kuukadhi mimi mwenyewe kwako,”amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete pia amemwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Makete, Hawa Ng’humbi kuhakikisha ama anampatia mama huyo dereva wa kuendesha Bajaj hiyo, ama kuhakikisha kuwa mama huyo anafundishwa mwenye kuendesha.
Rais pia amemkabidhi Mkuu wa Wilaya huyo hati zote zinazokamilisha miliki ya Bajaj hiyo kwa Bi. Mageni ikiwamo risiti ya ununuzi, kadi ya pikipiki, usajili wa pikipiki hiyo, shughuli ambazo kwa jumla zimegharimu sh milioni nne.
Rais amezikahakiki hati zote kabla ya kuzikabidhi akiwachekesha wanakijiji kwa kusema: “Hebu kwanza nizihakiki hati hizi. Nchi yetu imekuwa na wajanja wengi ambao wanaweza kuja kukuletea matatizo baadaye.”

Kuhusu msaada wa sh milioni mbili, Rais amesema kuwa ametoa fedha hizo kumwezesha Bi. Sanga kupanua duka lake, kusomesha watoto wake, na kuendesha shughuli zake nyingine kwa uhakika zaidi.

“Na fedha hizi tayari zimewekwa kwenye akaunti yako ya Benki ya NMB, tawi la Mkwawa, mjini Makete,” amesema Rais Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kumradhi, lakini nafikiri hatua imekuwa kubwa sana kuliko hali halisi, nani atakuwa anagharamia mafuta ya hiyo bajaji? Au halmashauri? Na kama ni halmashauri, basi iwe standing order kweli kweli ya yeye kwenda kujaza mafuta kwenye kituo kilichopangwa, vinginevyo...tutayasikia tu.


    ooh halmashauri haina pesa,..bajaji juu ya mawe, then back to square one!

    ReplyDelete
  2. hao wengine wanajidai kushangaa nini ina maana hawajui bajaji??

    ReplyDelete
  3. wadau hapo juu mskonde kuhusu swala la mafuta mwenzenu ataikodisha iwe inamletea mapato piga ua ndo itakavyokuwa

    ReplyDelete
  4. hao wangine wanaijua vizuri bajaji sema wanatafakari huyo atakaye kuwa anai-service.

    ReplyDelete
  5. Hongera mama mlemavu, lakini tunajua JK hizo ni mbwembwe za kuelekea uchaguzi..huna lolote!! utajidai hayo ndo maisha bora kwa watanzania wakati mama mwenyewe hakawii kuuza hicho kibajaji anunue mafuta..ha ha ha kazi kwelikweli!

    Michu hata ukiibana....

    ReplyDelete
  6. nyie wadau mnaobeza msaada huo poleni maana bora hata yeye aliyetoa bajaji kuliko nyie ambao hata fungu la kumi huko kwenye imani zenu au maulidi hamfanyi bora yeye baba JK ubarikiwe... unauliza kuhusu mafuta je umesikia walemavu hawafanyi biashara yoyote? je bajaji hawezi fanyia biashara ??? kuwa na busara

    ReplyDelete
  7. KWA MAONI YANGU NAFIKILI WALEMAVU WAPEWE MFUKO WAO WA KUWASAIDIA WOTE NCHI NZIMA NA KAMA BAJAJI WAWE NAZO WOTE ITAWASAIDIA SANA KAMA HIVI KAMPA MMOJA JE WENGINE PIA NAO NI WALEMAVU NA WAO NI WATANZANIA PIA NA WANAHITAJI MSAADA KAMA HUO KWANI HELA ZA MADINI,SAMAKI,KODI NA MBUGA ZA WANYAMA MILIMA N.K ZINAENDA WAPI? RAIS KAFANYA VIZURI SANA KUONA KUWA HAO WATU WANAHITAJI MSAADA ILA WATU WA KARIBU YAKE WAMKUBUSHE KUWA WATU HAWA TUNAO WENGI NA NI NDUGU ZETU WANAHITAJI MSAADA WETU NADHANI TUTABALIKIWA KAMA TUTAJIFUNZA KUWAJALI WENZETU MA MWENYEZI MUNGU ATATUJARI PIA MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE
    AMAN

    ReplyDelete
  8. WOTE HAPA ZIRO. JE MNAJUWA VIBAJAJI ASILIMIA KUBWA VIMEKUJA TANZANIA KWA NJIA GANI?

    BAJAJI VIMELETWA KWA MSAADA IWE NI VIGARI VYA VILEMA NA OMBAOMBA ILI WAPUNGUZWE WAFUNDISHWE WAENDESHE BAJAJI WAJIPATIE PESA.

    SERIKALI WAMEFANYA UJANJA UJANJA WAMECHUKUWA WAMEUZA VENGINE WAMEWAPA WAKE ZAO KUFANYIA BIASHARA KWA KUTUMIA WATU WENGINE.

    NA KARIBIA VINAKUJA BAJAJI MPYA NA BADO WATAPEWA WENGINE VILEMA NDIO WANATAKIWA KUPEWA HIVYO WAFANYIE KAZI JAMANI TUPUNGUZE OMBAOMBA WAPATIWE KAZI. UKWELI NDIO HUO. PAZI

    ReplyDelete
  9. SAFI SANA MUHESHIMIWA RAIS KWA KIDOGO ULICHOTOA ILA NAPENDA KUKUPA ANGALIZO UNAPOKUWA UNAKUTANA NA WATU WENYE ULEMAVU KAMA HAO HASA WASIO NA UWEZO KABISA WA KUTEMBEA SI BUSARA KUWEKA MIKONO MIFUKONO MARA NYINGI HIYO INATAFSIRIWA KAMA RADHAU NAJUA SI KOSA LAKO ILA NI KUTOFAHAMU

    ReplyDelete
  10. Hongera Ndugu Rais na MUNGU AKUBARIKI!
    AMINA.
    Nami namwomba MDAU MICHUZI anitafutie contacts za huyo Mama au huyo Mkuu wa Wilaya [lakini bora hiyo akaunti ya huyo Mama] ili niweze name kuchangia na kutuma angalau Dola 50 kila mwezi.
    Mie ni Mlemavu pia ingawa huyu Mama amenizidi na anahitaji kila aina ya msaada na ndio maana nasikia uchungu sana.
    Mungu awabariki wote waliochangia hasa kwa kauli nzuri!
    Mdau wa Blogu Mamboz Motomoto ya Soka ya England ndani ya
    Bongoz!
    Storming
    Doha, Qatar

    ReplyDelete
  11. Mwalemi Sitso Imbaha, twita mwalemi kavile na kadatu Munu va Nguluve

    ReplyDelete
  12. NI AFADHALI HATA MR JAKAYA KUMFIKIRIA MAMA KAMA YULE.. "GIVE CREDIT WHERE IS DUE".. WENGINE HUWA WANAFIKIRIA LEO NIMEINGIZA MILLION NGAPI. SEREKALI YETU IMEWATUPA SANA WALEMAVU SI WATU WAZIMA NA HATA WATOTO... WENGI WETU HATUJUI WATU KAMA HAWA WANA SUFFER KIASI GANI...SI KIMAUMBILE PEKEE HATA KIAKILI..MHESHIMIWA RAISI MUNGU AKUZIDISHIE NA AKUPE MOYO VILE VILE WAKUTATUA MATATIZO KAMA YA KULE ZANZIBAR...KWANI KAMA UTAWEZA KUTATUA TATIZO NA UKAWA MWANA WA HAKI...NA ASILIMIA 70 TUZO YA "MO IBRAHIM" INAKUSUBIRI.

    ReplyDelete
  13. HONGERA SANAA MH. JK, NAKUPOKEZA PIA MZEE WA QUARTA, MICHIZI MPE CONTANCT HUYO, OK, SASA JK UNAMAANA HUWAANIA WATU WAKO WA KARIBU KWAMBA WANAWEZA MUINGIZA MJINI MAMA?TEH TEH TEH

    ReplyDelete
  14. Tarehe Fri Oct 30, 01:45:00 AM, Mtoa Maoni: MBOGELA, Jackson

    Gue swamba Mbogela, Okhomwaletsa thomwaletsaghe leno, ebalabala jitsenga ndali mwe! Ototemekhe sanga atie jitsenga osevo ghua lami, aaasue, leno ipaka elelo hamna khenu.

    Leno ekhetukhutukhu ekyo jelekhobidi kheve kya khejiji ili khesahedele avanu voni. Kwani avamwaikini pakhejiji apo volosu ghue,

    Thomwaletsaghe sitso

    Mkulima

    ReplyDelete
  15. Tarehe Fri Oct 30, 01:45:00 AM, Mtoa Maoni: MBOGELA, Jackson

    Gue swamba Mbogela, Okhomwaletsa thomwaletsaghe leno, ebalabala jitsenga ndali mwe! Ototemekhe sanga atie jitsenga osevo ghua lami, aaasue, leno ipaka elelo hamna khenu.

    Leno ekhetukhutukhu ekyo jelekhobidi kheve kya khejiji ili khesahedele avanu voni. Kwani avamwaikini pakhejiji apo volosu ghue,

    Thomwaletsaghe sitso

    Mkulima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...