RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa Serikali kwa kuteua Makatibu Wakuu wa Wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili, na kuteua Katibu wa Rais mpya.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2009, Ikulu, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Philemon Luhanjo, imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kufuatia kustaafu kwa baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara.
Aidha, taarifa inasema kuwa mabadiliko hayo yanaanza leo, Oktoba 19, 2009.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais.
Bwana Jairo anachukua nafasi ya Bwana Arthur Mwakapungi ambaye amestaafu.
Katika taarifa yake, Bwana Luhanjo amesema kuwa pia Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Salula alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Mbarak M. Abdulwakil aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Bwana Abdulwakil anachukua nafasi ya Bwana Patrick Rutabanzibwa ambaye anahamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kama Katibu Mkuu. Ndugu Rutabanzibwa anachukua nafasi iliyoachwa na Bi. Salome Sijaona ambaye amestaafu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia amemteua Bwana Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na Umwagiliaji.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, na anachukua nafasi ya Bwana Wilson Mukama ambaye ameanza likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Bwana Luhanjo amesema katika taarifa yake kuwa vile vile Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Anachukua nafasi Dkt. Florence Turuka ambaye anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kama Katibu Mkuu. Bw. Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi, ambaye anamaliza mkataba wake wa utumishi wa Serikali mwezi ujao, Novemba, 2009.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya Bwana Jairo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19 Oktoba, 2009

DUUH WAKRISTU WATUPU!! BADO JK ANASHUTUMIWA KUWA NI MDINI. JK LETE USAWA SIO VIZURI MAKATIBU WOTE DINI MOJA TU.
ReplyDeleteWatanzania tuacheni kuangalia mambo kwa kufuata dini. Huu si uungwana.
ReplyDeleteWatu wanatakiwa wateuliwe kwa kuangalia sifa zao. Hao jamaa hapo hakuna aliyeibuliwa kutoka kusikojulikana kama ilivyokuwa kwenye nafasi zingine hapo nyuma. Tuwe wakweli na tukubali kwamba kwa sababu za kihistoria tu, maeneo mengi nchini yenye shule ni yale yenye makanisa. Kadri nchi inavyosonga mbele ndivyo mambo yanavyojipanga kwa usawa. Si vizuri kulalamika. Wamishonari Wazungu walipokuja walijenga makanisa, hospitali na shule; Waarabu walijenga misikiti na maduka; hii imeathiri muundo wa taifa letu. Sidhani kama unaweza kulinganisha mathalani jinsi Uchagani kwa Wahaya kulivyo na mahali kama Kilwa Masoko au Kilwa Kivinje, hata mkoa wa Pwani, ukiondoa shule chache za serikali, zilizobaki zilijengwa na mapadri. Tukubali historia, tuache kulalama kwani hata viongozi wetu wa kwanza wa taifa karibu wote walisoma shule za Wazungu Wakristo.
Hakuna anayetuonea Waislamu, na ndiyo maana Nyerere alitaifisha shule za Wakristo ili Waislamu nasi tusome. Muulizeni Yusuf Makamba alisoma wapi, mwenyewe anasema kama si Wakristo asingefika hapo alipo. JK mwenyewe alisoma shule za Wakatoliki awali na alishawahi kusema hadharani.
Tujengeni taifa letu kwa misingi ya utu na maendeleo na umoja, tuache kabisa huu wimbo wa udini. Hakuna hata mtu mmoja atakayefaidika na vita vya kidini au mgogoro wa kidini. Tukomae, Tanzania hii ilijengwa na Nyerere na Karume bila kubaguana, tusiibadilishe.
Michuzi naomba uweke, mimi ni Mwislamu, lakini inabidi kuelezana ukweli. Tusiharibu nchi hata kidogo.
Asanteni Watanzania wenzangu.
Kitu cha kwanza nilichotafuta kwenye orodha hii ni kama kuna mtuhumiwa wa ufisadi kapewa ulaji.
ReplyDeleteKuja kucheki comment kumbe kuna wadau kitu cha kwanza walichofanya ni kuotea dini za watu. Hii ni aibu kubwa.
Big up mdau wa pili. Tusiendekeze kulalamika tu wakati historia yetu imetuweka tulipo. JK aliingia Ikulu kwa ushindi wa tsunami kwa sababu 'Watanzania', sio watu wa imani fulani fulani za kidini walimpigia kura kwa kuamini atatufikisha tunakotaka kwenda. Kama atafanikiwa kufanya tulichokitarajia au la haitakuwa kwa sababu ya imani yake ya kidini, itakuwa kwa sababu ya uwezo wake.
JK hashutumiwi kwa udini, JK anashutumiwa kwa kuendekeza ushkaji kwenye kuendesha nchi.
Wewe anon. wa 10.01pm acha kubabaisha watu wewe ni kibaraka wa wakristo, unataka kunambia tanzania nzima kwa sasa wamekosekana waislam hata watatu kuweza kupewa hizo nafasi za ukatibu, acheni hizo, tatizo kiongozi wetu haoni mbali and he is incapable of making big decisions and Tanzanians are now sick of bieng heckled and bullied over the way he runs the country!
ReplyDeletewewe mdau uliyesema kuwa waislam wako nyuma sababu za kihistoria sio kweli.
ReplyDeletemara kadhaa wamechaguliwa wakuu wa wilaya wa kikristu wenye elimu ya kidato cha nne, jee hakuna waislam wenye elimu ya kidato cha nne kuwa wakuu wa wilaya?unasema tujihadhari na udini ili tusiingie kwenye vita vya udini njia moja wapo ya kujihadhari na vita ni kugawa nafasi sawa ili kuondoa masikitiko kama haya.kama waislam hawajasoma Professor Hamisi Dihenga alitoka wapi?ukitizama vyama vya siasa kama Cuf kina mwenyekiti ambaye ni professor Lipumba kama waislam hawakusoma kina Lipumba wasingekuwepo.
unajua kuwa rekodi aliyoweka Lipumba chuo kikuu hadi leo haijavunjwa?Professor Abdallah Safari aligombea uenyekiti wa CUF akishindana na Professor Lipumba.niambie lini ChADEMA kilikuwa na mgombea mwenye elimu ya Phd?Nccr au Tlp?unataka kuniambia kuwa hakuna muislam mwenye elimu ya kidato cha nne kama ya mkurugenzi wa shirika la utangazaji?
hivi unafahamu kuwa Professor Mtulia ni bingwa pekee wa moyo hapa Tanzania kwenye fellow yao ni yeye na DR.Hussein Mwinyi tu?
naomba hawa walioteuliwa wana sifa gani ambazo waislam hawana? ndugu yangu dawa ya matatizo ni kuyazungumza kuya address sio kunyamaza na kusema kuwa kuna sababu za kihistoria.
udini upo lazima tuukemee.sio fair kuwajaza wakristu watupu eti ndio wamesoma.
kwani hata wakiwa wakristo au waislamu tatizo liko wapi?? kwani mmeambiwa hizo ofisi zitageuka misikiti au makanisa?? acheni hizo nyinyi watu mnaong'ang'ana na dini kila kukicha akili zenu zimeganda acheni upuuzi wenu eboh!
ReplyDeleteJamani tuacheni udini, hao walochaguliwa mbona walikuwapo toka awali na ni kwa elimu zao hakuna aliyepachikwa, msitake kumchanganya JK wa watu ila analofanya liwe ni lawama tu kwake.
ReplyDeleteAma kweli kazi ipo, badala ya kuangalia masuala ya msingi jamaa anangalia dini!!!. Langu mimi ni je nini rekodi ya hawa makatibu wakuu wapya katika utendaji na ufanisi?. Watanzania tunatakiwa kutofautisha kuwa competent and kuwa qualified!, Tunataka watu competent siyo wenye vyeti tuu uwezo wa kazi 0. Hili ndilo jambo la msingi zaidi, pamoja na madegree, Tanzania tunapata mgao wa umeme kila mara! leo Ngeleja kaulizwa unaisha lini, sijui? kweli tunaposema wameshindwa kazi tunakosea?. Jamani tuangalie rekodi ya utendaji kabla ya kuwapa watu vyeo.
ReplyDeleteNi huzuni kubwa kuona mtu wa kwanza kutoa comment kwenye hili swala ambayo inahusu udini kweli ni aibu tupu mtu mzima na akili zako kutoa comment ya kijinga hivyo.
ReplyDeleteNinaamini wewe ndio mdini number moja na fitina zako hazitafanikiwa.
Jaribu kuangalia uwezo wa mtu na sio dini yake
Shame on you!!!!!
Hongereni mlioteuliwa na mkumbuke umma wa Watanzania unaowategemea katika kuwajibika itakiwavyo pasi uvunjaji wa sheria, taratibu wala maadili ya kazi / ofisi zenu.
ReplyDeleteNi upuuzi kuanza kuchambuka uteuzi wa rais kwa kuangalia kuwa wametoka dini au madhehebu gani.
Wanaotetea upuuzi huu hapa nina wasiwasi na ama uelewa wao au afya yao hasa inayohusiana na mifumo ya fahamu na ubongo na hata makusudio yao! Hawa nao ni hatari kwa usalama wa Taifa kama Econometrician alivyomuhasa Mashaka.
Maswali ya kuwauliza hawa wanaoshabikia Udini ni haya hapa:
1. Umetambuaje kuwa wote hao ni Wakristo? Je wajua kuwa mimi nina jina la Kiislam wakati ni Mkristo na zaidi ya hapo nina rafiki kibao ambao wanajiita Wakristo lakini hakika si Wakristo ni a true sense?
2. Kwa vile umeamua rais aonyeshe balance kwa kufuata dini, sasa nani kakwambia kuwa TZ ina dini mbili tu??????? Je Wanaoabudu katika dini za asili yetu na wale ambao madhehebu yao hayako katika Uislamu wala Ukristo unawapeleka wapi au wao si Watz? na je Wapagani ambao hawaamini uwepo Mungu wao hawafai kabisa kuongoza au unasemaje na naomba unipe jibu kwa kurejea sheria mama (Katiba ya nchi yetu).
3. Kwa vile umeamua kuwa dini iwe kigezo cha uchaguzi ili kuonyesha kuwa haki inatendeka sasa naomba hapa niungane nawe katika ukichaa huu ili tuende pamoja. Ebu sasa wachambue zaidi hao Viongozi Wateule maana inaonekana unawafahamu sana katika madhehebu yao maana kusema tu kuwa ni Wakristo haitoshi. Tunataka usawa kwa kila Dhehebu, Dayosisi, Jimbo na hata Mtaa ikiwezekana! Kwa maneno raisi nauliza,
Je rais amebalance Ukatoliki na Uprotestanti maana sisi si wamoja. Je rais amebalance nani Conservative na nani Liberal Christians hapo? Je wote ni wenye asili ya Charismatic Churches au la? Je walibatizwa kwa kutumbukizwa majini au kwa kunyunyiziwa. Na kama nafasi za Makatibu Wakuu zilikuwepo nne sasa madhehebu yenyewe ya Kikristo ( sijakueleza ya Kiislam) ni zaidi ya 38,000 sijui sasa ni zamu ya dhehebu gani kupewa na wengine 37,996 watasubiri mpaka lini??????
4. Je umetumia baseline data za kutoka utafiti wa nani na mwaka gani kutueleza kuwa hakuna usawa. Na una maanisha nini unapotamka neno 'usawa' kuna usawa wima na usawa mlalo (vertical & holizotal equity). Yaani utafiti wako utuonyeshe kuwa Wakristo (na sijui utawajuaje maana hata sensa iliyopita hakuna????) wana nafasi bora zaidi kuliko wengine(Kumbuka pia ukuu wa nafasi sio lazima kuwa ni nafasi bora)na kwa kulinganisha na sifa zitakiwazo walizonazo katika kazi husika kwa kila eneo kila mwaka kwa Tz nzima.
Mshikaji mbona utapewa PhD with honours saa hiyo!
Michuzi huu ni upuuzi sana watu wanatakiwa kutathimini utendaji wa viongozi wetu kwa kufuatana na matokeo ya utendaji wao unapolinganishwa na malengo ya kazi husika; Vinginevyo wakimaliza kutumia UDINIOMETER wataibuka na UKABILAOMETER, UKOOMETER, UJIMBOMETER n.k mpaka hapo Taifa litakaposambaratika!
NA MIMI NASEMA HATUKUBALI KUNDESHWA KWA VIPIMO HAFIFU NANMA HIYO!
ili nchiwe naamani ni bora marais wote wataokuja wawe waislamu, akija rais mkristo atakuwa na wakati mgumu sana
ReplyDeleteiasikitisha sana watu kuficha ukweli
WEE ANONY WA PILI ACHA UNAFIKI KUJIFANYA NI MUISLAMU KUMBE KAFIRI TUU,Hivi akina nani waliokamatwa na vyeti vya KUFOJI KAMA SIO HAO UNAOSEMA WAMESOMA missionary? tena maPHD ya uongo kumbe standard seven tuu na diploma ndo wanazo.
ReplyDeletewapo MUSLIMS kibao wana shule zao saafi na usilete upimbi wa kusema eti maduka na misikiti tu. Juzi tuu tumeona tena ripoti ya vilaza walioforge vyeti, hahahahahaha MAKAFIRI KIBAOOOOO. kweli kwa kuforge mna elimu nilikuwa sijui mimi.
Nami naomba kuchangia kidogo. Huyo mchangiaji wa kwanza naomba atoe vigezo vya huo usawa/uwiano anoutaka katika uteuzi wa rais,naomba ajibu maswali haya kwanza. Kwanza Je, huo usawa/uwiano anaoutaka utazingatia idadi ya wakristo na waislamu wote TZ? hapa nina maana ile kuwe na usawa/uwiano uteuzi itabidi uendane idadi ya watu wa dini fulani. Pili je, usawa/uwiano huo utazingatia idadi ya wakristo wote wenye sifa stahili na waislamu wote wenye sifa stahili? hapa nina maana wenye sifa stahili waorodheshwe pande mbili(wakristo vs waislamu) ili usawa/uwiano uzingatie wingi wao,walio wengi wapate nafasi nyingi na wachache wapate nafasi chache. Je,kuhusu madhehebu kama alivyosema mchangiaji mmojawapo itakuwaje ili kupata usawa/uwiano anaoutaka anony wa kwanza? NASIKITIKA SANA KUONA ANONY HUYU ALIVYO NA FIKRA NA MAWAZO MGANDO, ASHINDWE NA ALEGEE,ANAPASWA KUSOMEWA ALBADR KWA VILE FIKRA HIZI NI ZA KICHOCHEZI AMBAZO ZITAPELEKEA KULETA MATESO KWA WATOTO NA WANAWAKE ENDAPO KUTAKUWA NA MACHAFUKO YA KIDINI.
ReplyDelete