BIA CHAPA YA KILIMANJARO YAZINDUA KAMPENI YA “FIKISHA TANZANIA KATIKA HATUA YA JUU ZAIDI”

Kilaji cha Kilimanjaro leo kimezindua kampeni ya “Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu Zaidi”. Katika kampeni hiyo, bendera ya taifa itakimbizwa kuanzia jijini Dar es salaam mpaka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. “Hii ni namna ya pekee ya kufurahia na kujikumbusha mafanikio yetu ya kiwango cha juu” anaeleza George Kavishe, Meneja wa Bia Chapa ya Kilimanjaro.

Kampeni hii ya “Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu Zaidi” itaanza rasmi tarehe 1st Novemba, 2009 hapa jijini Dar es Salaam na inatarajiwa kufikia tamati katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo tarehe 6th Novemba, 2009. Safari ya kukimbiza bendera hiyo ya Taifa itapitia katika miji kadhaa kabla ya kufikishwa katika kilele cha Mlima Kilimajaro. “Hii ni changamoto ya kihistoria, tunaelekea na taifa letu kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro” anasisitiza David Minja, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, TBL.

Bia Chapa ya Kilimanjaro, ni maarufu kwa kudhamini matukio ya michezo na burudani yaliyopata mafanikio makubwa kama Mbio za Marathoni za Kilimanjaro za urefu wa km 42.2 na nusu Marathoni km 21.1. Mashindano haya yanayotambuliwa kimataifa, yanashirikisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 25 duniani. Mashindano hayo hutayarishwa kufuatana na kipindi cha ukame mbugani ambao hupelekea wanyama aina ya Nyumbu zaidi ya millioni moja kuhama katika makazi yao ya asili katika mbuga za Serengeti (Hili ni tukio la kipekee, kubwa na la asili duniani). Bia Chapa ya Kilimanjaro inadhamini mashindano haya ya Marathoni tangu yalipoanzishwa mnamo mwaka 2003. Mapato yatokanayo na Mashindano ya Mbio za Marathoni za Kilimanjaro hutolewa kusaidia jamii na kusaidia huduma mbali mbali mkoani Kilimanjaro.

Bia Chapa ya Kilimanjaro pia ni mdhamini wa tuzo maarufu za muziki za kila mwaka Afrika Mashariki zijulikanazo kama “Kilimanjaro Music Awards”. Tuzo hizi hutolewa kutambua jitihada katika sanaa hii na kukuza vipaji vya muziki. Tuzo hizi hutolewa katika makundi mbali mbali yanayoshiriki sanaa ya muziki.

Bia Chapa ya Kilimanjaro ni mdhamini mkuu wa timu mbili zenye historia ndefu katika mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania, Simba na Yanga. Bia Chapa ya Kilimanjaro inatumia jumla ya Shillingi billioni tatu za Kitanzania katika kipindi cha miaka mitatu, katika jitihada zake za kuongeza ushindani katika ligi kuu nchini. Hii ni sehemu ya mpango wa Kampuni ya Bia Tanzania, TBL wa kuenedeleza mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingine kwa ujumla nchini Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mungu atusaidie tuu. Nchi itafikishwa katika hatua ya juu zaidi kwa kuendelea kulewa.

    ReplyDelete
  2. Nyie watu, hacheni Ujinga.

    ReplyDelete
  3. WAPENDA HAKI TUSUSE BIDHAA ZA TBL KWA KITENDO CHA KIIHUJUMU SERENGETI.

    ReplyDelete
  4. mimi nazani safari ingeanzia zanzibar

    ReplyDelete
  5. Heheheeeee na mimi nilitaka kusema vivyo hivyo, hao watakao kwenda kileleni watafika kweli kwa kulewa. lol

    Wanaopanda milima, wakimbiaji, wacheza mpira na BEER wapi na wapi.

    Hizi kampeni zingine ni aibu tupu, hebu niambieni bia inatusaidia vipi katika kujenga miili yetu na kuwa juu zaidi.

    ReplyDelete
  6. Michuzi, wape TBL contact zangu kampuni yangu ina deal na marketing strategy! how to lunc a new product in the markert etc etc, naweza kuwapa proposal yangu.
    tukabadilisha hiyo kidogo.
    PQ. kama wako tayai nijulishe

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi hata wewe unashabikia ulevi.Hujui kwamba anaetengeneza,anayeuza,anaesambaza,anaetangazia wote muko kundi moja.
    Kazi kwako.Nimesahau pamoja na anayekunywa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...