FAMILIA YA ASHURA KASHEBA WA LONDON, TUNAPENDA KUMKUMBUKA MPENDWA WETU BABA YETU KIPENZI NDALA KASHEBA TOKA AIAGE DUNIA 22 OCT 2004 LEO HII AMETIMIZA MIAKA 5 KAMILI.
UCHESHI, UPENDO NA UKARIMU WAKO KATU HAUTASAULIKA ,MAWAZO NA USHAURI WAKO UTABAKI MIOYONI MWETU. UKO KWENYE MAOMBI YETU KILA SIKU NA TUNAKUMBUKA YOTE ULIYOYAFANYA KATIKA MAISH
UMEBAKI KUWA KUMBUKUMBU KUBWA SANA KWETU JAPOKUWA SIKU ULIPOTUTOKA ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUBWA SANA KWETU.
TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPA UJASIRI MKUBWA WA KUELEWA KUWA KIPENZI CHETU UMETUTOKA.
SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI,UKAE KATIKA AMANI MPAKA HAPO MWENYEZI MUNGU ATAKAPOTUKUTANISHA TENA INSHALLAH.
FAMILIA YOTE,WATOTO WAKO WOTE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI TUNAKUOMBEA MAPUMZIKO MEMA. MWENYEZI MUNGU AIWEKE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YAKE PAMOJA NA NDUGU WOTE WALIOKWISHA TUTANGULIA MBELE ZA HAKI.
AMIN.
WAKO MPENDWA MKEO
ASHURA KASHEBA
LONDON
KWA KUMBUKUMBU ZILIZPITA ZA KASHEBA
BOFYA HAPA
BOFYA HAPA
Mama Ashura Kasheba pamoja na familia yako nipo pamoja nanyi katika kumkumbuka gwiji huyo wa muziki hapa nchini, mafundisho mengi ametuachia kupitia katika kazi zake nyingi na nzuri za muziki alizozinakshi barabara kutumia 'kombora' lake la nyuzi dozen!! RIP Supreme Freddy Ndala Kasheba - Ben
ReplyDeleteRIP shemeji yangu!
ReplyDeleteMuddy
Ah muyoomba RIP
ReplyDeleteRIP Maestro, tunakukumbuka. Kweli ulikuwa umebarikiwa na kipaji cha hali ya juu
ReplyDeleteNAKUMBUKA SIKU YANGU YA MWISHO KUMUONA GWIJI LA MUZIKI NI PALE LION CLUB SINZA.SIKUJUA KAMA GWIJI AMEFARIKA HADI LEO NASOMA HII HABARI pumziko la milele gwiji,POLE SANA ASHULA,NA TUKO WOTE.SEMA NAPENDA PIA KUTUMIA NAFASI HII KUKUULIZA MDOGO WAKO WASTARA YUPO WAPI..?Pls mpe mail yangu...pachino8569@yahoo.com
ReplyDeletemdau uk.
Uendelee kupumzika kwa amani. Utuombee nasi tuliobaki huku duniani. RIP Ndala!
ReplyDelete