sehemu ya makaburi wanapozikwa watu mashuhuri jijini kinshasa. kaburi la lwambo lileeeeee... lenye paaa mbele kushoto. anko alikosa pesa kulisogelea kama askari wanaolinda hapo walivyotaka. leo ni miaka 20 kamili toka gwiji hilo la muziki litutoke
anko akitoa heshima kwenye kaburi la pepe kalle ambaye kama lwambo waliitangaza kongo ya kabila kwa nguvu zote na mafanikio. picha zaidi za kinshasa
BOFYA HAPA
na
BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Unajuwa Anko nanihii nimestuka kidogo sababu nimetoka sasa hivi kusikiliza zilipendwa, nilimsikiliza na Pepe kalle kibao chake cha "hidaya" kuingia humu nakuona kwenye picha upo kwenye kaburi la pepe Kale mwenyezimungu amrehemu. Juma.

    ReplyDelete
  2. Kuna nyimbo moja ya zamani sana, zilipendwa inasema namtafuta sasa sijui monica au nani kakimbia iringa Sijui ndala kasheba au nani, enzi za RTD Mikidadi Mahamoud ndio alikuwa Dj Radioni kama yoyote anaijuwa na anajuwa nani kaimba anipe tittle.

    ReplyDelete
  3. mi miaka ishirini na bado ngome dhabiti ya muziki wake imedumu hata sasa.

    ReplyDelete
  4. tuwekee makaburi ya mbaraka mwinshee na marijan rajab tuone yalivyo..

    ReplyDelete
  5. Wimbo ni wa pepe kale, 'Hidaya Wangu'

    ReplyDelete
  6. Wimbo ni wa pepe kale, Hidaya Wangu

    ReplyDelete
  7. hidaya wangu song by pepe kalle

    ReplyDelete
  8. We anonymous wa oct 12 saa 05:58 naguess upo kwenye kundi la vijana wa kileo za yoyoo..yoyoooo ngoja nikukumbushe wimbo ni Monica wa marehemu Ndala Kasheba huyu binti alitoroka na doti 10 za khanga na kudandia treni ya kwenda zambia....mmmmmh kibao murua sana

    ReplyDelete
  9. wee anon hapo juu nimehifadhi maoni yangu KUKUHUSU..ila nyiye ndo hufungua midomo kwanza, mkafikiri baadaye..Haya ameweka ni ya hukoooooo KINSHASA..sasa na hapo Mzenga na Kisutu pia nako 'akuendee'..wewe upo katika kusema 'tuwekee, tuwekee, tuwekeee..' - bhagosha!!

    ReplyDelete
  10. Kweli Ahsante ni Ndala Kasheba Inaitwa Kesi ya kanga nimeshaipata Kule eastafricantube.com

    http://www.eastafricantube.com/media/11658/RTD-MIKIDADI_MAHAMOUD/

    ReplyDelete
  11. Wimbo Kesi ya khanga by Ndala kasheba "NIkamtafute Monica........."

    ReplyDelete
  12. Hivi?anko mbona unaanzaa tabia mbaya?unakuwa kama yule dada sophia kessy na blog yake wamejaa wakongo tuuu,kwa nini?utuwekei picha ya makaburi ya kina hayati Salumu Abdala,Juma Kilaza,
    hivi wangapi wanamjua marehem mzee makongoro aliyekuwa na kwaya ya vijana wa Tanu?

    ReplyDelete
  13. Anko na wewe kwa kutaka kujichukulia mauspuni haujambo. Naona macho yako yalikuwa kwa mpiga picha wala siyo kwenye kaburi la Pepe. Au ndiyo ile ya kukaa kimya na kuhesabu mpaka kumi kisha imetoka. Anyway, hata hivyo anko misupu dunia ni yako mkuu.

    ReplyDelete
  14. Anko Misupu kwa mauspuni haujambo! Ninaona hapo macho yako yote yakiwa kwa mpiga picha na kiwiliwili kwenye kaburi. Au ndiyo zile za kusimama karibu na kaburi na kuhesabu mpaka kumi kisha imetoka. Hat hivyo mkuu, dunia ni yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...