rafael benitez, kocha wa liva,
akisononeka baada ya kufulia kwa mara ya nne msimu huu.
wadau wenzangu wa bwawa la maini, hivi tuna nuksi gani sie msimu huu yarabi toba??? yaani hatuna raha. mechi ya kawaida tu kamasi zinatutoka. tufanyeje wadau?????? ama na sie tuanze kuongea vizuri na marefa kama nanihii ili mambo yawe mswano???? huyu kocha anatufaa kweli jamani???
mjadala huu ni mahususi kwa wadau wa bwawa la maini tu. watani wa jadi tunaomba msituingilie. watu tuna hasira kweli, ohooooo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Kocha hana matatizo, kocha ni mzuri tu na kama mnabisha tukimfukuza hachukui hata muda atachukuliwa na timu nyengine kubwa hivyo hivyo, tatizo liko kwa baadhi ya wachezaji, wengine sio wazuri ukilinganisha na wachezaji wa timu zengine au hawajitumi kama inavyotakiwa kujituma kwa ari kama wanavyojituma wachezaji wa timu zengine, lazima tununue wachezaji, timu iuzwe, naamini kabisa kama bado ligi inaendelea na tutajinasua tu, sikati tamaa.

    ReplyDelete
  2. Tutapiga kelele huku Tz tutachoka lakini hakuna tunachoweza kubadili, hasa ukizingatia hatulipi hata viingilio kuona mechi. Tatizo sio Rafa, tatizo ni Wamarekani waliochukua timu. Baada ya kumuuza Alonso walitakiwa kumchukua Gareth Barry lakini Wamarekani wakaleta ubahili Rafa ikabidi aende kutafuta chaguo lake la tatu, majeruhi wa kutoka Italia.
    Kimsingi Liverpool ya mwaka jana ilikuwa inategemea wachezaji wanne: Gerrard, Alonso, Torres, na Kuyt. Mradi Gerrard akiwepo hao wengine wakikosekana haikuwa mbaya sana. Shida ni kuwa Alonso hayupo. Akikosekana Gerrard walau akawepo Alonso palikuwa hapaharibiki neno. Mambo yamebadilika. Mascherano ni hodari kukaba lakini hana uwezo wa kutoa pasi ndefu za hatari. Lucas Leiva ni hodari wa kukaba lakini hawezi kupandisha mashambulizi.
    Tunachotakiwa kufanya ni kuchangishana, tununue timu kutoka kwa Wamarekani na kufanya usajili wa kufa mtu.

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi pole na kazi,mimi ni msafiri wa mara kwa mara na ninatumia JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT mara zote lakini nimechoshwa na hivi vitendo vya kuibiwa vitu vidogo vidogo kila siku espicially saa(watches)sasa nilikuwa naomba kama kuna watu wengine na wao ambao wameshawahi kupoteza vitu vyao embu tujaribu kuwaandikia hawa jamaa wa SWISSPORT,maanake wao ndio wanaoshughulikia maswala ya mizigo pale Airport ,kwa mtu yeyote ambaye angependa kuandika na kulalamika tumia hii add Head Office
    Terminal II
    JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT
    P.O. Box 18043
    Dar es Salaam, Tanzania
    Tel: +255.22.2844610
    Fax: +255.22.2844343
    E-mail: info@swissport.co.tz
    Website: http://www.swissport.co.tz
    ikishindikana then tutatuma malalamiko yetu kwenye headquartes office yaoSwissport
    Flughofstrasse 55, 2nd Fl.
    8152 Glattbrugg, Zürich, Switzerland (Map)
    Phone: +41-43-812-20-20
    Fax: +41-43-321-29-01 .
    Naona hawa jamaa wanahitaji wake up call kwa kweli this is to much,tusaidiane jamani hii tabia ikomeshwe,mdau Marekani

    ReplyDelete
  4. hiyo ndio primia ligi kaka michuzi na hakuna mechi ya kawaida hata moja ndani zile 38 zote ni muhimu ili uweze kunyakuwa mwali mwishoni,hapo bado sababu vipigo vingine vinakuja..
    ila kocha wenu hana jipya tena ndani ya wachezaji 69 aliyoleta Anfield mpaka sasa hajanyanyua makwapa hata mara moja...
    mabadiliko MAKUBWA YANATAKIWA ikiwemo kutolewa kwa kocha na wachezaji wengine ambao hawatakiwi kukaa pale..

    mdau, shetani mwekundu!!!!

    ReplyDelete
  5. Tatizo la liverpool sio Coaching problem alone,hamna wachezaji walio health day in and day out.

    Poleni sana,mimi kama mshabiki wa ManUnited,ninashuhuda kikombe kwa mara ya 4 mfululizo kinanukia,Kwani Chalsae anaonekan hawezi kushinda mechi za ugenini.

    ReplyDelete
  6. kweli mkuu!
    mie nina imani na coach.
    tatizo tulilo nalo liverpool ni mafao.Liverpool haina pesa! period.
    hawa wamarekani ni hawana pesa,wanategemea mikopo kutoka benki, sasa na uchumi wa dunia umeyumba basi hawana tena nafasi ya kukopa.
    wakuu hatuwezi kuchukua Premier or any other trophy kwa kutegemea Torres na Gerrard. Liverpool haina depth au bench power.Angalia timu kama Man U, Chelsea au Man City,hao wanaokalia tu bench ni hatari mno!
    Ili kuweza kupambana na hizi power teams uwanjani na katika transfer markets.Inabidi tuwe na fwedha za kutosha na kubaki!
    so lets kick these americans out and get other owners with excess funds! zaidi ya hilo ni kuwa hawa wamarekani hawajui lolote kuhusu soccer.............
    nabaki hata nashangaa hapa Gillet alikwenda kuangalia soccer acadamies huko arabuni! does he know anything about soccer in the first place? hajui!

    ReplyDelete
  7. Fair enough!
    But why didn't the Liverpool keeper/defenders deal with this???
    Same happened to Man City v Sheff United and Joe Hart refused to clear the balloons....We lost. :(

    ReplyDelete
  8. Tatizo letu Anko Nanihii sio kocha, bwawa halina waogeleaji wazuri ukilinganisha na darajani au watani wa jadi mashetani wekundu, huwezi kumtoa Kuyt ukamuuigiza Ngong, wakati unaweza kumtoa Giggs akaingia Nani,au kumto Lampard ukamuingiza Ballack. Kocha ni mzuri sana, ndio maana alisifiwa mwaka jana (na ESPN Soccernet Press Pass) kuwa timu hii angepewa kocha yoyote mwengine kutoka big 4 wasingeweza kufika alipofikia yeye, na isitoshe mwaka huu tunataka kushambulia sana wakati wote sasa counter attack ndio zime tukosti kwa Aston villa, Chelsea, na Sunderland, Bora waarabu wachukue timu tutapata waogeleaji wazuri, hawa wamarekani miyeyusho.

    Mdau Mkuu Bwawa la Maini, Wazo Hill, Tegeta

    ReplyDelete
  9. Mwaka huu mtakiona kilichomnyoa kanga manyoya shingoni, hahahahahah!! Gooonerz mwendo mdundo.

    Na mwaka huu hata nafasi ya nne haipo!

    ReplyDelete
  10. Mzee wa Zeze, Columbus, Ohio- U S AOctober 19, 2009

    Kaka Michu, hiki kifaa bado kinatufaa ila inafaa kishauriwe namna ya kupanga timu inayoanza na muda wa kufanya mabadiliko. Sasa hivi hata vijitimu vilivyopanda mwaka huu vinaipania Livermaini hivyo dawa yao ni kuanza na kikosi kamili cha akina Masherano( Argentinian Team Captain) tokea alfajiri badala ya kuwaingiza dakika kumi za mwisho.
    Watoto wetu akina Spearing waingizwe baada ya kumpiga mtu 3 au 4 kama tulivyowafanyia Real Madrid, Man U, ile timu ya Ufaransa nimeisahau jina na wengine msimu uliopita.

    ReplyDelete
  11. bwanamichuzi mie naona wewe unaanza kutembea peke yako!! maana hakuna mpenzi wa club yetu tukuka ya Liverpool ambaye ameshuku ewezo wakiteknikali wa nguli w soka "BANITEZ" Isipokuwa wewe,

    hilo liaonyesha kabisa kuwa wewe sio damu damu, na kwa hali hiyo ni bora uamie darajani ambako wanabadili maofisa wa juu "meneja" kila kukicha.

    Banitez ataendelea kuwa mkuu wa itifaki katika club hii kongwe na mafanikio yataendelea kupatikana.

    Mdau,
    Dennis Clyton.
    Leicester,UK.
    Liver bird- never walk alone.

    ReplyDelete
  12. Wapuuzi wanasema wenger bahiri wengine utawasikia yule ni muiconomist,... hebu waangalie hawa makocha ambao sio mabahili, Rednap wa tott kila siku anasajili kwa mamilion na anawalipa wachezaji mamilioni kibao OUTPUT sifuri, Morinho kawaachia Chelsea loss zaidi ya Pound 200ml mpaka pamoja na kuchukua ubingwa mara kibao wataalamu wa soka wakamwita "TITLE BUYER" ferg usiseme sasa hivi timu inadaiwa acha na ikifuka mwakani mwezi wa sita haijapunguza deni inafilisiwa pound zaidi ya 390ml si mchezo yeye kazi yake ni kuwahonga marefa na kununua wachezaji wa bei chafu na kuwalipa mishahara minono ingekuwa Italia man wangeshushwa daraja kama Juve,Fiorentina,...
    Man city du! chaliiii, Sasa liver Gerard, Torres na Mascherano lazima wauzwe haiwezekani ukope halafu fedha uende ukajengee heshima baa halafu hutaki kulipa... Benitez ili apate mafanikio anatakiwa amuige Ferg kale kamchezo kachafu ka kuhonga marefa manake haiingii akilini kila mwaka anasajiri kwa mamilioni ya pound halafu matokeo hayatofautiani na Arsenal ambayo kila mwaka wanauza wachezaji kibao na deni lao linapungua... halafu mwaka huu asilimia tisini ya watoto wa wenger wamekua fanta ukiwapa wanamaliza, upande wa mademu usithubutu kuwaachia umpendae....

    "IN WENGER WE TRUST"

    ReplyDelete
  13. ha ha haa uuwwwi mwenzako akinyolewa na wewe tia maji anyway siku hazigandi mtaibuka tuuu
    manuuuuuuuuuu!!!!

    ReplyDelete
  14. TIMU YETU NI NZURI ILA TATIZO KUBWA MSIMU HUU NI MAREFA NAONA WAMEAMUA KUTUKOMOA TU.LILE GOLI LA JUZI HALIKUSTAHILI KUWA GOLI,MPIRA ULITAKIWA KUDUNDWA NA REFA KWA SABABU KULIKUWA NA OUTSIDE INFLUENCE.PILI KOCHA WETU NI BOMBA TU TATIZO NI WALE WAMARECANI HAWAMPI USHIRIKIANO WOWOTE,WAO WAMEIFANYA LIVERPOOL NI KITEGA UCHUMI WANATAKA FAIDA TU.LAKINI NDUGU YANGU TULIA WIKI IJAYO LAZIMA MTU ATALIA TU!!!!!!!YNWA.

    ReplyDelete
  15. Hii mbona rahisi, njooni kwangu niwasafishie nyote zenu, nineangalia nimeona zimechafuka sana!!

    ReplyDelete
  16. HATA UKIHONGA REFA KAMA MPRIA HAUNGII KIMIANI REFA TAFANYA NINI? NA KAMA HUZUII MIPIRA KUINGIA NDANI MWAKO REFA ATAKUSAIDIA NINI? TATIZO NI KUJENGA TIMU IKITEGEMEA WACHEZAJI WAWILI, AKIUMIA MMOJA AU WOTE MMEFULIA, MAN U UNAWEZA PELEKA TIMU 2 KWENYE LIGI KUU NA ZIKACHEZA SAWA SAWA, CHELSEA NAYO VILE VILE, MWAKA HUU HATA NNE BORA HAMUTAKUWEPO.

    MDAU WA MAN U

    ReplyDelete
  17. Anony wa Mon Oct 19, 08:15:00 AM kibwengo kweli, hebu kakojoe ukalale kule,alaaa!!

    ReplyDelete
  18. tatizo watu wanashindwa kumuelewa mzee alex, yeye ana mbinu na nje ya uwanja pia, kwa maana ya wachezaji wa akiba, na hao ndio wanaokupa ubingwa ikifikia una majeruhi.wenger na benitez wanashindwa kubadilika kwenye hilo, wakiumia wachezaji wawil au watatu basi team inaboronga, mnaanza hoo sir anahonga marefa, hakuna kitu kama hicho, yule mzee ni mzoefu anajua fitina za ligi ile,nyie endeleeni kubadili makocha lakini suluhisho ni mpaka sir ang'atuke pale trafford othersise mtasubiri milele na mtakufa bila kelele,

    mdau,

    ReplyDelete
  19. Tanzan1anDreamOctober 19, 2009

    Unajua msimu huu mi nilitaka niongee mapema lkn nikakatwa kauli na mechi ya kwanza...Ila kama we unadhani bwawa la maini msimu huu litakuwa doro jaribu kuangalia game ya chelsea na Villa utaona tu kuwa msimu huu hadi ifike feb ndio unaweza sema una matumaini ya ubingwa otherwise mi napiga kimya najua wajinga wajinga wengi tu...Kama tulivyopatwa sisi kuna mwezi utakuwa mbaya kwa timu nyingine na hiyo ndio Premier itakavyoenda msimu huu....Likija suala la kiufundi Rafa inabidi amrisk tu Aquilani,maana tupo desperate now tunahitaji mtu anaeweza ipandisha timu mbele,Spearing mzuri lkn bado hana xperience na ni wazi hatupo kwenye majaribio kwa sasa...So i'd say give Babel more startin' time,Keep Kuyt on the bench"we need to attack sio kupooza mpira kila mara"halafu Weka Benayoun Acheze na nyuma ya Torres,GErro arudi kati wakati Aquilani anaanzia benchi hadi dk ya 55...Hii ni immediate response"vs Lyon"...Halafu wakija mabwege wa Trafford tutatumia hata ndumba kushinda.....

    ReplyDelete
  20. naona timu haina morali. utashangaa kuona beki kama carager anavyologota siku hizi. lakini vile vile kiungo hakichezi ipasavyo.

    kocha anachangia kwa namna moja au nyingine. aliamua kununua majeruhi ambaye hamsaidii halafu kanunua beki wa ajabu huyo Karigyakos.

    kwa ujumla timu sio nzuri.

    ReplyDelete
  21. Mimi naona tatizo sio kocha. Kwa upande wangu wamiliki wanachangia sana. Malumbano yao na kocha yanaathiri wachezaji. Halafu ni mapema mno kuanza kuibeza timu. Ebu tuone Aquilan atakapoanza kucheza timu itakuwa vipi. Hivi sasa hakuna aliyeziba pengo la Alonso. Nina matumaini kama Aquilan atatimiza matarajio, Liverpool ni nzuri sana

    ReplyDelete
  22. anko hapo tatizo ni kocha huwezi ukamuuza bellamy sisoko risse alonso owen na wengine wengi wazuri kwa chuki zake binafsi halafu tukae tukitegemea miujiza kutoka kwa akina ngong lucas na riera hapo aondoke tu atuachie timu yetu tuna hasira nae sana tu

    ReplyDelete
  23. michuzi sijatambua kama unataka kubaki na watu wako wa bwawa la maini ndani ya hii blog yako !!mbona unanibania kila comment yangu?? inaniudhi kweli?naona tu kama unanifukuza kwako duh!!!

    ReplyDelete
  24. weee uliyesema ati man uu inadaiwa ati ikifika mwezi wa sita bla blaaa na nyinyi hongeni marefa kwani mmekatwa mikono? maneno ya mkosaji na jilaz kwa sana tu mnatuonea kijichoo mtajijuuu wa kenda havai moja ni kawaida yetuuuu hata mseme tunabebwa ebo nani hapendi?? kubebwa raha ati kiru!! na hizo hela zitalipwa tuu babu hajaanza kazi jana poleni eee kalaghabao
    man uuuuuuuuuu i luv youuuuu over michuzi

    ReplyDelete
  25. Mi nadhani tactically Bernitez hana matatizo..tatizo ni over reliance on Torres Gerrard na Carrager...hamna plan B when say those players are injured or are out of form...Bernitez amesajili wachezaji wengi..wabaya na wazuri but hawapi chance ya ku intergrate kwenye timu...watu kama kina Crouch na Bellamy walikuwa ni wazuri but no enough playing time..Man Utd for Example ina wachezaji kibao lakini kila mmoja yuko happy..kila mtu anapata chance..wote wanakuwa motivated..as a result they have a very strong squad and not strong first eleven...vilevile scouting system ya Liverpool sio nzuri...ukiangalia Arsenal and to some extent Man Utd (chama langu) they dont have to buy big..they just buy smart..change potentials into stars..liverpool hawana hicho kitu ..matokeo yake ni kununua wachezaji na kuuza kwa Hasara ..Keane for example
    I Would Rather Walk Alone
    Mdau Manutd

    ReplyDelete
  26. Makocha huwa wana kauchizi mulani hivi!!. Mjomba hapo tatizo ni mido 2, huyo wa kuitwa LUCAS hatufai,huyu ndo wakuingia pindi ya pili dakika ya 70,80. 2ombe munguhuyo muitaliano apone haraka maana hali ni mbaya!!!!!!!!!!


    Mdau,
    Ndanya

    ReplyDelete
  27. Mon Oct 19, 08:15:00 AM matatizo yako ni makubwa.
    linganisha fedha alizotumia fergie na benitez hlf linganisha na output. Alonso is overated mbona sisi hatumtajitaji CR7,TEVEZ na juzi rooney,vidic,fletcher,oshea hawakuwepo na moto mmmeuona(5 key players hawapo) na kila mechi inaingia timu mpya
    chelsea wana timu moja tu sawa na bwawa la nyongo

    MONEY CAN'T BUY EVERYTHING(U CAN'T BUY SUCCESS)till fergie is out of utd

    ReplyDelete
  28. Tatizo ni kocha jamani. Ili kuwa kocha mzuri inabidi uwe na uwezo wa kuwafanya wachezaji wako wajitume kwa uwezo wao wote na katika kila mechi. Mfano Man U, Chelsea na arsenal they get the best out of their players. Benitez kakazania laptop tu kuangalia statistics tu, hawezi kumotivate wachezaji hata wakifunga goli huwa hashangilii yaani ukocha kwake ni kazi tu na sio burudani kama makocha wengine.
    Kupanga timu nako kunamsumbua sana, mascherano na lucas hawawezi kucheza pamoja lakini anawang'ng'ania, caragher na skytel wametufungisha mechi zote lakini bado anao tu, kuna yule mtoto ayala kacheza vizuri mechi zote alizocheza lakini hapewi nafasi. pia substitution huwa anachelewa sana kufanya hata tukiwa tumezidiwa anasubiri hadi dk 75, kaclemisha tactics zake.

    ReplyDelete
  29. Na kwa taarifa yenu wadau wa BWAWA,MANUTD will kill OFF your title dreams comes next weekend,manake wanataka kuhakikisha kwamba wanakumaliza mapemaa ili wabakie na mdudu CHELSEA,hao ze gooners ni baiskeli ya mbao tu ile,hawana safari wale.Poleni na COMEDY goal lile duuh,lakini ile kipa yenu nayo laaazy,muda woote ule aliokua nao wa kulibutua lile dude hakuutumia,thatha mnalalama nini???

    ReplyDelete
  30. mdau 4:18 hata usemeje man uuu iko juu tu na hela ipo we ndo una matatizo ya oblangata man uu haijaanza kununua wachezaji wa bei kali jana dau lako ni sawa na la kuku halimlengi mwewe umefuliaaaaa meza moto

    ReplyDelete
  31. gerard asipokuwepo uwanjani tu mnajamba cheche na nyinyi kakopeni mdaiwe kwani mikopo imewekwa ya nini? mijitu mingine ni pumba tuu man u siyo timu za pale jangwani sijui msimbazi hivyo ni vijicent tuu kama unaweza meza wembe na tutaendeleza libeneke la kukopa na kununua bidhaa originali bakini kusema tutashindwa kulipa mkopo huku tunaleta makombe ndani ati ng'wee ng'wee nyoooo

    ReplyDelete
  32. Fugerson juzi ametoa kauli kupitia MUTV kuhusu liverpoll kimafumbofumbo akisema''I BELIEVE A MOJOR TEAM WILL COLLAPSE IF OWNERS WILL NOT ACT RESPONSIBLY!!''
    alimaanisha sisi livapuli

    ReplyDelete
  33. TATITO NI ULE BEACH BALL TOKA KWA SHABIKI WETU WA BWAWA LA MAINI...TEH TEH TEH TEHHHHHH

    ReplyDelete
  34. Kuna mdau kasema SI REFA ANAYERUHUSU MABAO KUINGIA KIMIANI bali ni wachezaji.ALAFU WE MDAU ULIYELETA HII MADA UMEILETA KINAZI MNO "ETI MUANZA KUONGEA NA MAREFA KAMA NANILIU" kAMA HAWA MAREFA NI WATEJA WA Fergie vipi tena wamemkomalia wakitaka afungiwe kwa moja ya comments alizotoa? biashara itakwendaje hapo, acheni taharifa zenu za vijiweni za kutaka kufurahisha baraza.
    Mdau ManU 4ever.

    ReplyDelete
  35. nshimimana aka dumisaneOctober 19, 2009

    Bwana Michuzi,

    mimi nimepiga makelele sana hapa kuhusu Liverpool ila sijui ni kwanini watu hawaelewi..

    Sasa, kilichobakia ni kuwaachia TRUE fans ili waanze ku-coup Mechi. Ujue fans wakiacha kuingia kiwanjani nadhani Management watafikiria vizuri.

    Tukiangalia upande wa ushambulia utakubaliana na mimi kwamba Mspaniola aka 'mzee wa mapande' Alonso hatunaye tena. Mungu ametoa na Mungu ametwaa!?

    Sasa amebaki Gerrard yuko mwenyewe pale na hakuna mtu wa kutumbiza Mipira ili Gerrard amalizie..

    Mimi ningependa kuandika Barua ya wazi kwa Benitez kumtaka kwamba, kama angeweza kum-train sentaaf (center half kwa ung'eng'e) ili awe anatoa mapande kwa Steven aka Stevie!?

    Ujue, Benitez akikaa chini na sentaaf akamwonyesha KWENYE video za Training au Mechi zilizopita nini Alonso alikuwa anafanya tutaanza kushinda tena.

    kwanini Benitez asiwe mshapu na kumweka mtu dedicate kwa ajili ya kudondosha mipira kwa Stevie lakini!? !? !?.. yaani hata copy and paste. kwanini wasiangalie walikuwa wanashindaje alafu una-copy. kwanini lakini jamani!?

    ..Alwatan!

    = = =
    Buffalo (Karibia na Tube Station hapa Liverpool)
    New York

    ReplyDelete
  36. Mimi sitaki kuchangia ila tu nauliza kwamba juzi hapa mlifungwa na Sunderland je ndio mtaweza kuwafunga Man united??Nadhani itakuwa maajabu mwaka huu.....Maana mimi niliyekuwa namuogopa sana ni Alonso!!

    ReplyDelete
  37. tatizo ni uchumi anfild ndogo inawabana fact!!!
    wakati man u wanaingiza 75000 kwa mechi liva nyongo 48000 fact!
    muuizeni mwana uchumi arsen aliona highbury inwabana ? fact
    glory glory united

    ReplyDelete
  38. We Tarehe Mon Oct 19, 08:15:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    For your info kocha anayesifika kwa ubahili ni Sir Alex no body else so ongea unalolijua.

    Pole kaka Michuzi najua unaipenda timu yako, Mungu atakuonyesheni njia

    ReplyDelete
  39. tatizo rafa anamg'ang'ania sana lucas leiva na ndo chanzo cha magoli yote.kwanini timu haisajili watu kama villa, silva, melo,negrebo,xavi na wengineo na kubaki kusajili watu wasio na uzoefu na majina. bora mwarabu achukue timu nasi tuwe kama man city, real au chalsea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...