hakuna kulala
kazi usiku na mchana
sehemu ya msikiti wa zamani
msikiti wa zamani baada ya kubomolewa kupisha mpya na wa kisasa zaidi

Asalaaam A'alaykum Kaka Michuzi,

Nimekutumia picha za mabaki ya msikiti wa Mkwajuni Kinondoni Dar-es-salaam. Kutokana na habari za wadhamini wa msikiti huo ni kwamba patajengwa msikiti wa kisasa wenye ghorofa si chini ya tatu.

Tungeomba uziposti kwenye mtandao ili wadau waone maendeleo baada ya historia ndefu ya malumbano kwenye msikiti huo. Uwe ni mfano kwenye misikiti mingine.
Tuwaombe viongozi Mwenyezi Mungu
awajaalie wafanikishe, Inshaallah.
Shukran
wabilahi taufiq
Mdau Kinondoni Mkwajuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hilo ni jambo la kheri kwakila mchamungu, inshaallah tunamuomba mwenyezimungu awazidishie nguvu wale wote wanaondeleza zoezi hilo la ujenzi mpaka haop litakapokamilika!

    ReplyDelete
  2. Wadhamini wa Msikiti wa Mkwajuni wanaosimamia ujenzi huu wanastahili pongezi kwa jitihada yao. Pia wafadhili mbali mbali waliojitolea kwa hali na mali wanastahili pongezi kubwa.Wote kwa ujumla Mwenyezi Mungu awajaalie kheri kubwa Amin!

    ReplyDelete
  3. mpaka naondoka bongo kuja ughaibuni,kweli msikiti huo ulikuwa na "BAKORA" Kila kukicha mpaka shule yetu hapo ilifungwa,lakini nashukuru KAMA KWELI viongozi wetu hapo wamebadlika, mdau uliotuletea picha hizi naomba sanaaa usiache kutufahamisha maendeleo ya ujenzi wa nyumba yetu ya ibada

    ReplyDelete
  4. Inshaalh Mungu azidishe kheri!! hapo ndio nilipojifunzia dini toka nikiwa mdogo. Kwa kweri wadau tunajivunia jitiada zenu na mungu awajaalie!! Amin!

    ReplyDelete
  5. Mashallah naona kamati ya wazee chini ya usimamizi wa Mzee Suleiman Seif nawapa pongezi kubwa kwa jitahada hii Allah walipe yalo mema hapa duniani na kesho akhera.Tunashauri msikiti uwe wanawake na watoto friendly Inshallah.
    Kibabu cha Kipemba
    London
    Barking

    ReplyDelete
  6. tunashukuru ndugu zetu waisilamu kama mnafanya mambo yenu ya dini bila kuihusisha serikali ya jamuhuri ya muungano ya tanzania huko ndiko kukomaa kifikra,mnatafuta wafadhili kimya kimya bila kumtuma waziri au kiongozi wa serikali

    ReplyDelete
  7. Hongera Alhaj Suleiman Seif kwa kazi yako makini. nimefurahi kusikia kuwa utakuwa na Library na shule ya nguvu.
    kweli tuna mengi ya kujifunza kwako.

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa uongozi wa msikiti huo na kuna chachafi kutoka kwa waumini waliokua kwenye kikao kabla ya ujenzi kua msikiti huo utakua wa ghorofa tano ambao itakua na library na madarasa ya ziada.

    Ni jambo la kufurahisha hususan kwa walala hoi wanaosoma hapo mkwajuni.

    Mwisho ni pongezi kwa mwenyekiti wa baraza la wazamini hapo mkwajuni. Ndugu umefanya kazi kubwa kuweka msimamo na mshikamano wa waumini ijapo kua ulikua na uwezo wa kuwacha hao walalahoi na kuishi ushuani.

    Umeonyesha kua uislamu hauchagui rangi wala uwezo.

    ReplyDelete
  9. mmhh wenzetu wanatunza majengo ya zamani ili uwe ukumbusho na urithi wetu nyie mnabomoa!!!!! kweli watanzania hatuna asili ya kuenzi na kutunza kumbukumbu zetu.tumejaaliwa nchi yetu ni kubwa je kama tungeamua kujenga msikiti mpya mahala pengine ingetughalimu nini?je kuna ulazima gani wa kuubomoa huo msikiti? mbona zanzibar kuna majengo mengi ya zamani na bado kunapendeza na kunajulikana zaidi kiutalii kuliko hata hapo dar? think about it!!!!

    ReplyDelete
  10. MDAU 12:54 NAONA UNGEJIUNGA NA KAMATI YA UTALII KUITANGAZA NCHI. HAYA MAMBO HAYAINGILIANI. KAMA UNGEJUA SIKU ZA RAMADHANI,.IJUMAA, NA EID PANAKUA HAPATOSHI. WATU HUSWALI MPAKA BARABARANI.

    KAMA UNAKUMBUKUMBU HADI MSIKITI WA MAKA ULIBOMOLEWA NA KUJENGWA UPYA. MSIKITI WA MAKA NA MADINA ZINA HISTORIA KUBWA KWENYE DINI YETU PIA ULIREKEBISHWA KUKIDHI WINGI WA WATU.

    KUHUSU WATALII KWANI SERENGETI KUMEJAA MPAKA WAANZE KUANGALIA MAJENGO YALIOKUA MIJINI?? KAMA NI HIVYO NYUMBA ZILIZOKO KARIAKOO ZINGEHIFADHIWA KUVUTIA WATALII.

    MDAU KUA KIFIKRA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...