Mkurugenzi mtendaji wa BenchMark Productions ambaye pia ndiye mwandaaji wa shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search, Madame Rita Paulsen, akiionesha Globu ya Jamii picha aliyopiga akiwa na Mtoto wa Dandu enzi za uhai za mwanamuziki huyo aliyefariki jijini Dar kwa ajali ya gari wakati nyota yake kimuziki ndio ikianza kupaa. Mtoto wa Dandu, kijana mtanashati toka Mwanza, kabla ya hapo alikuwa akiishi ughaibuni na alipotua Dar alibuni Tanzania Music Awards ambayo leo ndio hii Kilimanjaro Music Awards.
Madame Rita amepozi leo mara baada ya kuwazawadia washindi wa BSS 2009 ofisini kwake Mikocheni jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Dada yetu kumbe naye umekula chumvi kiasi. Mbali na hivyo, nakupongeza kwa kuwa mwanamke wa shoka. You have been not only innovative but also persistent in what you are doing. Keep up the good work.

    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  2. Kumbe Madam Rita kabla ya make ups ndivyo alivyo hivyo...nice..very natural..ila akipaka shedo anakuwa msichana zaidi.

    RIP Mtoto wa Dandu.

    www.sinamakosa.nl

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa duka la music LÄnggatan (Long Street), Gothenburgh, Sweden mwaka 2007. Nikaokota CD upande wa CD zilizotumika ilikuwa ni DJs' material ambayo ilikuwa imeandikwa nyimbo za huyu kijana. Miaka kadhaa kabla ya hapo alikuja Helsinki, Finland na kufanya onesho Jambo Club yeye na mwenzake Mzee James. Miaka kadhaa baadaye nilipokuwa likizo Dar es Salaam tulipita na ndugu yangu pale alipofarikia (karibu na Kijiji cha Makumbusho)wakati hata oil ya gari alipopata ajali haijakauka.

    Mtoto wa Dandu? Kumbe ndiwe uliyebuni Kilimnanjaro Music Award!? Tuzo hii si tuzo bali ni fukuzo linalokutuza sanaa Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Michu, unaweza kupata picha kubwa ya hiyo Rita amebeba tuione vizuri. Walipendeza sana - RIP Mtoto wa Dandu.

    ReplyDelete
  5. mwandishi wa Fri Oct 30, 11:14:00 PM, sijaelewa kiswahili chako cha sentensi ya mwisho. Ni kwamba unaona lilikuwa wazo zuli au unaona tuzo hizo hazisaidii kukuza sanaa tanzania? Ni hayo tu.

    RIP Mtoto wa Dandu. Yeye pamoja na mtoto wa Mengi aliyefariki nadhani ni watu waliokuwa na upeo mkubwa, na nia kubwa zaidi ya kukuza muziki wa kitanzania, bila kuwa na nia ya kufaidika nayo kifedha. Inasikitisha kwamba walitutoka wakati tunawahitaji zaidi.

    ReplyDelete
  6. Anon Sat Oct 31, 05:52:00 PM

    Kuwa na tuzo ni wazo zuri tena zuri sana. Lakini wazo zuri linaweza kubadilika kuwa baya kama litafujwa:

    Mosi, vigezo vya tuzo zinazotolewa vilipitishwa na nani?

    Pili, Kamati ya tuzo inawajibika(answerable to) wapi?

    Tatu, vigezo gani vinatumika ili kumpa msanii tuzo hizo? Kwa mfano, mauzo ya rekodi kwa mwezi au mwaka, kupigwa (played time)sana maredioni au kwenye madisko, sanaa (beauty/aesthetic) iliyomo kwenye muziki kwa kuangalia utunzi (composition) katika mirindimo (Rhythm), ghani (melody), mwafaka wa tungo (harmony)au ujumbe (Lyrics).

    Nne, mtu au wanakamati ya kutoa tuzo wanatakiwa wawe na sifa (Qualifications/prerequisite)gani kuwemo ndani ya kamati ya tuzo?

    Tano, je tuzo zinatolewa kwa mtu au vikundi kwa kazi wanazofanya sasa au zilizopita. Kwa sababu sijawahi kusikia tuzo hizi zikigawiwa kwa watu au makundi yaliyotoa mchango mkubwa sana kwenye fani ya muziki. Kwa mfano, kikundi cha Taarab cha Ikhwan Safaa ambacho kina miaka takribani 102/mia moja na mbili kinawezekana kuwa ni kikundi kikongwe barani Afrika na labda duniani hakijawahi kupewa tuzo yoyote.

    Msondo Ngoma Band ambayo ni bendi nzee (ina miaka takribani 43)kuliko zote za muziki wa dansi nchini Tanzania, zaidi ya hivyo Msondo na Sikinde ndiyo bendi pekee ambazo zimedumisha signal tune ya muziki wa Kitanzania hadi leo, au The Tanzanites (wana takribani miaka 38)sijawahi kusikia wameenziwa.

    Ukija kwa wanamuziki watunzi kuna kina Mzee Kiki, Cosmas Thobias Chidumule, Remmy Ongala na wengineo wengi tu ambao wametunga na kuimba miziki yenye maudhui mbali mbali ya kijamii, kisiasa na hata kiuchumi sijawahi kusikia wamepata tuzo.

    Kuna waimbaji ambao hadi hii leo hakuna mwimbaji ambaye ameweza kuwakwaa kwa sauti zao, kwa mfano Bi Shakira, Rukia Ramadhani, Elizabeth Sijira, Betty Enock, Carola Kinasha, Mzee Makame Faki, Mzee Khamis Shehe,Hassan Rehani Bitchuka, Cosmas Thobias Chidumule.

    Ukija kwenye muziki wa disco huwezi kulitaja Disco Tanzania bila kuwahusisha The Kussagas, Mbowes, Sudi Mwarabu au Nassoro Born City lakini sijawahi kusikia wametuzwa lolote.

    Kama mwenzangu una ufahamu zaidi kuliko mimi katika hivyo vipengele nilivyotaja naomba unielimishe.

    Asante.

    ReplyDelete
  7. Nimeelewa na kuheshimu wasiwasi wako, lakini sina uhakika kama tuzo hizo alizosaidia kuanzisha angeziita mfano 'Dandu Awards' ungetaka kujua yote hayo. Nadhani malalamiko yako yamelenga zaidi kwa kuwa tuzo hizo zinaitwa 'tanzania Music awards', kwa hiyo unaona ni muhimu zikawakilisha muziki wa tanzania na historia yake, hiyo ni kweli na nakubaliana na wewe.

    Lakini kama nilivyosema, alitutoka wakati tunamuhitaji zaidi. Naamini wakongwe wote wa muziki angetafuta njia ya kuwaenzi kwenye tuzo hizo. Na mimi sijui tuzo hizo zinaendeshwa na nani sasa hivi, I mean, hadi jina limebadilishwa. Kuna watu watakuwa wameiteka, na kuzitumia kupromote wasanii wao, hayo malalamiko nimeshawahi kuyasikia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...