


pia inafadhili Swahili Fashion week mwezi ujao
SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA RASMI
Kwa mara ya pili mfululizo wiki ya mitindo –Swahili Fashion Week (SFW) - itafanyika tena jijini Dar Es Salaam na kuwapa wapenda mitindo siku tatu zilizojaa shoo za mitindo za aina mbali mbali.
Swahili Fashion week ni siku chache za mitindo ya kisasa yenye mahadhi ya uswahili na vile vile hujumuisha wabunifu wa mavazi wenye vipaji kutoka sehemu mbali mbali nchini, nchi zinazozungumza Kiswahili na nchi nyinginezo. Katika onyesho hilo wabunifu huonyesha kazi za kipekee zenye mahadhi ya kiafrika zikijumuisha, nguo, viatu, mapochi na urembo mwengine.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa onyesho hilo la mavazi mwanzilishi wa SFW Mustafa Hassanali ambaye ni mmoja wa wabunifu maarufu nchini alisema mwaka huu Swahili Fashion Week inahamasisha ‘Mitindo kama biashara.’
“Swahili Fashion Week mwaka huu ni mwanzo wa ari mpya; tunaandaa onyesho litakalohamasisha mitindo kama biashara. Tunataka kukuza shughuli za mitindo nchini ili isiwe inachukuliwa kama fani ya burudani bali mojawapo ya njia za kukuza kipato.
Ulimwenguni kote fani ya mitindo ni moja kati ya fani zinazochangia katika uchumi wa nchi, hivyo basi na sisi tungependa kusisitiza umuhimu wa fani hii nchini ili watu waipe umuhimu unaotakiwa kama njia mojawapo ya kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa ujumla,” alielezea Hassanali.
Wiki ya Mitindo ya mwaka huu itajumuisha wabunifu mavazi 14 kutoka mikoa mbali mbali nchini na wabunifu 6 kutoka nje ya nchi na maonyesho hayo ya mavazi yatafanyika tarehe 4 hadi 6 novemba mwaka huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam.
“Swahili Fashion week inatoa nafasi kwa wabunifu wanaoibuka na waliobobea kuonyesha kazi zao ndani ya paa moja na hivyo kuwapatia nafasi wabunifu wakongwe kuwapa ushauri wale wachanga.
British Council inashiriki katika hili kwa kuaanda tuzo ya mbunifu asiyejulikana mwenye kipaji inayoitwa ‘Emerging Designer Award.’ SFW pia inatoa nafasi ya kipekee kwa wabunifu kukutana pamoja kubadilishana mawazo na pia kupata ujuzi zaidi kupitia warsha mbali mbali zitakazoandaliwa na Goethe Institute,” aliongeza Hassanali.
Kama ilivyokuwa SFW ya 2008, mwaka huu pia washiriki wa fainali za shindano la kisura wa Afrika maarufu kama ‘M-net Face of Africa’ watashiriki katika maonyesho hayo ya mitindo kama sehemu ya shindani hilo kwa kuonyesha mavazi.
Wabunifu wanaoshiriki katika SFW wanachaguliwa na bodi ya wana mitindo inayoitwa ‘Fashion Advisory Board (FAB)’ ambayo wajumbe wake ni pamoja na Emelda Mwamanga Mkurugenzi Mkuu wa Jarida la Bang, Mwanasheria Matukio Chuma, Mkurugenzi wa sanaa na promosheni wa BASATA Nsia Shalua, na mmiliki wa klabu maarufu ya starehe jijini Dar es Salaam Abigail Plaatjees.
Maonyesho ya Swahili Fashion Week mwaka huu yanaletwa kwa ushirikiano na kampuni za Vodacom Tanzania na ZTE.
Vile vile wadhamini wngine ni, Infinity Communications Ltd, REDDS, Southern Sun, Goethe Institute, British Council na BASATA.
Pia wadhamini wengine ni Ultimate Security, Primetime Promotions, Vayle Springs, ZG Designs & Films, Jan Malan Umzingeli, Choice Fm & Clouds fm, Mwananchi Communications Ltd, Brooklyn Media, 1&1 Internet solutions, Channel Ten, Imaging Smart, IMAN Cosmetics, Darling, Runway Lounge, Perfect Machinery na African Life Assuarance.
...kuslimu siyo kuingia dini ya uislamu...au mimi tu?
ReplyDeleteYou don't have to be a rocket scientist to know the secret behind Hassanali's weight loss, I am certain he went under the knife (Liposuction).
ReplyDeleteHey folks...its called weight loss surgery....Lmao
ReplyDelete.... aisee hata mie pia nataka kujua siri ya mafanikio mustafa toka bwanyenye hadi model kazi kweli kweli
ReplyDeleteSafi sana! Keep it up nasubiria siku hiyo ili nijue siri ya mafanikio
ReplyDeleteanon wa kwanza uko nje ya topic kabisaa hapo ni jinsi mustafa hasanali alivyopungua tukirudi kwa ishu ya mustafa hilo sio tizi wala mazoezi wala vidonge vya kukonda hiyo ni surgery alifanyia south africa asidanganye watu ati ni diet lol diet miezi miwili unakuwa kipotapo namna hiyo aah wapiiiii na jinsi alivyokuwaga ithili ya pepekale hata angefanya diet mwaka mzima asingekuwa jinsi alivyo sasa hiyo ni SURGERY TUUU FULL STOP!! tena wakati yuko south kwenye wall ya facebook akawa anadai amelazwa kule ati anaumwa malaria isshh kumbe alikukwa anakula kisu kupunguza mamichelini hongera kwa kupungua si useme ukweli tuu kwani utakufa mbona ni vitu vya kawaida sana??
ReplyDeleteSIRI YA MAFANIKIO NI NGOMAA
ReplyDeletemh! ok,basi ameloose weight.
ReplyDeleteNjia rahisi ya kuslimu ni kupata ngoma tu, unachuja mwenyewe bila kujishughulisha.
ReplyDeleteKuslimu ni kubadili dini kuwa Mwislamu iwapo unatumia lugha ya Kiarabu kutengeneza msamiati wa Kiswahili, yaani kutoka "kuwa Mwislamu" kuwa kuslimu, jambo ambalo ni sahihi kwa mantiki na muundo wa Kiswahili.
ReplyDeleteKuslimu inaweza kuwa kujikondosha au kupunguza uzito iwapo unatumia lugha ya Kiingereza kutengeneza msamiati wa Kiswahili, unakumbuka watu husema amevaa "slimu fiti" ambayo ni Kiingereza kamili katika matamshi ya Kibantu.
Kwa hiyo maana zote mbili ruksa.
Mwenyekiti Mtarajiwa BAKITA.
Mwanaume rijaliutakaaje umekunja nne ya kufumba hivyo!
ReplyDeleteKatoa siri ya kukonda kwenye gazeti la udaku la Shigongo. Na pia ni mchumba/mume wa Jacklin Ntuyabaliwe.
nimesoma udaku wanadai amefanyiwa operation ya kupunguza minyama sauzi aflika na special tritmenti alivyokwenda india.
ReplyDeleteThu Oct 15, 03:58:00 PM
slim= practise to become thinner in attractive way
lol @al musoma
ReplyDeleteAme "slim" ndio kuchanganya swahili -english huko...
ReplyDeleteMay be amefanya gastric by pass surgery....not sure labda diet tu.
nin kimempata huyu jamaa?alikuaga mnene sana sio ugonjwa umempitia kwel?manake wakat wote yuko na vimodo.du kali hiyo.
ReplyDeleteGASTRIC BYPASS SURGERY! Is that right?
ReplyDeleteNna hakika 100% huyu sio Mustafa original, huyu ni pacha wake ambae alikuwa yuko kwao huko india, sasa huenda huyo mustafa mwenyewe kaenda kwao vacation, then huyu pacha kaja kutuzingua, na hiyo siku ya swahili show ndo atakuja mustafa original (bwamnyenye), yuko vile vile kitambi maji!
ReplyDeleteNi kupunguza unene.
ReplyDeleteNYINYI WATU HAMNAGA HAKILI NDIO MAANA MNAROPOKA OVYO.HUYU AMEKULA PILIPILI ZA KIINDI NDO MAANA AKIPITAGA NAMUONA KAMA VILE ANADENGUA NA MIKONO YAKE. SISI WATU WASOMI KUTOKA MUZUMBE CHUKO CHA UNIVESITY HAYA YOTE TUNAYAJUA LAKINI YUNANYAMAZA TU KWA SABABU WE ARE EDUCATE PEOPLE LIKE ROGER MTAGWA NA MR. BLUE
ReplyDeleteHe got to be on crack.You can loose weight fast on crack and thats real.
ReplyDeleteexcellent bwana...however, mbona wakati umeslimu there are no beautiful girls in the pictures and and when you ere heavy weight, you were sorrounded by beatiful GIRLS all around you...can some explain me that?
ReplyDeleteHebu na yeye mustafa aache roho mbaya.Kuna watu kibao wenye unene kama aliokuwa nao yeye na wanahitaji msaada ili nao wapungue. Lakini yeye kila siku akiulizwa kafanya vipi hadi kupungua ili angalau na hao wengine walio wanene wafuate nyao zake yeye anabaki kutoa majibu ya kubabaisha tu. Kama si roho mbaya ni nini? Acha hizo wewe.
ReplyDeleteMustafa ana eating disorder, inaitwa anorexic, This guy barely eats na akila anakua na hasira, Mustafa ni anaogopa chakula sana na akijiona amekula sana, he feels guilty, hana siri ya mafanikio zaidi ya kua na mental disorder which is related to eating disorder.
ReplyDeleteHAYA NYIE WATU WA LEEEBOOZIII KWENYE MAKOTI TOENI HIZO LEBO SI MNAONA SUTI INAVYOKUWA.
ReplyDelete"Tarehe Fri Oct 16, 02:57:00 AM, Mtoa Maoni: PETER NALITOLELA
ReplyDeleteNYINYI WATU HAMNAGA HAKILI NDIO MAANA MNAROPOKA OVYO.HUYU AMEKULA PILIPILI ZA KIINDI NDO MAANA AKIPITAGA NAMUONA KAMA VILE ANADENGUA NA MIKONO YAKE. SISI WATU WASOMI KUTOKA MUZUMBE CHUKO CHA UNIVESITY HAYA YOTE TUNAYAJUA LAKINI YUNANYAMAZA TU KWA SABABU WE ARE EDUCATE PEOPLE LIKE ROGER MTAGWA NA MR. BLUE"
Ndo maana nchi haiendelei, kama wasomi mnakaa kimya huku mambo mkiyajua je yule mbongo asiyefahamu mnamsaidia vipi, au hiyo elimu unataka ikusaidie peke yako.... Mtaendelea kufa maskini kama elimu mliyopata haitawasaidia PUMBAVU ZENU!!!
Michuzi mimi moyo wangu umemdondokea dada Stella...kwa kweli kanivutia sana...kwa kifupi nimempenda..naomba nipe data zake zaidi..huyo jamaa wa pembeni ndo mdau wake nini...email yangu rashmaki@gmail.com
ReplyDeleteHAKUNA KISWAHILI CHA KUSLIMU UKIMAANISHA KUPUNGUA UNENE, UNAWACHANGANYA WATU KUINGIA DINI YA KI-ISLAMU NDO KUSILIMU
ReplyDeleteWewe mdau unayejiita Peter Nalitolela nadhani unamuharibia jina mshkaji tu..Peter nnayemjua mimi hawezi kuongea pumba namna hii..don't do that, jiite anony tu, tutakusoma..
ReplyDeletehuyo anayejiita Peter Nalitolela ni Nshimimana aka Dumisane
ReplyDelete