wasani wa tasnia ya filamu na muziki walikusanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Msasani, Dar, na kufanya usafi kuadhimisha miaka 10 ya kifo chake. Shughuli hii iliratibiwa na African Stars Entertainment, wamiliki wa bendi ya Twanga Pepeta, chini ya Mkurugenzi wake Da'Asha Baraka akisaidiana na Mamaa Dotnata, pamoja na kikosi kizima cha twanga pepeta na mastaa kibao wa filamu. Shughuli ilifana sana Mjukuu wa Mwalimu, Fortunata Nyerere, aliwashukuru wasanii hao kwa niaba ya familia
aisha madinda alikuwa mmoja wa wasanii waliofaidika na matunda ya Baba wa Taifa kwa kujipatia mzigo wa nazi kwenye bustani ya nyumbani kwa Mwalimu
Mamaa Dotnata akiwa kazini
Dk. Cheni alishughulikia taa za bustanini
JB naye alikuwa bize kutwa nzima kubeba taka

anko alikuwepo. hapa anakula konozzz na lillian internet, Lwiza Mbutu, Janet Isinike na paparazzi Muhidin Sufiani
wanenguaji wa twanga wakipepeta takataka zote
Mjukuu wa Mwalimu, Fortunata Nyerere, akiwashukuru wasanii hao kwa niaba ya familia
baadhi ya wasanii hao wakipozi baada ya kazi
Ujumbe: Mtandao wa
umetoa toleo maalumu la kukumbuka siku hii adhimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. anko, kwa kweli unafahamu kula nchi kwa njia mbalimbali. shukrani. thanks-a-million for the informative pictorial narratives. shukrani.

    wathenia walisema, "a picture is worth a million words."

    ReplyDelete
  2. anko kwenye huo uzi wa carlsberg wakati wa kula konozz umetoka bomba sana nana kale kafulana kapo jalalani je wewe ulisaidia kidogo manake najua hukuwa biiize kufotoa tu anyway kazi nzuri ila bustani imepauka sana na pia hakuna flowers zenye mvuto kupo kawaida sana hivi kakuna shamba boy huko??
    miss michuzi

    ReplyDelete
  3. THIS IS SOMETHING BEAUTIFUL EVER HAPPENED, I LOVE THIS AND AM SO MUCH PROUD OF THOSE ARTISTS AND I WISH MANY OF US TO DO SOMETHING FOR THE LATE MWALIMU

    ReplyDelete
  4. Anko pamoja na yote hivi ni kweli hao wasanii hapo walikukuwa "wakipizi" au wakipozi? tafadhali rekebisha hilo kabla hujashambuliwa na wanablog wako.

    Mdogo wako - Ughaibuni.

    ReplyDelete
  5. Ahsante sana uongozi wa ASET kwa kubuni na kuratibu shughuli ya kihistoria kama hii. Kwa kweli wasanii wote wa luninga na twangapepeta mnastahili sifa kwa kuwajibika ipasavyo. Bila kukusahau wewe Mzee wa nani hii kwa kushiriki pia kwas njia moja au nyingine.

    ReplyDelete
  6. kaka hebu rekebisha kwanza hii kauli chini!!!, ...wakipozi na sio wakipizi

    baadhi ya wasanii hao wakipizi baada ya kazi

    ReplyDelete
  7. Picha ya mwisho wanaPIZI sio, nimeipenda hiyo.

    ReplyDelete
  8. Hivi kweli kabisa hiyo familia ya baba wa taifa wanashindwa kufanya usafi/ kutengeneza bustani wenyewe mpaka wakasaidiwe? Na hapa Michuzi hajatunoesha "before" pictures, kwamba palikuwaje hadi uongozi wa ASET ukaamua kupashughulikia!!

    Hata sisi wengine tumefiwa na baba na familia zetu ni za kawaida kabisa lakini tumeendelea kutunza mandhari nyumbani!!

    Duh! Aibu. Au basi serikali ipachukue kama sehemu ya Makumbusho ya Taifa kama hampawezi?

    ReplyDelete
  9. MBONA KING OF COMEDY MR.KINGWENDU SIJAMUONA? AU YUPO UWANJA WA FISI ANAPIGA MATAPUTAPU KWA KWENDA MBELE?

    ReplyDelete
  10. Hii safi sana, pengine watatumia tasnia yao kuhamasisha kizazi kipya kupiga vita ufidhuli ambao baba wa taifa alipigana nao hadi kifo chake.

    ReplyDelete
  11. Kwa hiyo usafi unafanyika mara moja kwa mwaka?

    ReplyDelete
  12. Huu wizi mtupu, eti kusafisha ina maana hakuna wafanyakazi hapo wakutunza nyumba na kusafisha, ndio maana ina bore sana kila siku kusikia mambo ya ujamaa , ina maana ujamaa ni uchafu na kutosafisha sababu eti uko simple?

    Kama kweli mlitaka ku muenzi baba wa taifa nadhani mlihitaji kufanya hayo kwa watu lio kweli na mahitaji ya msaada, , mnge safisha meeneo ya sio safishwa au hata kwenda picknic na watoto wa mitaani , kuliko eti kusafisha huyo Mansion hapo wakati ina wafanyakazi wa kumwaga ndani

    ReplyDelete
  13. anony 15.9:00 kweli umeshiba maharage.vuta vuta time ukalale.

    ReplyDelete
  14. We mjuba hapo juu(Oct 15,9:00) hueleweki kinachokutatiza ni nini Ujamaa? wafanyakazi wa ndani? au wasanii? Inawezekana uko frustuated so kila kitu kwako ni kero.Jaribu kutulia au kufanya mazoezi ya mwili kabla hujaenda next level.

    ReplyDelete
  15. mdau wa TwangaOctober 16, 2009

    Safi sana Michuzi na uongozi wa ASE.
    Hata hivyo, usafi wa mazingira ya kwa Nyerere uendane na wa miili yao wenyewe kila siku. Wapunguze mapouda na michubuo. Na kama kuna wanaopuliza mioshi inayosababisha uchizi waache kabisa!

    Halafu nguo walizovaa leo akina dada wa Twanga zimewapendeza na wamekuwa watoto wazuri kuliko zile zao za kila siku majukwaani. Kama mnaweza kuona aibu kwa Nyerere oneni aibu pia Lidaz klabu,sigara na hata kwa Biliz.

    Michuzi hii huwa aiminywi maana ni wosia!

    ReplyDelete
  16. NILITOWA WAZO KAMA HILI, HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA, SIKU YAKE WATU WAJITOLEE SEHEMU MBALI MBALI KUFANYA USAFI NA UJENZI NA MICHANGO MBALI MBALI, NAWAPA HONGERA WASANII NA MOYO WAO SAFI

    ReplyDelete
  17. KWELI TANZANIA BADO NYUMA.KIONGOZI KAMA MWALIMU NYUMBA YAKE CHAFU????hadi twanga pepeta wakafagie?????
    mdau money uk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...