Habari Bwana Blog,
Nafurahishwa sana na Blog Ya kwako,na leo naomba uni oneshee hii matatizo yamenipata hapo Kilimanjaro Airport.Mimi natokea Rwanda naishi Ulaya,imetokea kusafiri kutokea Kilimanjaro,lakini nilipofika pale nilizuiliwa ku board Aircraft wakaniambiya kuya mimi ni mrwanda sitakiwi kuruka pare,kwa sababu pengine nimekimbia Refugee Camp au nikienda uraya nitajiripua sitorudi.Arakini cha kushangazya ni kuwa mimi mwenyewe ninaishi kwa sheria za Ulaya na nirikuja Arusha kutemberea ndugu zangu tu wanafanya kazi mahakama ya Genocide pale.
Sasa Nikawekwa ndani kama 3 hours na nikamiss Flight,then offisa akaniambia kuwa hii visa yako sio ya Ulaya na ni ya RUSIA,nikamfahamisha kuwa hii resident permit ya Grek,(greece) BASI akaniambia kuwa atanisaidia kusafiri nikimpatia 2000.00 us au atanirudisha Rwanda kupitia Immigration,sasa Mimi nimepeatiwa hii resident under humanitarian kule Greece na sitakiwi kuenda Rwanda kwa kuwa ndio nime claim kuna matatizo,kwa hiyo ningepelekwa Rwanda Ningelienda mahakama.
Kwa kuwa ilikuwa Usiku sana na simjui mtu pale Kilimanjaro Afisa akaniambira kuwa nikitoka atakuja dereva wa Taxi nimpatie hiyo hela na atanisaidia Jumatatu kusafiri,kwa kuwa yeye hafanyi kasi Saturday and Sunday anaingia Mchana,so nikakubali Kutowa 300 USD. nikapatiwa sehemu ya kukaa,na wakanizuia nisitoke nje kwa kuwa mi ni mgeni nitapata matatizo pale Moshi.
Kutoka Thursday night hadi ikafika Jumatatu,kwa kuwa nilikuwa sina jinsi,na passport yangu ipo mikononi mwa ofisa nikawaomba kuwa sina hela ya kutosha kwa hiyo wakaniambia niwapatie tena 600 us ili wanisaidie kuruka,so ilipofika wakati wa safari wakanipeleka KIA airport na wakaniambia niende tu kila kitu ni kizuri,lakini nilipofika tu nikawekwa ndani tena na sijaruhusiwa kuongea chochote,hadi asubuhi wakanipatia Passport yangu baada ya kuwapatia .50.00 us doller,na kuniacha niende,sasa kitu vile sisikii ni kuwa nimepoteza US.1450.00 kwa KLM TICKET,950.US KWA Mikono ya Polisi,na kuniwacha nimerudi Rwanda bila hata ya shililingi tano.
Nimesaidiwa kufika Rwanda kupitia Kahama bila ya kuonesha Travel document yangu kwa kuwa ingekua matatizo,na sasa nipo Rwanda na nimepoteza hela yote na watu nikiwapigia sim hawaongei na mimi,lakini nawajua kwa majina na namba zao ninazo.
SASA JE HAPA NIFANYE NINI KUPATA HIZO
HERA ZANGU?
ASANTE NASHKURU SANA
Mdau Kigali


...si ajabu afu hii stori ya kutunga...
ReplyDeletepole sana ndugu yangu, kwa bahati mbaya sana Tanzania yetu wafanyakazi wengi wamekosa uaminifu na uadilifu. Watu unaotarajia kupata msaada kutoka kwao ndiyo hao wanakufanyia mabaya. Hao si askari bali ni majizi tu. wanaipaka matope nchi yetu hadi haitamaniki siku hizi. Serikali nayo imekaa domo wazi haijuwi la kufanya.
ReplyDeleteNashindwa hata nikupe ushauri gani, ila ninachoweza kukuambia ni kwamba ni vigumumu kupata pesa yako. Natamani tungewapata kama akina Sokoine na Mrema kwa sasa angalau tunge kuwa na imani. Kwa sasa sina imani na Tanzania na muda si mrefu itakuwa ni failed state! Remember my words! There is very little to be optimistic about in TZ.
We! wacha hiyo maneno ya kusingizia polisi yetu!
ReplyDeleteUnachanganya mambo, mara unasema una permit ya kuishi Greece,mara Rwanda kuna matatizo we ni mkimbizi, na sasa umerudi Rwanda na unajiita mdau Rwanda. Vipi wewe?
Kama ungekuwa na pasipoti halali, ticket ya ndege wasingekuzua. Nadhani tu ulijichanganya.
Na sasa we kama mkimbizi mbona umerudi kwenU? Au nyi ndo wakimbizi wa njaa mkifika huko Ulaya mnaanza kuipaka nchi yenu matope? Sasa yamekurudi?
Sasa humu tutatoa msaada gani wakati pesa umetoa mwenyewe?Rushwa niadui wa haki,umetoa rushwa imetoa haki yako!Kwa nini usiwashirikishe ndugu zako wa mahakama ya genocide siku zote hizo?Mi naona hiyo pesa imeenda kwa kuwa huna hata udhibitisho wa kumpa mtu.utashitaki vip?
ReplyDeletesasa wewe si umefaili asilum inakuwaje tena unakwenda Rwanda? si ungebaki tu huko huko Ulaya, umekuja Arusha kufanya nini sasa. umekana kwenu then unataka kutumia nchi za wengine kama kivuli. Any way, kwa msaada tu nakushauri andika barua inde moja kwa moja kwa wakubwa wa hapo KIA, then orodhesha hizo number zao za simu then complain about what happened, hao watu wanatakiwa kusimamishwa kazi mara moja
ReplyDeletepole sana ndugu yangu, hayo ndio mambo ya afrika, kama uliombwa rushwa na ukatoa sahau habari ya kuuliza utaipataje hela yako uliotoa rushwa, wewe ulishasikia wapi polisi wanarudisha change ukiwahonga? mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana makosa hivyo na wewe una makosa pia ilistaili ushitakiwe kwa kutoa rushwa, kwa nini usiwaone viongozi wa ngazi za juu wakusaidie? wewe ni refugee na una haki zote za msingi hiyo imekula kwako pole sana...
ReplyDeletePAMOJA NA KUKUPA POLE SANA LAKINI NINAWEZA KUSEMA KUWA KAMA KUNA NCHI YENYE RUSHWA NA USUMBUFU WA KIJINGA NI TANZANIA IDARA YA UHAMIAJI HAIFAI KABISA RUSHWA TUPU NA USUMBUFU RUSHWA ZA KIMASIKINI KWA KWELI INAUMA,BADALA YA KUSHUGHULIKIA WA PAKISTAN WANAOINGIA KILA SIKU NA WACHINA MTU ANAKUELEWESHA UNACHUKUA CHAKE HARAFU UNAPOTEA HII KWELI INAUMA WENGI WANAFANYIWA HIVYO MIMI NI MFANYA BIASHARA WA TANZANIA NINASEMA KILE CHA KWELI NASAFIRI SANA NAONA UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM,
ReplyDeleteKWANZA POLE SANA MDAU
ReplyDeleteMIMI NAFIKILI UTOKE KIGARI MARA MOJA URUDI TANZANIA UENDE MPAKA DAR KTK UBALOZI WA NCHI YAKO ILE UNA DOCOMENT NAYO AMBAYO NI GLICK KISHA USITOKE PALE WAELEZE MATATIZO YOTE WAO WATAKUSAFIRISHA NA WATAJUWA WAFANYE NINI UNACHOTAKIWA NI KUSAFIRI TU WALE MAJAMBAZI WA ARUSHA HAWATAKURUDISHIA PESA ZAKO KWANI HATA UKAWACHUKUWA CURT HUTAKUWA NA USHAHIDI NA PIA ITAKUCHUKUWA MDA MREFU. KURUDI RWANDA UNAPOTEZA POINT KTK UBALOZI WA NCHI YAKOKWANI WATAKUULIZA ULIPATWA NA MATATIZO LINI JE ULIKUWA WAPI? MAMBO KAMA HAYO POLE SANA UJUWE AFRIKA IMEOZA YOTE INANUKA RUSHWA
WE MTAFUTE PINDA ATAKUSAIDIA UKIENDA POLICE U WONT GET ANYTHIGN THERE SANA SANA WATAKUOMBA TENA ONGO! WE NENDA SERIKALINI UA ANY un ORGANISATION! FORGET ABOUT POLISE IN tz THEY ARE USELESS!
ReplyDeletepole sanaaa ndugu yangu,nimesikitishwa sana na yalio kupataa...ushauri wangu, kamaa una wajuaa hao mapolisi walio kuchukulia hela, unaweza kwenda PCB..toa maelezo yako, au tafuta chombo cha habari na uwanike majina ya hao wala rushwaa atharani,wanatiaa kinyaa kwenye nchi yetu.pole
ReplyDeletepole sana
ReplyDeletemdau mussa
Pole sana mdau.
ReplyDeleteLakini inasikitisha sana kusoma maoni ya wadau hapo juu, kumshutumu huyo jamaa kana kwamba yalio mtokea ni kwa sababu ya ujinga wake. Lakini nachotaka kusema leo hii ingelikua ni mmoja kati ya hao wadau hapo ndo wange elewa vizuri mdau kilicho mtokea. Kwa kweli Idara ya uhamiaji IMEOZA na INANUKA kwa rushwa, Mpaka imesababisha hata Idadi ya utalii hapa TZ kupungua na watalii wengi kupitia kwa watani zetu hapo jirani ili kuingia Tz, na hivyo kusababisha serikali kukosa mapato ya kutosha kupitia secta hiyo.
nenda kwenye magazeti,radio clouds, television hapo ndio kiboko ya wezi wote wa mjini waumbuliwe waeleze kila kitu na alafu wataje hao maaskari majina yao walio fanya hivyo ili kukomesha watu kama hawa imekua kero.kama haijakukuta haitakuuma ikikukuta utamkumbuka huyu.ikishindikana nenda ubalozini kwako watakusaidia.
ReplyDeleteHebu cheki maneno yake "kuruka pare", "nikienda uraya", "nitajiripua", "nirikuja", "arakini" taking only few words. Jamaa mkurya anazuga tu.
ReplyDeleteAsalaam Alykum bro sisi wantanzania kweli tunakasumba kwani mtu akisema kitu sharti tumuone muongo au katunga je atapata faida gani kusema oungo?
ReplyDeleteWajinga ndio waliwao.
ReplyDeleteSijakufahamu naona unajizongazonga tu.Wewe kama ulikuwa na document halali haikuwa na haja ya kutoa rushwa,inaonekana wazi wewe ni mbabaishaji tu.Sioni haja hata ya kupewa pole.
Mambo vipi kaka??Hope ishu zinakwenda salama kabisa....kwa ujumla wengi wao waliotoa comment hapo juu naona wapo TZ ndio maana wamekulaum...Ina maana mtu akisafiri haruhusiwi kutumia nchi jirani??Kwa ujumla nimekuelewa matatizo yako na pia hiyo ni sheria ya kila nchi kwamba ukipata travel document yao kule nyuma kabisa wameandika kwamba huruhisiwi kwenda kwenye nchi yako na hiyo passport nadhani ni hivyo...
ReplyDeleteNa wewe huna makosa ulivyofanya kushukia nchi jirani nadhani wengi wetu ndio tunafanya hivyo...Lakini usijali mkubwa sasa wewe problem yako sasa hivi ni nini??Kama tichet bado unayo na ime expire sasa cha kufanya wewe nenda kwenye ubalozi wako dar then ukifika pale watakusafiri free of charge na waeleze problem zao zote.....Pia kama ukihitaji msaada zaidi maana umesema unawajua hao jamaa na namba zao za simu unazo basi jibu hapa then tutawasiliana ukifika dar uje ofisini alafu alafu tujue nini cha kufanya...Sidhani kama serikali ina amri ya kumzuia mtu kusafiri...Angekuwa na passport ya rwanda sawa lakini ana passport ya grece alafu unasema eti atakwenda kujiripua wakati passport anayo ya hiyo nchi na pia umeonyesha kabisa ticket unataka kutoka......Anyway pole sasa basi wewe fanya hivyo kama upo rwanda njoo tz then fanya kama nilivyokuambia hapo.......
Ahsante!!
Pole mtoa mada,haya mambo ni ya ukweli kabisa,mimi mwenyewe yamenikuta hapo Dar es salaam mara 2,na Ethiopia mara moja(ambapo walinirudisa Tanzania kwa kushindwa kujua document yangu ni ya nchi gani na pia kwa kuwa iliandikwa lugha hii ΑΔΕΙΑ ΠΑΡΑΜΟΝΗΣ,Ukweli ni kuwa lugha ya kigiriki inafanana sana na ki rusi herufi zake na ndio maana wakakwambia kuwa ni ya urusi,ila usijali kwa hela imekwenda na hiyo ndio Bongo,Sasa tushaizowea na ndio maana baadhi yetu baada ya kulaani hayo mambo wanasema ni ya uongo.yaani yaendelee ,Ndio wale wanaosema Licha ya barabara kuwa na mashimo wacha iwe na visima lakini bado tutaipa kura.......hatujali,instead ya watu kuelimika ndio wanazidi kuwa wapumbavu,kwa kuwa wao sio anga zao hizo Airport,na sawa na hao waliosema kuhusu barabara kwa kuwa wao hawamiliki usafiri,lakini wajue kuwa siku moja watasafiri au watamiliki usafiri na mambo yatawakuta.Licha ya kukupa pole mara ya pili tafuta pa kurukia kwa kuwa umesema kuwa una humanitarian hutoweza kurukia kwenu Rwanda basi karukie UGANDA AU KENYA kwa nini tena uje TANZANIA?Mimi mwenyewe ni Mtanzania na sirukii Jiji la Maraha ila narukia kwa yakhe kule Zanzibar hadi Kenya mbele kwa mbele.Kwa kuwa wenzangu wengi wamekua wakitoleshwa hela pale AIRPORT na document za halali.Pole sana.
ReplyDeleteAh! haya matatizo ya Airport zetu ni ya kawaida tu,Ukishakua na rangi nyeusi basi hata uwe na passport kutoka mbinguni utakoma tu,Lakini ukiwa MZUNGU tu wafanyakazi watakubebea hadi mabegi yako ndani ya ndege,inasikitisha sana,mimi nilikutana nayo hayo Dar Airport mwaka 2006,baada ya kucheck in nikafuatwa Juu wakati nasubiri ndege,nikaombwa passport na nikaulizwa kwa nini wewe mtanzania unaishi ulaya,Je serikali inatambua hilo?Nilishangaa sana kwa maswali kama hayo,baada ya kuwazidi kwa hoja wakaniambia je unachochote umebakisha katika TZshilings,nikawambia kuwa nimempatia Bro nilikuja nae nje kwa sasa sina kitu kabisa,basi nikapatiwa namba ya sim na mtu mmoja anaanzia jina la G.. na akanihakikishia kuwa kama nina mtu ana tatizo lolote lile yeye anauwezo wa kusolve.Cha kushangaza huku ughaibuni kuna watu wanajisifu kuwa walitoa 50 - 100 doller ili wapite ijapokuwa wanavitambulisho vya halali,sasa haya mambo yatabadilika lini jamanii?(mdau Buruda)
ReplyDeletePole mdau Rwanda,hayo yanatokea kila sehemu sio Tz tu hata huko kwenu,Pia nimefahamu kuwa wewe sio ulitaka kutoa rushwa ila walikuforce utoe hela na kwa kuwa ulikua ugenini na huna pa kuenda wala huna msaada na kwa kuwa ndege pale zinaruka usiku wala sikulaumu,Maswala yapo kama kawaida,mara moja nilikua nasafiri nikakutana na msichana na mvulana walikua na visa ya Italy,tulikua pamoja kwenye document verification pale JULIUS NYERERE AIRPORT.Mimi mwenyewe nilitakiwa kila aina ya kitambulisho kuthibitisha ukaazi wangu wa ulaya,Driving licence na mambo kibao,lakini ulaya ninayokaa mimi hiyo leseni ni sawa na kuezeka bati hadi uipate harama zake,cha kushangaza sijui kama ni meneja wa Swiss au Mkubwa tu,alitufata pale kwenye Document Check akakaa nyuma yetu kama 3 minute bila sisi kufahamu,then akaanza kuwashambulia wale wanaochek document kua wao kazi yao ni kucheck kama ni genuine au sio,na si kuuliza maswali,kwa kuwa huko ubalozini washaulizwa ndio wakapatiwa hizo visa kwa sasa mtakua mnatuchelewesha kuruka NDEGE,mambo ya kuuliza mtarudi au mtafanya nini huko mnapokwenda sio ya kwenu,basi ndio wakaachiliwa pamoja na mimi,basi pia nikafuatwa na askari kuniuliza tena maswali akanisaidia hata kujaza boarding card nashkuru,na pia akanifuata juu kunitaka chochote lakini sikuwa na hela.Kwa ufupi haya mambo ni yakubadilika tu kama mshahara mtu haumtoshi basi atafute kazi nyengine na sio kutunyanyasa.(Mdau RINKEBY)
ReplyDeletepole sana. Ushauri wangu kwako ni huu.. Rudi tanzania haraka kisha nenda ubarozi wa ugiriki lakini usiwaambie kama ulifika rwanda watakusaidia kurudi ulaya na hizo pesa ulizotoa sahau nazani wausika wa rushwa washaona malalamiko yako watayafanyia kazi, Be strong n stay positive maneno ya waosha vinywa yasikuuwe nguvu
ReplyDeleteKuna wadau wanachangia hapa huenda nao ni matapeli au ndugu zao matapeli au wanafahamiana na hao matapeli.Uhamiaji ni Uozo.Wanamdhulumu huyu mtu kwa kuwa tu ana Visa ya kuishi Greece.Kama mdau mmoja hapo juu aliyekupa ushauri nenda nchi jirani Kenya au Uganda na mojakwa moja nenda ubalozi wa Greece au nchi yoyote ya EU Uwaeleze shida yako na watakusaidia ipasavyo kwa kukupa nauli na wewe kuweza kusafiri.Ila ukifika Greece tuma mashitaka kwa Rais Kikwete au Pinda na huu ni wakati wa kujiandaa kwa uchaguzi suala lako litashughulikiwa
ReplyDeletePia tunaomba uwataje majina hao wajinga humu ukumbini
jaribu kutafuta Mabalozi wa EU watakusaidia ndugu yangu pole sana na hii inatia aibu sana Uhamiaji Bongo!!
Pole sana kwa shida uliyopata.
ReplyDeleteNamba hii hapa ya Mkuu wa Polisi wa Tanzania (Inspector General of Police) +255 754 785557.
Kama shida yako ni ya kweli (tafadhali usipige kama huna hakika na shida yako), atakusaidia na utasaidia wengi wanaopata shida kama yako.
Andika email kwa Jeshi la Polisi la Tanzania, copy kwa Greek authorities (if you are considered Greek citizen). Weka majina na namba za polisi na maofisa wa Uhamiaji KIA waliokusumbua na kuchukua hela zako.
ReplyDeleteHakikisha email hiyo inaenda kwa Mkuu wa Polisi pia (IGP).
Email: phq@policeforce.go.tz
Yaani hicho kiswahili chako lazima wakutilie wasi wasi
ReplyDeleteNdugu,wakati tuna deal na allegations kama hizi ni muhimu kuwa makini hasa ku verify "authenticity" na "accuracy" ya allegations, ili kubainisha endapo ni kweli yanayosemwa yametukia,wakati na sympathaze na mlalamikaji, assuming kuwa yaliyotokea ni kweli, aidha, najaribu kujiuliza, katika mazingira kama hayo, kwa mtu wa kawaida, reaction ya kwanza ingekua ni kuwasiliana na "ndugu" zake wa arusha aliotoka kwao, maana ni watu wake wa karibu,kwa wakati huo,na kuwaeleza juu ya tatizo lililomtokea, tungetegemea wampe msaada..mlalamikaji haonyesha any such references!well, najiuliza tu,katika ku test validity ya story hii,kwani ingawa kuna umuhimu wa kufuatilia malalamiko kama haya,ni vyema vilevile tuwe waangalifu katika kulinda mustakabali wa watu na nafasi "kazi" zao especially kwa kuwa allegations za corruption if proved to be true to have happened (by mahakama) matokeo yake ni kuharibiwa kwa maisha ya mtu na pengine familia yake kwa ujumla, ingawa inawezekana ki uhalisia hakutenda kosa hilo,alishindwa kesi kutokana na "technicalities", wanasheria wanajua ni nini nichoongelea,
ReplyDeletesijatoa hukumu, nafikiria tu!
you wish. bwahaa ahahahaaa
ReplyDelete= = =
Buffalo (karibia na Greece/Ugiriki),
New York
pole sana, hii ilitokea kwa binti mmaoja aliyekuwa akisafiri kupitia tz kwenda uk, naye alisumbuliwa hapo dar na siku aloyopanga kuondoka walimzuia kwa sababu za kijinga(kwa nini anaondokea Tz na sio Burundi) aliwaona mkuu wa uhamiaji na siku ya pili alipoenda air port alihudumimiwa kama VIP, Those guys are useless, sheria hawajui kazi utafuta kupewa ushuru, once again report case yako uhamiaji nahidi utashugulikiwa
ReplyDeleteMatatizo kama hayo yapo kila nchi Tanzania, Rwanda, Ufaransa Ethiopia nikitaja nchi chache tu. Ila nchi zingine hawakuombi rushwa na taratibu zao zinaeleweka kiasi.
ReplyDeleteMfano Ethiopia uwanja wa ndege Bole Addis Ababa nilizuiliwa kuendelea na safari yangu toka DSM kwenda London via Addis Ababa.
Kisa Jamaa wa Ethiopia Airlines na uhamiaji Addis Ababa Bole Airport wakasema wanaogopa kubeba abiria 'haramu' sije wakapigwa faini ya paundi 3000 London. na pia Dar-es-Salaam ni kitovu kikubwa cha abiria haramu wa kimataifa.
Basi nikazuiliwa kuendelea na safari na pasipoti yangu ya Uingereza kuzuiliwa uhamiaji Bole Airport, mpaka nionyeshe leseni yangu kuendesha gari Uingereza, kadi za benki za Uingereza au cheti cha kuzaliwa cha Uingereza!
Leseni sikuwa nayo mfukoni wala cheti za kuzaliwa, ila nilisita kuwaonyesha kadi zangu za benki. Hivyo baada ya kujaribu kuwaelewesha hawakutaka kuelewa kitu. Hivyo nikasema ubalozi wa Uingereza DSM una taarifa ya raia wao wa Kiingereza kuondoka Tanzania hivyo tuwasiliane na Ubalozi wa Uingereza hapo jijini Addis Ababa.
Hivyo wakasema kwa utaratibu wao wanaizuia pasipoti yangu, wakanipatia fomu nijaze na ikagongwa muhuri wa "On-Transit Viza' ili nitolewe Airport nijilipie hoteli Addis Ababa na Kesho niungane na abiria wengine wenye matatizo mbalimbali kwenda balozi zilizopo Addis Ababa kuthibitisha uhalali wa pasipoti zetu,viza n.k kwa masharti ikiwa pasipoti zetu ni halali wataturejeshea gharama za hoteli na chakula.
Asubuhi nikafuatwa hotelini nikateremshwa na kibasi cha Ethiopia Airlines ubalozi wa Uingereza Addis Ababa. Maofisa wa ubalozi wakafanya kazi yao na kutoa barua ya uthibitisho kuwa pasipoti ni halali na hakuna tatizo.
Nikapoteza siku 5 Addis Ababa kutokana na mkasa huo, ila nilirejeshewa gharama za hoteli na chakula na kuendelea na safari yangu kurudi London.
Hivyo ni muhimu wasafiri kuwa na mikakati ya safari kama kuripoti ubalozini, kusindikizwa na jamaa zako na kuwa na contact details za mawasiliano kujinasua toka matatizo kama hayo.
Mdau
Jijini London.
Oh man, this is a scam,hawa ni wezi kwenye internet, Tanzania is one of the good African countries
ReplyDeletehuyu bwana muongo kabisa, anataka
watu wmuonee huruma waanze kumpelea pesa,wake Tanzania people
KAMA WEWE KILA KITU UNACHODAI NI HALALI, WALA HUJAPOTEZA KITU TENA UNAWEZA KUWAFUKUZISHA KAZI HAO WATU, RUDI TANZANIA NENDA UBALOZI WA GREECE KAJIELEZE, NA NENDA KWA VYOMBO VYOTE VYA HABARI KAJIELEZA WATU WAONE USHENZI HUO NA ANDIKA BARUA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KOPI KWA BUNGE, SPIKA, WAZIRI MKUU NA RAIS WA TANZANIA PAMOJA NA CNN NA BBC, USIOGOPE KITU HUWEZI KUPOTEZA KITU KAMA NI KWELI UNACHODAI NI HALALI NA HATA KAMA SI HALALI, NILISAHAU PIA KOPI KWA EU BRUSELS HEAD QUATER KUWA KAMA KICHAA HIVI WACHAFUWE KABISA TUKIKAA KIMYA HATUWEZI KUKOMESHA RUSHWA NA VITENDO VYA UONEZI, NA WEWE MICHUZI UNAJUKUMU LA KUWAFICHUWA HAWA WATU WA AINA HII NI LAKO KAMA MWANDISHI WA HABARI. I THINK YOU KNOW HOW TO PRESENT TO THE PUBLIC SUCH KIND OF ISSUES WITH DISCLAIMER CLAUSE. tANZANIA IMEOZA, PIA NAOMBA WATU WA SERIKALI WANAOSOMA HII HABARI KUCHUKUWA HATUA NI KAZI YAO SI LAZIMA MTU AJE KWAO KULALAMIKA HII HABARI TU INATOSHA. NDO MAANA TUNASHINDWA KUWACHUKULIA HATUA SAHIHI WATU WANAOIBIA SERIKALI NA UMMA KWA SABABU TUNAKUMBATIA WATENDAJI WABOVU SERIKALINI NA TUMEFANYA RUSHWA NI UTAMADUNI WETU.
ReplyDeleteMIMI SINGETOA WALA SENTI TANO MPAKA TUNGEFIKA MAHAKAMANI KUWEKANA WAZI, UGEKOMAA TU, NEXT TIME USITOWE PESA KAMA 100% UKO HUNA MATATIZO NA DOCUMENT ZAKO
ReplyDeleteUgiriki ni memba wa European Union (EU), hivyo hata kama hakuna ubalozi wa Ugiriki Tanzania au Kenya, wasiliana na ofisi za European Union(EU)katika nchi yoyote ya Afrika Mashariki au nchi yoyote mwanachama wa jumuiya hiyo ya Ulaya.
ReplyDeleteNina uhakika utasaidiwa na EU kuwasiliana na ofisi za mambo ya ndani/nje Ugiriki, na mambo yako yatatatuliwa kirahisi baada ya mawasiliano na lawyer, marafiki Ugiriki.
Mdau
Iceland.
Wahenga wanasema,ukimpatia uhuru mpumbavu aelimike basi anakua mpumbavu zaidi,Haya mambo hata kama ni ya kubuni,basi yanatokea tu ni kweli,na sio Tanzania tu,Kama mdau hapo juu alosema alipata matatizo ETHIOPIA,mimi mwenyewe nimepata matatizo hayo hayo na pia natokea Greece,Kwa kweli lugha ya kigiriki au document za kigiriki zina matatizo sana kutokana na kuandikwa lugha yao tu,Na hii ni kipande tu cha barua niliyotumiwa baada ya kufungua claim nilipofika Greece,This has reference to your e-mail dated 31 March 2008 regarding your travel experience with Ethiopian while travelling from Zanzibar to paris via Addis Ababa .
ReplyDeleteWe sincerely regret the inconveniences you might have went through due to the reported incident.
Airlines are basically responsible to give air transport and passengers are expected to comply with the government travel requirements; present, exit entry and other required documents. One of the means to find out about the visa requiremnet is from the designated consulate of the country of transit or destination country.Lakini kwa kuwa siku niliyozuiliwa safari ilikua ni kipindi cha easther na ilikua ni Alhamis usiku na Ester ilianza Ijumaa hadi jumatatu,ilishindikana kuongea na Balozi wa Kigiriki kwa hiyo ilibidi niombe uhamiaji wanirudishe Tanzania,basi wakaibadilisha ticket yangu ya kutoka Bole airpot kwenda Paris na kuifanya ndio ya kurudia Tanzania ili kukwepa harama za usafirishaji,na Uhamiaji wakaniambia kuwa wataandika kuwa nimerudi Tanzania kwa Freewill,ili nisipate matatizo na Nilipofika pale Tanzanzania nikapatiwa Passport zangu zote 2 pamoja na supporting document na Flight Captain,lakini zilidakwa na Maofisa wa Uhamiaji ijapokua Captain alisema kuwa tumemzuia kwa kuwa airline tuna haki ya kumzuia mtu asisafiri,haikuwa hayo niliwekwa katika chumba pale Airpot pamoja na watu wengine walionieleza kuwa wametokea Brazil na wamekamatwa kwa kesi za Unga.nilikaa pale kama 2 hours hakuna alienishuhulikia hadi nilipokutana na kijana mmoja JINA NALIHIFADHI akaniambia kama kuwa bosi anasema umpatie chochote ili akuchukue maelezo kesi yako sio kubwa,lakini kwa kuwa Nimeshakua mgeni Tanzania na nilikua nasumbuliwa na jino sana ijapokua nilipatiwa huduma pale pale ndani,ilibidi nitoe hicho chochote,na kweli haikufika dk 10 nikapatiwa document zangu na nikachukua Swiss Air hadi Greece via Zurich.lakini nilipofika swiss pia nilitiliwa mashaka ya karatasi yangu ya kigiriki kwa kuwa waliona nimekata ticket TENA ya oneway kutokea DAR,Nikawafahamisha yalionitokea ndio wakaniachia bila uchunguzi zaidi.kwa kweli haya mambo Aiport zote yanatokea ila kwa kwetu rushwa ndio imewekwa mbele.Pale Ethiopia nilikataliwa hata kutoka nje kulipa Hotel kwa hela yangu kwa kuwa walifikiri nitakimbia,na nilikutana na watu wengi tu na mmoja aliniambia hapa hata watu wanaonda kuhiji wanakataliwa.Kizuri ni kuwa sikuombwa chochote kama nilipofika Tanzania.Nilichoambiwa pale ni kuwa wanipeleke kwa Balozi wa kigiriki siku ya pili na kweli nilifatwa na Minibus pale lakini tulipopiga sim tukaambiwa kuwa hakuna kazi balozi amerudi Greece.hadi jumanne,na nilishindwa kulala kwenye makochi kwa siku zaidi ndio niliomba kurudishwa Tanzania.Kwa kweli misuko suko katika safari ni mingi tu na cha kufanya ni tuamke Tanzania na tufuate sheria.Mdau (UMANGANI)
Wadau napenda nitoe hii nakala ya barua kuthibitisha hayo niliyoandika hapo juu.Dear Ayda
ReplyDeleteWarmest Greetings!!!!!
As you can see from the below e-mail, passenger traveled ZNZ/ADD/PAR on the 19th of March on board ET704. Passenger commented that due to document related problems (As pax put it “question on the genuineness of the document”) he was denied to board ADD/PAR flight. He was forced to sleep at the airport couch despite his request for hotel at his own expense. Please refer the e-mail for detailed description of the case.
Please get me all the information you have as to why he was denied to board and accommodation offered to him. Moreover why is he denied hotel at his own expense.
Thank you
Gabrel
nashkuru kwa kuwa nilipatiwa nusu hasara yangu baada ya kwenda nao mchaka mchaka hao Ethiopian Airlines nilipofika Greece,nilisikitishwa nililpokua pale BOLE AIRPORT kuona sisi watu weusi ndio Passport zetu zimekusanywa na tukaambiwa kuwa tutapatiwa tukifika Paris,kitendo ambacho nilikipinga kwa kuwa Passport ya Tanzania imeandikwa hairuhusiwi kuchukuliwa na mtu yoyote asiehusika,na ndio hapo matatizo yalipozidi na kukataliwa kabisa,lakini waliokubali kupewa passport mbele ya safari waliruhusiwa.Kwa hiyo hayo mambo ni ya Ukweli kabisa yanatokea kila sehemu sio Tanzania tu.
Cha kufanya wasiliana na Afande Mkuu wa Polisi (IGP) umpe stori yako. Bahati mbaya sina namba yake ya simu ya kiganja lakini ukiitafuta utaipata. Kama stori yako ina ukweli kutakuwa na kumbukumbu za ulivyowekwa ndani hizo siku unazosema ulilala ndani na hiyo ndege unayosema uliikosa. Atawachukulia hatua za kinidhamu wabaya wako kama walifanya mambo kinyume na utaratibu. Sijui kama utapata hela zako lakini walau utaweza kutoa onyo kwa wabaya wako na watu wenye tabia kama hizo.
ReplyDeleteNdugu wapendwa,sasa njo nafika wakati yakuona nani lafiki juu nipo kwenye shida,arakini nashkuru nimepatiwa kusolve,na nimeanza kushuhulikia kwa wahusika na sipendi kuweka majina ya hawa watu hapa ila nakusudia kuweka IMAIL ya mkuu wa usalama wa Airport hapa kuthibitisha hii claim,nimetoa hapa majina yao kwa kuwa sitaki niharibu uchunguzi,From: xxxx_inv@hotmail.com
ReplyDeleteTo: xxxxx@yahoo.com
Subject: COMPLAINTS ABOUT YOUR TREATMENT
Date: Thu, 29 Oct 2009 14:22:42 +0300
GOOD DAY,
LET ME INFORM YOU THAT I HAVE INTRODUCED TO
YOU BY MR xxxxxxxxx OF JNIA.
I READ YOUR COMPLAINTS REGARDING YOUR MONEY
WHICH WAS TAKEN AS BRIBE BY SOME OF THE STAFFS
OF KIA.
I ALSO FOUND YOUR POINT THAT THERE ARE STAFFS AT
JULIUS NYERERE INTL AIRPORT WHICH YOU MENTIONED
AS DAR ES SALAAM AIRPORT WITH THE NAMES BEGINING
WITH G AND S WHO AS WELL INVOLVE THEMSELVES IN
CORRUPTION.
PLEASE IF YOU DONT MIND KINDLY SEND ME FULL NAMES
OF JNIA STAFFS WHO HAVE THAT HABIT OF CORRUPTION
SO THAT WE CAN CONDUCT INVESTIGATION AND TAKE
ACTION.
I FEEL SORRY FOR WHAT HAS HAPPENED TO YOU.
WITH REGARDS,
xxxxx xxx
HEAD OF SECURITY OPERATION -JNIA
nashkuru sana tena sana kwa ushauri na kazi inashuhulikiwa
Mdau Taratibu umeongelea kisheria na nakubaliana nawewe,lakin kwa watu wa FALSAFA na Pia FASIHI(LITERATURE) inakua ni tofauti na hukumu yako,kwa kuzingatia kuwa Mtoa hoja alikua anaongelea upande mmoja wa matatizo na haikuwa na haja ya yeye kueleza nini tena alikifanya kwa upande wa Ndugu zake,nia yake ni kumurika sehemu ya matatizo na ndio maana waswahili wanasema USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA,NA KIRAKA HAKIWEKWI KWENYE NGUO KONGWE,Na BIBLE inasema"hakuna mtu anaewasha taa akaiweka chini bali huweka juu ili waingiao wapate kuona nuru yake"kwa maana hiyo ilikua haina haja kutueleza tena ndugu zake walimsaidia nini,pili ukizingatia kuwa alikua chini ya mikono ya Polisi kama alivosema na pili kua hamjui mtu na document yake ilikua mikononi mwa hao watu,Pale Moshi pengine wamempeleka Meli sita huko au Pasua,atafanya vipi mawasiliano?especial katika situation kama hiyounafikiria umeshapoteza Ticket yako na uko ugenini,na hayo yanatokea sana kila sehemu na ndio maana likitokea tatizo tunalaumu kwa nini usipige polisi,au kwa nini usiende hospitali,na hii ni kutokana na hali ya kuchanganyikiwa na ndio maana tunaambiwa watu kama hawa you have to reassure them constantly,na sio kuwalaumu,kuna wageni wengi sana wanarukia Tanzania na wanaopata tabu zaidi ni waafrika wenzetu.Pole mdau utapatiwa msaada tu
ReplyDeletePole mkubwa, ila makosa umeyafanya mwenyewe bahada ya kwenda dar ubalozini ukaenda Rwanda, na ndugu zako walikuwa Arusha hiyo story mbona hiko na magumashi mengi. Sema ukweli kilichokusibu kuwa mkweli bwanaaaa'''
ReplyDeleteMdau,, Malaysia
Nyie mnaomsema huyu mtu hajui kabisa...ni heri mngekaa kimya tu. Wala hajawaomba hela yeyte. Mimi nawafahamu warwanda watatu wamekua kama ndugu zangu sasa hivi. Kwa vile wanaaishi kama wakimbizi huku basi hawawezi kwenda nchi yao kabisa. Wameshakwenda TZ mara tatu na wakashukia nyumbani kwetu na ndugu zao wakatoka Rwanda kwenda kuwasalimia.
ReplyDeleteHuyo anaroho ngumu na ya ujasiri sana ya kuvuka mipaka ya panya na kuingia nchini kwao kuona kusalimia ndugu zao.
Na hapo KIA wanajua haya yote ndio maana wanatafuta sababu ya kuwasumbua na kutaka kitu kidogo.
SINA USHAURI, UKIMFATA JK ATAKWAMBIA NENDA MAHAKAMANI WAKATI MAHAKAMANI KWENYEWE YALEYALE.
ReplyDeleteKwa kweli IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA imejaa walarushwa kibao. Mimi mwenyewe nina visa vitatu ambavyo nilisolve kwa kutoa rushwa kuwasaidia jamaa zangu wageni waishio hapa bongo. Na mara ya nne nikasema nikomae kwa kweli chamoto nilikiona.Maana hata baadhi ya wakubwa pia wanashiriki kimtindo kula rushwa. Mwishowe jamaa zangu walilazwa ndani na kesho yake wakaondoka baada ya kulipia malipo halali ambayo hao jamaa wa Uhamiaji walikuwa wanayatamani watie mfukoni.
ReplyDeleteKWA KWELI IDARA YA UHAMIAJI INABIDI IMULIKWE. PCB MKO WAPI? AU NA NYIYI NDIO WALE WALE? RICHMOND STYLE.
K.O.R.
Ndugu zangu tujitahidi kujenga Nchi zetu ili tusipatwe na matatizo kama haya
ReplyDeleteHivi nyinyi wakimbizi wakinyarwanda mko je?Mbona sisi wakimbizi wakongo tunaishi huku ulaya lakini hatuwezi kuthubutu eti tunaenda afrika?kwanini mkae na kihelehele cha nchi zenu mboooovu zilizojaa wauwaji tu? yani watu bwana!! hawaliziki kwelikweli,,sasa hapo ulipo watanzania wakikutalia kupanda ndege urudi!uataenda wapi? Watanzania mimi nawafahamu saaana washenzi mno,,wanaweza akakukatalia kupandia ndege kwao ,,hio ni nchi utadhani haina viongozi ni kama kongo kipindi cha mobutu.Siwezi kumaliza bila kukurushia ushauli kidogo fanya chapchap utafute utaratibu wa kurudi huku ulaya usubili kupewa ulaiya wa Greece,,usiwe unatembea na pasport za kibandia ambazo haujulikani vizuli na hukubaliwi kutembelea nchi uliyotokea.Wengine hapa tumesota na upweke na ndugu tunao kibao huko afrika lakini bila ulaiya wa Norway sivuki mpaka.
ReplyDeletemimi sikuelewi kabisa huwezi kusafili toka ulaya ukiwa na dolla hazifiki hata 3000au 2000 mfukoni ,,umejiweka ndani yamatatizo tangu unatoka huko,,na bado ukiludi tena huluki bila kutoa hela nyingine,,wewe kaa rwanda tuu,,umependa kukaa huko.tanzania ni nchi ya weeeeeezi tu.
ReplyDeleteDo you need a ‘work permit’ to pray in church?
ReplyDeleteDear Editor,
As a recent visitor to Arusha, I enjoyed reading your newspaper. Although I believe that you deal with particularly northern Tanzanian issues, I wanted to mention something to your readers that might be of interest. If this were an isolated incident, I would not take the time to address it, but I have since found out that it is apparently an on-going and persistent problem.
I enjoyed the hospitality of Tanzania very much. I would recommend your country to friends ands strangers alike with one exception: The town of Morogoro. Wanting to see the beautiful Uluguru Mountains and the Mikumi Game Park, I traveled with friends to this city. We stayed at the picturesque “Kola Hill”. On awaking on the very first morning, we were met by Immigration officers demanding to see our passports and wanting to know our plans.
We openly told them and stated that we had already been invited to a local church to see their service. We were then told we were not allowed to pray if asked or engage in any kind of “work” in the area. If we did, we would require a “work permit” at a substantial cost to each one of us. This also included if we wanted to visit any area schools, help out with a local family or etc. At first we passed it off as nothing.
However, after spending several days in this area and meeting other tourists and local ex pats, we were told the same story again and again. Tourists being hassled, treated rudely, and basically told to “push on” by the Immigration of this town. We never experienced anything else like this at our stay in your country. However, I believe that you should warn people that Morogoro is an UNWELCOME place. My question also is “Do you really need such a thing as a “work permit” to pray in local place of worship?”
If the above is indeed not true, then your government should remove these men from their positions in local government. I would hate other visitors to leave Tanzania with a bad taste in their mouths because of one local government.
Disgusted Tourist
hii ni kwa mujibu wa ARUSHA TIME kwa wale wanosema huyu jamaa katunga hiyo story na hii ni ya kutungwa hii nchi bana watu wengine wako kwenye nafasi za kazi lakini wanafanya ufisadi tu sasa anagalia vilea wanachafua nchi yetu. juzi tu nimekutana na wazungu wanalalamika kwamba kwenye nchi nyingine za afrika ya mashariki wanakuomba uende ukawekeze lakini tanzania ukitaka kuwekeza wankuuliza watapataje 10% kutoka kwenye huo uwekezaji ushenzi mtupu wanaruidisha maendelo nyuma
TAFUTA MBINU ZINGINE URUDI ULAYA KWANI ULIKOSEA KUPITA NCHI AMBAYO SHETANI NDIYO AMEWEKA MAKAO MAKUU YAKE PALE.
ReplyDeleteMDAU MONEY UK.