KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, BAN KI MOON, AKITETA JAMBO NA BALOZI WA TANZANI AKATIKA UMOJA WA MATAIFA, DKT AUGUSTINE MAHIGA, MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA KWA MJADALA KUHUSU UMUHIMU WA MAGEUZI YA VIWANDA KWA MAENDELEO YA AFRIKA. BAN KI MOON ALITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA MJADALA HUO AMBAO USIMAMIZI WAKE ( MODERATOR) ALIKUWA NI BALOZI WA TANZANIA.
BALOZI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WAMATAIFA, AUGUSTINE MAHIGA, AKIONGOZA MADADILIANO KUHUSU UMUHIMU WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA AFRIKA, MJADALA HUO ULIFANYIKA KAMA SEHEMU YA MAADHIMISYO YA SIKU YA KIMATAIFA YA VIWANDA KWA AFRIKA AMBAYO HUADHIMISHWA NOVEMBA 20. KUSHOTO KWAKE NI KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, BAN KI MOON NA KULIA NI RAIS WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA, DKT. ALI ABDUSSALAM TREKI


BAN KI MOON ASISITIZA MAGEUZI YA VIWANDA AFRIKA
NA MWANDISHI MAALUMU
NEW YORK
Ikiwa ni miaka 20 sasa tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio la kuifanya Novemba 20 kuwa siku ya Kimataifa ya Viwanda Afrika, ukuaji wa sekta hiyo ni wa asilimia moja ikilinganishwa na mabara mengine.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akifungua mjadala kuhusu suala zima la umuhimu wa viwanda kwa maendeleo ya Bara la Afrika.

Mjadala huo ambao ulikuwa chini ya usimamizi ( moderator) wa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Augustine Mhiga uliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda ( UNIDO). Kama sehemu ya maadhimisho ya siku hiyo.

Akawaeleza wajumbe wa mjadala huo ambao mada yake ilikuwa, “ mikakati na sera za viwanda, ufumbuzi wa mabadiliko ya uchimi kwa afrika. Kwamba, mwaka uliopitia ( 2008) ulikuwa mwaka wa tano mfululizo ambapo Afrika ilishuhudia ukuaji mzuri wa uchumi wake kwa kiwango cha asilimia tano.
Hata hivyo anasema Katibu Mkuu.
Licha ya ukuaji huu mzuri ambao umesukumwa zaidi na uzalishaji wa bidhaa, kilimo na utali, bado ukuaji wa sekta ya viwanda si mzuri na haukuleta matokeo yaliyotarajiwa.

“ Takwimu zinaonyesha mwenendo wa ukuaji wa viwanda katika Afrika ni wa asilimia moja ya ukuaji wa viwanda duniani kote, ni wazi kwamba kwa mwenendo huu, maendeleo ya viwanda Afrika bado ni wa kusuasua sana ikilinganishwa na nchi zinazoendelea”, akasema Ban Ki Moon.

Na kwa sababu hiyo, Ban Ki Moon anatoa changamoko kwa viongozi wa Afrika na wataalamu mbalimbali kutafuta mbinu zaidi pamoja na kuwa na majadiliano ya kina ya namna ya kusukuma mbele ukujai wa viwanda, ambao amesema ni muhimu sana kwa maendeleo ya bara hilo na watu wake.

Akabainisha kwamba utandawazi na ukuaji wa haraka wa teknolojia, kunatoa changamato kwa Afrika kujiangalia upya katika suala zima la maendeleo ya viwanda na matumizi ya teknolojia za kisasa.

“ Kuna makubaliano ya jumla kwamba tunahitaji mikakati na sera madhubuti ili kusukuma mbele maendeleo ya viwanda katika Afrika. Lakini kuna maoni na mitizamo tofauti kuhusu ni mikakati ipi na sera zipi ambazo ni sahihi katika kusukuma maendeleo ya viwanda Afrika “akasema, na kuongeza “Tunahitaji majadiliano zaidi kuhusu namba bora ya kuleta mageuzi ya viwanda Afrika na kuamua nini tunachoweza kujifunza kutoka wa wenzetu wengine ambao wamefanikiwa kuleta mabadiliko hayo maendeleo ya na mfano ukiwa ni kule ninakotoka mimi, Bara la Asia, akasisitiza Ban Ki Moon ambaye asili yake ni Korea ya Kusini.
Katibu Mkuu huo anasisitiza pia, haja ya a viongozi wa Afrika kujitazama na kujifunza kwa nini Afrika imeshindwa kuweka kipaumbele katika maendeleo ya viwanda.

“ Majadiliano haya ya leo ni uwanja mzuri wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu ajenda hii muhimu sana kwa maendeleo ya Afrika. Nimatumaini yangu pia kwamba majadiliano haya yataanzisha mchakato wa uhakiki na uchambuzi wa kina ndani ya Umoja wa Mataifa na ndani ya nchi za Afrika kuhusu umuhimu wa maendeleo ya viwanda.

Naye msimamizi wa mjadala huo , Balozi Augustine Mahiga allisema mjadala huo licha ya kutathimini umuhimu wa viwanda kwa maendeleo ya afrika, lakini pia ulikuwa ukitoa fursa kwa washiriki kuelewa ni kwa nini Baraza Kuu la Umoja wa mataia miaka 20 iliyopita, iliamua kupitisha uamuzi wa busara wa kutenga siku maalum ya kutoa msukumo kwa maendeleo ya viwanda Afrika.
Akasema “ mjadala huo ulikuwa ukifanyika katika kipindi ambacho Dunia ilikuwa ikiibuka kutoka katika moja ya mtikisiko mkubwa wa kuyumba kwa uchumi. Huku Afrika ikikabiliwa na changamoto kadhaa.

Akawaeleza washiriki wa majadiliano hayo akiwamo Rais wa Baraza Kuu la 64 la Umoja wa Mataifa, Dkt. Ali Abdussalam Treki, mabalozi, wataalamu wa masuala ya uchumi na wataalamu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, (UNID). Kwaba Afrika inatakiwa kuzitumia changamoto hizo kuleta mageuzi ya viwanda pamoja na kutumia teknolojia za kisasa sahihi na zinazolinda mazingira.

Mwaka 1989 kupitia Azimio namba 44/237, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika mkutano wake wa 44 kwa kauli moja lilipitisha Azimo hilo la kuifanya Novemba 20 kuwa siku ya kimataifa kwa lengo la kuhamasisha Jumuia ya Kimataifa na Afrika kutilia mkazo mageuzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mageuzi ya viwanda huku mwananchi wa kawaida anatumia jembe la mkono! Hizo Mali ghafi zitatoka wapi! As far as I know huweza kufikiria kutengeneza gari wakati hata kisindika nyaya tu imekushida!

    ReplyDelete
  2. Jamani najua tunapenda kuandika kwa lugha yetu lakini hili neno la " Mageuzi ya viwanda" kwangu mimi its not reachable.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...