Ule ufunguzi (premire) wa Movie ya Baby Powder utakao fanyika katika jiji la Atlanta hapo Novemba 14 ndio huo unazidi kunukia. Juzi kamera ya Mdau iliwanasa Ma Celebrities wakubwa hapa Marekani wakitoa shouts zao Kwa Babby powder katika Soul Train award iliyofanyika hapa ATL.

Watanzania, Wakenya na Wanaafrika Mashariki kadhaa kutoka majimbo mbali mbali ya United States wameanza kumiminika jijini. Habari za kutoka kwa waratibu sinasema tickets walizochapisha hawali zinakaribia kumalizika kwa hiyo wapo mbioni kuchapisha zingine kwani idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Onyesho hilo la ufunguzi limepangwa kuonyeshwa katika theater ijulikanayo kama Porter Sanford III Performing Arts & Community Center 3181 Rainbow Dr. Decatur, GA 30045. Onyesho litaanza saa 12:00 jioni (6:00) ambalo litatanguliwa na mapokezi maalum ya Waigizaji na Wageni wote kwa ujumla ujulikano kama RED CARPET!!

Waandishi na Wapiga picha mbali mbali watakuwepo kufanikisha zoezi hilo. Tafadhali "Dress to impress"!!

Baada ya zoezi hilo onyesho litaanza katika theater yenye uwezo wa kuingiza watazamaji 500 per session. Habari kutoka kwa waratibu zinasema kutakuwa na uwezekano wa kuwa na maonyesho mawili lakini hilo bado halijathibitishwa.

Baada ya movie waungwana na wadau wote wataelekea katika Club mpya na ya Kimataifa ya "The Valley"" kuyaruka masneki mpaka asubuhi please usisahau kubeba mswaki!!

Shukrani maalum zinatangulizwa kwa Wanaafrika Mashariki wenzetu kutoka hapa Atlanta, Alabama, North & South Carolina, Tennessee, Frorida, Dc na NYC na miji mingine mingi ambao wameanza kumiminika kwa shughuli hii.


Unashauriwa kuchukua hotel maeneo ya Sandspring kuanzia exit 23 to 31B kwenye Perimiter-285. Kumbuka kufika kwenu ndio ufanikishi wa shughuli hii ya kihistoria. Kwa maswali yoyote kuhusu Baby Powder, tickets na direction tafadhali wasiliana na Wafuatao au pitia @

www.babypowderthemovie.com.
Abdallah Mustafa Dallas 786 402 7173
Lawrence Karabani 770 656 3280
Emmanuel Sajoman 678 517 4371
Carlos Mwaibula 678 497 6695
Hadji Saeedia Helper 678 651 5242
tafadahali burudika na trailer hii
http://www.youtube.com/watch?v=Atj_Nn4m4Ao
Mdau Hadjihelper

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hahah, tusisahau miswaki siyo, vipi kuhusu lip gloss! Tutakuja basi. Mbona watu wote wa kuwapigia ni mameni, mnatutisha wazee wa baby powder, wengine tunakuja kutafuta wake huko!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...