Watu watatu wametiwa mbaroni sasa hivi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kwa kutuhumiwa kuwa miongoni mwa kundi la matapeli linalolaghai watu kwamba wanafanya kazi WFP na wana madawa kwenye maghala makubwa makubwa ya kuhifadhi chakula aina ya Damoline Liquid solution made in Sweden ambayo inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises.
Bahati mbaya ama nzuri matapeli hao walikutana na mdada mmoja (jina na anakofanyia kazi kapuni) mtotot wa mjini ambaye walipomvaa tu na kumpa hilo dili, akawazidi kete na sasa wapo kituo cha Polisi Oysterbay ambako wameshaanza kutajana na mmoja baada ya mwingine wameanza kukamatwa.
Inasadikiwa kundi hilo ni la zaidi ya watu wanane, wakiwemo kinadada fulani almaarufu hapa jijini, na lina wazungu kadhaa ambao nao wanasakwa.
Stori kama hii ilirushwa humu katika Globu ya Jamii hivi karibuni nawe unaweza kuisoma yote na kujihadhari na mapema. Habari zaidi zitakujia kila zitapopatikan. Kwa sasa soma hiyo stori iliyopia ambapo mdau alilizwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Asante kwa taarifa. Yule mdau aliyetusimulia humu hakulizwa bali siku hiyo hakupata faida katika biashara ambayo amejizoeza nazo.

    Ukitafuta jinamizi utalipata!

    ReplyDelete
  2. Mungu mkubwa afadhari wamekamatwa tupate majina yao. Maana wapo wengi sana watu wa namna hii jamani

    ReplyDelete
  3. saafi sana kina galeba na yule jamaa alotuletea story na wengine woote muende mkachukue mshiko wenu kwa hao matapeli na mtoe ushahidi wa nguvu ili wakajifubnze adabu segerea

    ReplyDelete
  4. tunaomba sana hao wazungu koko watafutwe hadi wapatikane na wapewe masaa 24 ya kurudi kwao ni hayo tu nyambafff sie viza za kuja kwao wanatuchoshaaa na maswali yao marefu kama treni ya mizigo mnaenda kufanya nini sasa mizungu hii inaingia kwetu kiulainiii yani ikikamatwa hadi embassy zote zijue cnn bbc magazeti yote ili na wao waaibike waone upuuzi wao shwain sana

    ReplyDelete
  5. mie kuna mtu walimtapeli wakamtajia jina linalofanana na langu, yeye akadhani mie nimeshiriki kumtapeli, tukapelekana hadi Oysterbay Police lakini kama ujuavyo Polisi wetu ukweli wanaujua hawakutoa ushirikiano unaotakiwa. watu hao wanatakiwa waonyeshwe kwenye magazeti au televisheni ili tuwaone na kuwafahamu.

    ReplyDelete
  6. KAKA MICHU MIMI SIAMINI KAMA HAWA JAMAA WAMEKAMATWA ILA KAMA NI KWELI FANYA MIPANGO TUMJUE ASKARI MWENYE HIYO KESI AU RB NAMBA ILI NA MIMI NIKAMTAMBUE MAANA NA MIMI NIMESHAWAHI KUPIGWA KWA STAILI HIYO NA CHUPA NINAZO KIZIBITI NINACHO

    ReplyDelete
  7. Kaka michuzi ahsante kwa kazi nzuri ya kujenga jamii iliyo na uelewa kwa kutuwekea matukio.
    Nampongeza sana huyo dada kwa kazi nzuri aliyo ifanya,ila ningefurahi kama wote waliopatwa na mkasa huo wangeenda kituoni hapo ili kuwatambua hao majizi na matapeli ili kuweze kuwa na ushahidi wa kutosha, bila shaka wote waliopatwa na mkasa huo kama bro Alex wataenda ili kupigilia msumari

    thanks
    Mdau

    ReplyDelete
  8. KAMA KWELI WAMEKATWA BASI WATAKUWA NI MATAPELI WAJINGA KABISA. KWANI WATU WAJANJA WANGEJUA TU HILI DILI NI PUBLIC INFORMATION SASA NA RISK YAKE NI KUBWA.

    WAPEWE ADHABU YA KUTOSHA NA KIBANO CHA NGUVU. WATU WAHATAKI KUFANYA KAZI HALALI WANAENDEKEZA WEZI TU.

    KUDADEKI

    ReplyDelete
  9. shenzi, safi sana. Nyau wakubwa hao! Waende segerea wakaolewe tu.

    ReplyDelete
  10. Washenzi sana hawa,hata mie pia walinipigia simu,kwa bahati mbaya niliwahoji sana maswali ya kuzushi,hivyo nilipotaka kusuka tego wakawa wameshtuka.

    ReplyDelete
  11. Mimi ndugu zangu SIWAELEWI kabisa......How comes ukubali kuzungumza na "PERFECT STRANGER"....na ukajilengesha mpaka akakuvua chupi na kukutoa pesa!!!.......bwana tukaneni mmalize hayo matusi yenu....lakini mambo ya kutapeliwa kwa staili ya kijinga tena mchana kweuupe huwa mnayatakwa wenyewe!....anyway POLENI lakini

    ReplyDelete
  12. Mimi walinipigia simu na bahati nzuri niliweza kurekodi baadhi ya mazungumzo na sauti yao ikiwa clear kabisa.

    ReplyDelete
  13. SAFI SANA NASEMA TENA NYAU HAO. MIE NAFAHAMU BAAZI YA HAWA NA NI WAHAYA WENGI KWENYE CHENI HII. NILIWAKILISHA MAONI YANGU LAKINI KAMA KAWAIDA HUYU MICHUZI HAKUYAPOSTI, NAUHAKIKA HATA WADAU WENGINEO WALIANDIKA MAONI, KWAMANA WASHKAJI ZANGU WAWILI PIA WAMEKIRI JAMBO HILI, CHA KUSHANGAZA NI KWAMBA MICHUZI ALITOA ILANI MTU AKIANDIKA MAONI YA KUTUKANA NA KUDHALILISHA WATU HUMU, HATOYATOWA. ILA WATU PIA WAKIINGIA HUMU KUTOA UKWELI WA MAMBO WAJUAYO AMBAYO NI MANUFAA KWANI YATAFUNGUA WATU MACHO. HUYU MICHUZI HAYAPOSTI, ANAYAMINYA. SASA MAANA YAKE NINI? KWA TAARIFA YAKO IMEBIDI TUWATONYE POLISI OYSTEBAY WAMEFATILIA NAAMINI BAAZI YAO NDO WASHAKAMATWA KINONDONI, NA WENGINEO BADO SINZA. AMBAO HUU MTANDAO UNGESAIDIA KWAMANA TULIWATAJA KWA MAJINA HAPA. LAKINI MICHUZI HAKUTOWA MAONI YETU. HAYA BWANA ENDELEA NA KAZI. SIJUI UNAMAANA GANI KWAKWELI TUNASHINDWA KUELEWA UNAENDESHA AJE HII BLOG YAKO.

    ReplyDelete
  14. Huyo wanayesema "mzungu" ni mswahili kabisa ila stage name yake ya kufacilitate dili hiyo huwa anajifanya yeye ndiye "mzungu" wa UNHCR.

    Lakini pia inawezekana wamo wazungu wa kweli...........

    ReplyDelete
  15. Poe sana Anon wa Nov 26,11:01;00.
    Hii siyo sehemu ya kutajia majina ya matapeli au mafisadi. Sehemu nzuri ni pale "Temeke Mwembeyanga" kama walivyofanya akina Dr Slaa wa Chadema.

    ReplyDelete
  16. Hawa jamaa baadhi yao walikamatwa siku ya Jumapili walikua wanaelekea kumliza jamaa yangu ila kwa bahati nzuri akawawahi pia kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama na wezi hawa walikamatwa pale maeneo ya Magomeni hospitali...mtandao wa uporaji wa mali kwa njia ya akili utamalizwa ikiwa watu wataacha tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka

    ReplyDelete
  17. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  18. COMMENTS ZA 27,03:31:00 kuwa zimeondolewa na blog administrator. kama wanavyodai wadau, INAONEKANA YALIWAHUSU SWAIBA WA MMILIKI WA BLOG HII AMBAYE NI MICHUZI. NDO MAANA YAMEONDOLEWA.
    HAINA MAANA BASI KAMA KUNA UBAGUZI NA HAKUNA UHURU, WA KUTOA MAONI ESPECIALLY WATU WAKIZOZA UKWELI NA SI MATUSI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...