Busta Rhymes akiwa na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga baada ya kufanya onesho la nguvu usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Posta Jijini Dar ambapo Busta alifanikiwa kuziteka nyoyo za mashabiki kwa kiwango cha juu huku akisifu Tanzania na watu wake akisema ni watu wazuri wakarimu na akasema anafurhishwa sana na umati wa mashabiki uliokuwa umejitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta One Love 2009.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga alisema anamshukuru sana Busta Rhymes kwa kuwa na moyo wa huruma kwani onyesho hilo lilikuwa lifanyike Novemba 7 likaahirishwa kutokana na msiba wa baba yake Joseph, Mzee Kusaga. Busta alikubali kuja kufanya onyesho Novemba 21 pamoja na kazi zake nyingi akamshukuru sana na akasema onyesho hilo analitoa kama Dedication kwa Marehemu baba yake.

Buster Rhymes kulia akiwa na Spliff Star mkali mwingine aliyeongozana naye.

picha kwa hisani ya
Full Shangwe


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kilichonifurahisha ni namna Busta, dj na audience walivyokua wakiwasiliana,ni somo zuri sana kwa wasanii wetu. Ila waandaaji hawakuwatendea haki kina Fid Q, Mangwea,Madee, na ProfJ walipowaweka kuimba baada ya Busta Rhymes daah ilikua mtihani mgumu sana kwao,maana jamaa alishamaliza kila kitu hivyo wadau wengi walianza kurejea makwao muda ule.
    Japo Serengeti walifunika jana(yaani 500ml kwa buku ie $0.74 hivi) ila ushauri wa bure kwenu ndugu zangu jana ni kweli tulifurahia ile kitu yenu na leo tumeamka vichwani safi kabisa utadhani jana yake hakukua na ugeni kichwani(samahani wasiotumia),ila zile chupa zenu zilivyokua zikizagaa uwanjani katika umati kama ule,tunashukuru Mungu anaupendo sana na sisi maana kama ingetokea vurugu pale,sijui nandani wajirekebishe kwa hilo maana walisema ulinzi upo wa kutosha lakini ilikua ni wakati wa kuingia na ulinzi wa jukwaani tu,kwani kule kusukumana kwa watu pindi mtu mzima alipopanda jukwaani walinzi walishindwa kutuliza,na bali ile motto ya tamasha lenyewe ONE LOVE ndiyo ilinusuru!
    Yoyt kwa yote ile mishikaki na chachandu ya M.... daah,jamaa mbaya Mox hakukosea kumwimba!

    ReplyDelete
  2. Dah! bila Joseph kupanda jukwaani mwishoni na ku elezea msiba na watu kuguswa na hilo na uhakika watu wangemzomea Busta , maana alibore kichizi , nashangaa nasema aeti atarusi sijui nani aatalipa hela ya kumuona tena , labda atoe vitu vya ukweli , show ili bore kinoma, big up to TZ artis ,walifanya kweli, haswa Chiddy .

    ReplyDelete
  3. afu huku ulaya watu wala hawamzunguzii tena huyu basta... kashapitwa na wakati, Joseph tuletee watu wa maana Alicia Keys, Beyonce, etc ambao wako kwenye chat huyu kashapitwa na wakati NEXT...........

    Afu we kamichu mbona hauko kwenye picha? manake tukuone na wewe unavyoendelea nawe kutwa kucheka tu, hivi unakasirikaga kweli?

    ReplyDelete
  4. Kweli huyu bwana ni old school! sasa ni enzi ya akina TPain, Lil Wayne, Chris Brown, Bird man, R. Ross and etc etc!

    ReplyDelete
  5. Birdman na Cash Money si wametoka around the same time na Busta? Wabongo mna hela ya kuwaleta kina Eminem na Chris Brown nyie? Labda waje kwa charity tu, hata hawa wenyewe mnaoita old school kina Ja Rule sidhani kama wanalipwa, zaidi ya nauli. Ni wazo zuri kuleta watu wenye catalog kubwa, nyimbo umekuwa unazisikia miaka mingi, ukiletewa Drake, hata Lil Wayne nadhani ni hardcore hip hop fans tu ndiyo watakaokwenda, ni mtazamo wangu. By the way, ukumbi wa kisasa wa maonyesho unajengwa lini, haya mambo ya kucheza muziki kwenye vumbi huku ukimuangalia mwanamuziki kama yuko mbinguni yamepitwa na wakati.

    ReplyDelete
  6. sio flip Star..anaitwa Spliff Star

    ReplyDelete
  7. Clouds mpo JUU JUU JUU....yoyote anayesema busta sijui kachoka, sijui ldo skul...to hell. It was really great to see him perform live on stage in Dar. That was an experience mayne..i dont care if he ain got no hits hittin the airwaves right now...all i know is I HAD FUUUUUUUUUUUN!

    ReplyDelete
  8. ....Wabeba maboksi ndio mnaongoza kuwa critics wa tour hii ya Buster mtu ambaye pengine wala hamjawahi kumuona tangu mmefika huko. Kama wasanii maarufu mbona kina Jigga, Beyonce, Ja Rule, 50Cent wameshatimba maguu huku Bongo..
    Hiyo ndivyo ilivyo hata mfano ukiwa Nai.., Buja.., au Kigali na Kampala wasanii wanaotamba kutoka Bongo na wanaofanya tour utakuta kina sister P, Bwana Misosi na wenyewe wanaEnjoy tena sana tu. Cha muhimu ni ili Show na sio yuko katika chati ipi, na pia ujue sio kila msanii kutoka America anaweza kupata watu wengi akija hata iwe bure.. Mlete huyo Lady Gaga anayetamba sasa uone kama wataenda watu 100.
    ..

    ReplyDelete
  9. Huyu jamaa wa Mon Nov 23, 01:08:00 AM dah! ulitaka aje nani tena maana kwenye list ya hit albums Back on my B.S ni mojawapo na ilikamata namba 5 kwenye billboard top200 soma hapaupate zaidi kuhusu hii album. Big up Clouds FM kwa kutuletea real MC, yaani kuanzia enzi ya old school ya Coming of Age album hadi sasa Back to My B.S album bado yupo juu, legend of the hiphop. Wasiokubali ni wapenda taarabu na si wanaHIPHOP!, kwani hata ukiwauliza hao wasanii uliowataja watakucheka!

    ReplyDelete
  10. Nani amlete Beyonce, mnahela ya kumlipa. wa-marikani wakisha choka ndo wanataka kuja bongo. anyway.. acheni waje tuu japo tuwaone live

    ReplyDelete
  11. Kwendeni zenu clouds hawaku target wapenda old school , walitarget hawa wapenda bongo flava ambao wengi ni vijana na kiukweli walibahili hela kumleta Busta aliye pitwa na wakati.
    Kwenye show nilikua mzee peke yangu wengine wote ni ma dogoz, ambao walikuja kwenye show sababu hawana option yeyote, zaidi ya kumcheki huyu rapper mwenye umri kama baba yao .
    Watu walikua wame boreka na kuchoshwa na Busta kiasi yeye mwenyewe Busta aligundua hilo na kuuliza kila saa je Mmechoka?
    Busta hakua chaguo sahihi kwa ile Audience iliyo kuwepo , bora ume mwaka walimleta Ja-Rule .
    Na tusidanganyane eti jay-Z kaletwa na Cluods jamani , kama Busta alivyo semama na kutangaza hivyo
    This time na wapongeza sana clouds kwa kuweza kua ndaa show nzuri kwa hawa opening acts, kwakweli na dhani wali invest hela nzuri kwenye performance na na dhani kiwango kina zidi kukua ila kwa taratibu bado kuna mambo mengi ina bidi yazingatiwe ila so far show kidogo ili panda quality kwani suala la Busta ilikua ni mchemsho wake mwenywe na pia ilikua ni wrong audiance.

    ReplyDelete
  12. Watu mtaponda na kudis lakini ile nyomi iliyokupo pale posta ni nomaaaaa yaani haijalishi amepitwa na wakati au vipi? na pia wabeba box wanakandia kila kitu kwa vile hawapendi huko bongo tunavyojirusha ila wao hata huyo busta hawajawahi kumuona na pia sio ushamba video zote mpya zinapigwa bongo na idadi kubwa ya wabongo wanadstv wanaangalia miziki yote. Kwa hiyo kutoka ni kawaida yetu sio kwa ajili ya ushamba. Mbona yousou ndour na angelique kidjo walivyokuja hamkusema kitu na wakati pia ni siku nyingi... Tambaeni huko, sisi tulienjoy kinoma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...