Mkurugenzi Mkuu wa PCCB, Dr. Edward Hosea, amemtembelea Spika wa Jamhuri ya muungano Mh. Samuel Sitta Bungeni leo Dodoma. Pichani Spika akimkaribisha Hosea mara baada ya kuwasili ofisi za Bunge. Kulia ni Mheshimwia Nyalandu
Mh Sitta akiongozana na mgeni wake
Mh. Samwel Sitta na Dr. Hosea wakiwa katika mazungumzo ofisini kwa Spika leo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. HAPA HAKUNA CHA KUZUNGUMZA YAISHI.

    DR HOSEA LAZIMA AWAJIBISHWE KWA ISSUE YA RICHMOND NA WABUNGE LAZIMA WAHOJIWE KWA ISSUE YA POSHO MBILI FULL STOP.

    ReplyDelete
  2. Kila mtu anajaribu kumbembeleza mwenzake wasiumbuane.Hii ni kali ya mwaka!!!!

    ReplyDelete
  3. SPIKA SITA ANGALIA SAANA BADO TUNAKUPENDA

    ReplyDelete
  4. Huyu jamaa alikuwa wapi siku zote asitembelee bunge mpaka aone kesho kiama kinakaribia ndo anaanza kujipendekeza kwa mheshimiwa speaker ali apunguze makali ya waheshimiwa wabunge, lakini atagonga mwamba, kwa jinsi ninavyofahamu uadilifu wa speaker lazima tu huyu jamaa apewe kitu tomorrow, haiwezekani mtu ubariki uozo wa rushwa wakati wewe ndiyo kiongozi wa kupambana na rushwa,huku ukijua unacho kifanya tukufumbie macho, zama hizo zimeisha tena ikiwezekana jiulu leo kabisaaaaaaaaaaaa..Tumechoka, Next time tunaomba JK tupigie chini moja kwa moja watu kama hawa hatuwataki, mwenzake wa sheria tayari bado huyu najua issue yake iko kwenye pipe..

    ReplyDelete
  5. Hapa nadhani wataongelea jinsi ya kuanza kudeal na Richmond kwanza alafu ifuatie hii ya wizi wa posho mbili manake mafisadi wako pande zote: wapambanaji na wasio wapambanaji, wizi mbele kwa mbele.

    ReplyDelete
  6. Tehe tehe teheeeeeeeeeee ........................ Vita ni Vita muraaaaaaaaaaaa, .................. Kirimo kwanza ............. Mifuko raki .....

    ReplyDelete
  7. tuyamalize kifamilia

    ReplyDelete
  8. JAMANI MIMI NIMESOMA NA HOSEA CHUO KIKIUU CHA DAR UDSM. NI KIJANA MZURI SANA NA MWADILIFU NA MCHAPA KAZI MZURI. UKWELI HAUSIKI CHOCHOTE NA RICHMOND, ILA HAKUTAKA KUMCHOMA LOWASA. SASA KUFANYA HIVYO SI KWAMBA YEYE ANAHUSIKA NA RICHMOND ILA HAKUTAKA KUMUHARIBIA UWAZIRI MKUU WAKE. SASA HAPA KOSA LAKE LINAKUWA NI KUSHINDWA KUTAMKA KUWA LOWASA ALIKIUKA TARATIBU ZA UAGIZAJI. HUU NI UTAMADUNI TULIOKUWA TUMEJIJENGEA TANGU ENZI ZA MWALIMU WA KUTOWAUMBUA VIONGOZI HADHarani. SASA HIZI NI ZAMA ZA UWAZI NA UKWELI, NDIYO MAANA HOSEA AKAPEWA ADHABU YA KUONYWA NA KUAMBIWA AWE ANASOMA ALAMA ZA NYAKATI, UNAPASWA KUWA MAKINI SIKU ZA USONI. VINGINEVYO SERIKALI INAMJUA NI MCHAPA KAZI MZURI NDIYO MAANA ANAENDELEA KUWA MUKURUGENZI WA TAASISIS HIYO NYETI. ANASTAHILI BENEFIT OF DOUBT. CHAPA KAZI HOSEA, SASA USIMUOGOPE MBUNGE YEYOTE WALA WAZIRI.

    ReplyDelete
  9. aisee Lazaro Nyalandu ndiyo huyo hapo kwenye picha ya kwanza mwenye suti ya brown? du na wewe ni muheshimiwa siku hizi? kweli watu wanatoka mbali.
    kuanzia summer camp program to now member of Parliament
    ulipeleka wengi Marekani.
    hongera sana bwana


    mdau Canada

    ReplyDelete
  10. WABUNGE WETU WASIJARIBU KUTAKA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI, KUPEWA POSHO NA YULE UNAYEMCHUNGUZA SIYO TAKRIMA HIYO NI RUSHWA, TAKRIMA NI PALE UNAMTEMBELEA MTU KWA NIA YA KUMONA NA KUWA NA MAZUNGUMZO NAYE TU BILA KUMCHUNGUZA KIKAZI. HIVI WABUNGE MNATUTAKA HATA SISI TUVUTE KITU KIDOGO TOKA KWA WALE TUNAOWAHUDUMIA NA TUITE TAKRIMA KAMA ALIVYODAI MHE. SPIKA KUWA NI DESTURI YETU WATANZANIA KUWAKARIMU WANAOTUTEMBELEA? HAPANA, ITAKUWA NI RUSHWA KWA LUGHA SAHIHI. DR. HOSEA WAWAJIBISHE WOTE HAO KWA KUPOKEA RUSHWA TOKA KWENYE MAKAMPUNI NA MASHIRIKA HUSIKA. UBUNGE USITUMIWE KAMA KIGEZO CHA KUIBADILISHA RUSHWA KUWA UKARIMU.

    ReplyDelete
  11. nakupa 5 mchangiaji wa kwanza, they both err... Dr Hosea you should be acocuntable for Richmond,

    and all you wabungez should be accountable for double allowances, prepare your cheque books

    ( muosha huoshwa ) tafakari!!!

    ReplyDelete
  12. Mazungumzo yalikuwa hivi:
    Hosea: Ahsante sana mheshimiwa spika kwa makaribisho hapa Bungeni. Nimekuja kuwachunguza wabunge waliopokea posho mara mbili kama vile sheria waliyoitunga na kunipa inavyotaka niwashughulikie.

    Mh Spika: Sawa Hosea lakini unaonaje ukiwaachia kwa sasa halafu wachukue hatua za kurejesha kidogo kidogo? Kama hiyo sheria haipo nitawambia tuitunge mara moja.

    Hosea: Ah ikibidi hivyo mh Spika itakuwa vizuri la sivyo mimi lazima niondoke nao sambamba

    Mh Spika: ah basi mwafaka umeshapatikana, tutakuletea hiyo sheria mpya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...