SWALI: Je unadhani elimu ina nafasi yoyote katika soko la muziki?


DULLY: Ndiyo ni kweli elimu ina nafasi kubwa sana kwenye soko,sio letu tu bali na kimataifa pia,na ndio sababu tunaanza kusema tunaibiwa na hatufiki mbali sababu vilevile hatuna japo upeo wa elimu ya masoko ambayo ni muhimu kiliko elimu yoyote hasa kwa sisi wanamuziki,pia wakati mwingine tunajaribu kufanya mawasiliano na wasanii wenzetu wa nje,ila ukijaribu hata kuomba kufanya nyimbo ya pamoja au kushirikishwa unakuta mnapishana maneno kutokana na wewe kutoitambua lugha husika ya unayetaka kufanya naye kazi,mfano yeye anazungumza kiingereza nawewe hukifahamu.


SWALI: Kama msanii wa bongo flava,unadhani kutoa Album na kutoa single kipi kinalipa zaidi?


DULLY: Kutoa single inalipa zaidi,kushinda Album

SWALI: Kwa nini?

DULLY: Sababu wasanii wamekuwa wengi sana na ndio maana msamabazaji anashindwa kukidhi mahitaji ya kila mmoja, ina muwiya vigumu kuchagua Album ipi ni bora zaidi ya zingine lakini ukitoa single nzuri itakulipa zaidi kupitia show za hapa na pale.
Kupata intavyuu yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...