Na Mwandishi Maalum, Kingston, Jamaica

MAPOKEZI makubwa yamemkaribisha Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili mjini Kingston kuanza ziara rasmi ya siku nne ya Kiserikali katika Kisiwa cha Jamaica.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Norman Manley, Mhe. Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete, amepokewa na Gavana Mkuu wa Jamaica, Mhe. Sir Patrick Allen, ON, GCMG, CD; Waziri Mkuu Mhe. Bruce Golding pamoja na Mkuu wa Majeshi.

Mara baada ya kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake kwenye uwanja wa ndege, Mhe. Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Jamaica Pegasus, ambako kundi la Watanzania wanaoishi Jamaica limempokea Mhe. Rais kwa nyimbo, vifijo na vigelegele.

Wakati wa ziara yake, Mhe. Rais Kikwete amepangiwa kukutana na Mhe. Sir Patrick Allen, leo , Jumanne, Novemba 24, 2009, ofisini kwa Gavana Mkuu huyo kwenye Jumba la King’s House, kabla ya kushiriki shughuli nyingine nyingi ikiwa ni pamoja na kuhudhuria tamasha rasmi la kitamaduni katika Jumba la Sanaa la Little Theatre.

Kesho, Jumatano, Novemba 25, 2009, Mhe. Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Golding kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu. Mhe. Golding wa Chama cha Jamaica Labour Party aliingia madarakani mwaka 2007.

Kabla ya kukutana na Waziri Mkuu, Mhe. Rais Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha Peoples National Party (PNP), Mhe. Portia Simpson Miller, ambaye alipata kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica kwa kipindi kifupi.

Kesho hiyo hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu mwingine wa zamani wa Jamaica, P J. Patterson, ON, OCC, PC, QC ambaye pia anatoka chama cha PNP

Kwenye ziara hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia atahutubia Mkutano wa Pamoja wa Bunge la Jamaica (Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi) na pia atatoa mhadhara maalum kwenye Chuo Kikuu cha Visiwa vya West Indies cha University of West Indies katika kampasi yake kuu ya Mona.

Mhe. Rais Kikwete pia anatarajiwa kupewa Nishani ya Utumishi Uliotukuka ya Order of Excellence ambayo hutolewa kwa heshima maalum na nchi ya Jamaica kwa marais na marais wastaafu.

Mhe. Rais Kikwete vile vile atatembelea Jumba la Makumbusho la mwanamuziki maarufu kuliko wote waliopata kutokea katika Jamaica, marehemu Bob Marley na pia atazindua Kumbukumbu ya Herb McKenly katika shughuli iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Jamaica.

McKenly alikuwa mwanariadha maarufu wa Jamaica ambaye pia alipata kuwa kiongozi wa riadha nchini humo.

Mhe. Rais Kikwete anakuwa Rais wa pili wa Tanzania kufanya ziara rasmi ya kiserikali katika Jamaica. Rais wa kwanza kufanya ziara rasmi ya kiserikali katika Jamaica alikuwa Mwalimu Julius K. Nyerere mwaka 1974.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MJOMBA MBONA UMEONDOKA BILA KUNIAGA, SHULENI MWALIMU ALITUAMBIA KESHO TUPELEKE SHILINGI 500 HELA YA KURUDUFU MTIHANI WA KILA JUMAMOSI SASA ATANICHAPA.

    ReplyDelete
  2. Yaani Wajamaica wakisikia jina la Rais wetu watampenda saaana.
    You can imagine..Jah Kaya!That says everything a Jamaican needs to know.Gwaan JK! show bredren inna Jamdong seh Africa run tingz!

    ReplyDelete
  3. VIPI WATU WETU WA PROTOCOL HAWA KUMPANGIA MZEE KUTEMBELEA KWENYE KABURI LA MWANAMAPINDUZI MARCUS GAVREY MTU MWEUSI WA KWANZA KUWASHITUA WA AFRICA JUU YA KUDAI UHURU?

    ReplyDelete
  4. Aende Cuba kwa Komredi Fidel.

    ReplyDelete
  5. Chakalaka BoomNovember 24, 2009

    Vasco Da Gama........

    ReplyDelete
  6. hahahaha jah kaya lazima wamzawadie kg 10 za kaya

    ReplyDelete
  7. we mdau wa kwanza hapo juu nilikuwa nakunywa maziwa nimecheka hadi nimeitemea computer yangu maziwa kwa kicheko manake nilipaliwa ghafla na kicheko acheni tu huwa nasemaga blog ya jamii ni dawa ya stress full dozi enyi wadau wa huko kingston tumeni picha zenu basi tuwatie machoni
    mdau canada

    ReplyDelete
  8. yaani kweli hii tanzania kila kitu atuwezi leo hii kutemebela kaburi la bob ni muhimu sana wakati wanamuziki wetu nawaandishi wetu wamekufa hata makaburi yake atuyajui watanzania kuna watu wametoa mchango mkubwa sana nani amjui shaban robart aliyekuwa mtunzi mzuri lkn serikali hata kukumbuka mchango wake leo wapi marijan rajab,manet,mbaraka mwinyishee waimbaji wazuri na wamejitaidi sana kutoa mchango wao hata kwa kukuza lugha ya kiswahili lkn maskini leo hii tunamjua sana na rais kumtembelea bob aambaye mi wakati nikiwa mdogo nilisimuliwa kuwa nyerere alimpa bob fimbo km mkono sio kwamba naona alifanya vizuri hapana hila kwanini tusikumbuke wakwetu na hata makaburi yao tukajajua
    yaani inakatisha tamaa nasikitika kwa wanamuziki wetu wanausubiri kumuona rais awasaidie poleni ok mzee na la michael jackson usisahau basi

    ReplyDelete
  9. Rais wetu kweli anaipenda nchi yake. Halali kabisa, na anaendelea kubadilisha ndege kila kukicha akiwatafutia watanzania maisha bora. JK natamani utawale Tanzania milele. Uongozi wako umetukuka. Wewe ni kiongozi bora. Ukitoka Jamaica na Tobego, usisahau pia kupitia huko US, Canada, Ulaya na kwingineko kuiombea Tanzania misaada zaidi. Achana na wanaokuonea gere unaposafiri. Wewe chanja mbuga tuu. Wao walie tuu.

    ReplyDelete
  10. MASKINI WAWILI WATASAIDIANA VIPI????JAMAICA NJAA KALI NA BONGO NJAA KALI...KUMALIZA MAFUTA YA NDEGE TU.
    NAJUA HII UTAIBANA MICHUZI.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...