Huyu ndiye kipa mpya wa timu ya taifa ya bara a.k.a Kilimanjaro Stars Mohamed Mwalami anayechezea klabu ya Ferroviaro ya Maputo, Msumbiji. Anachukua nafasi ya kipa Shaaban Dihile ambaye ametemwa. Kipa mwingine ni Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar. Kwa habari kamili ya kikosi kinachoondoka asubuhi hii kuelekea Kenya kwenye michuano ya Chalenji inayoanza Jumamos

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Afadhali Maximo na TFF wamesikia kilio na shinikizo la wadau na mashabiki wa soka kwa kuwaondoa makipa wabovu. Ali mustapha kaingia mitini kiana kwa kuwa Maximo anamng'áng'ania wakati mwanyewe anajijua hana uwezo. Tuna mshukuru Juma Pondamali nadhani ni kwa ushauri wake wamempata kipa Mwarami Mohamedi (Shilton). Shabani Kado tunamuaminia, hapo sasa anatakiwa aongezeke Juma Kaseja, timu itakuwa bomba.

    ReplyDelete
  2. Afadhali Maximo na TFF wamesikia kilio na shinikizo la wadau na mashabiki wa soka kwa kuwaondoa makipa wabovu. Ali mustapha kaingia mitini kiana kwa kuwa Maximo anamng'áng'ania wakati mwanyewe anajijua hana uwezo. Tuna mshukuru Juma Pondamali nadhani ni kwa ushauri wake wamempata kipa Mwarami Mohamedi (Shilton). Shabani Kado tunamuaminia, hapo sasa anatakiwa aongezeke Juma Kaseja, timu itakuwa bomba.

    ReplyDelete
  3. Hivi huyu maximo (cijui masikio) atatuchezea hivi hadi lini? kama angekuwa ni kocha wa timu ya taifa ya kwao Brazil angebadilisha badilisha wachezaji hivi kweli? Kila ukiamka asubuhi, basi timu mpya imetajwa...unajua ni aibu ukiulizwa leo hii utaje hata wachezaji watano walioko timu yako ya taifa ukashindwa. Kuna ubaya gani katika ile timu ya taifa iliyotoa draw na senegal? kwa nini asingeiacha hadi leo?

    Pia huyu bwana amekuja kufundisha nidhamu au soka hapa bongo? Yaani jamaa akiamka nidhamu...akilala nidhamu....akienda toilet nidhamu. Nadhani kuna haja ya kuupitia tena huu mkataba wake huenda nidhamu ndio cha kwanza then soka nido cha pili. Kama sivyo, basi tumchagulie timu ya taifa then yeye afundishe, hataki basi achape lapa anatuyeyusha!

    Haruma moshi hana nidhamu, kapata timu huyo anaenda zake ulaya....inaboa

    Mheshimiwa mkuu wa nchi, naomba utucikie kilio chetu, tuondolee huyu bwana umuweke hata Kanumba awe kocha wa timu ya taifa, kama kanumba humtaki, tuwekee hata Jumanne Maghembe basi...

    Aaah, ngoja ninyamaze mie, nicije nikatukana nikamkosea kaka michuzi na wala cio maximo!

    k'dume

    ReplyDelete
  4. Anaonekana wa ukweli!

    ReplyDelete
  5. huyo kipa naona atatufaa kwasababu hata miondoko yake ya kudaka daka.

    ReplyDelete
  6. ni bora alivyobadilisha kipa manake yule kipa aliyefungwa magoli 5 sijui alimtoa wapi.taifa stars timu nzuri ila kipa na mabeki awafai.maximo anafanya ajuacho .

    ReplyDelete
  7. Mimi muono wangu ni tofauti kabisa,,,Hivi inakuaje KOCHA wa timu ya TAIFA ya JAMHURI ya MUUNGANO aikochi timu ya UPANDE MMOJA tu(BARA)????,,,kama TFF wangekua na uelewa MPANA,,huyu bwana MAXI angekua anaenda kuangalia timu mbili hizi(BARA na VISIWANI) zinafanya nini,na ikibidi kuzisaidia ushauri tu,then TFF ingechukua kocha yeyote MZAWA ili aikochi BARA,just kuleta taste ya maujuzi mengine angalau kwa muda.Hivi embu chukua hii na ujaribu kuifikiria kwa upana zaidi,,,Iwapo watakutana BARA vs VISIWANI na BARA wakapigwa,picha hili litaisha vipi??,,TFF na wadau wengine tuamke sasa.

    ReplyDelete
  8. Mimi naona bado hatujaliona tatizo.......mpaka tutakapopata timu nyingi za vijana......waalimu wa kisasa.....muundo wa soka ulionyooka......wadhamini wanaona na kuzipa uzito/umuhimu timu zote ( sio Simba na Yanga).........viongozi wenye wivu wa maendeleo ya mpira (sio umaarufu..kujaza matumbo kisha waende kwenye ubunge)....TUNAHITAJI WATU WA SOKA WA KWELI sio wasanii. Bila hivyo sisi tutabakia Arsenal.. Barcelona...Real Madrid etc....Lazima tubadilike haraka....usanii, wizi, husuda, majungu na maneno matupu hayatufikishi popote.....

    ReplyDelete
  9. Nawaunga mkono wadau wote. Tatizo halipo kwa kipa tu ila ni mfumo mzima wa uongozi Wa TFF ubadilishwe. TFF ni baba kama hawawezi kusuliisha watoto wake wamekubali nini kuzaa???

    Tatizo la Maximo na baadhi ya wachezaji wengine ndio kama tunavyojua wadau. TFF kimya kwa sababu kocha ni mbrazili halafu ana rangi za benki. Kama kocha angekua kaka michuzi na mimi na rangi zetu za kitumwa mbona tungekua tunaishia kupaa samaki Feli.

    Mdau hapo juu inaonekana una upeo nimeshayazungumza hayo ya kocha wa jamhuri ya muungano kufundisha timu moja. Kilichatakiwa akae pembeni awaache wasaidizi wake Akina Pondamali wajifunze na ku build konfidensi. Nimeshayaonge huko nyuma nikaambiwa nachafua na sina Uzalendo. Myaone

    Lakini mjuba sichoki kulonga. Nitalonga mpaka kufa kama kunaukweli.

    Kisiju

    ReplyDelete
  10. wachezaji wa bongo bwana! jamaa anacheza na makubazi (sandles! Mwondoko wake nao ni wa kijotijoti!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...