Mama EMILY TIKU GELLEGE.
( 24 /05/ 1948---29 /11/ 1996 )

Jana mama tarehe 29 /11/ 2009 Umetimiza miaka 13 tangu ulipoaitwa na Bwana tarehe 29 /11/ 1996 saa 2 asubuhi.
Mama tunakukumbuka sana Upendo wako,Hekima zako,busara zako na ulikuwa mshauri mzuri sana katika familia.Unakumbukwa sana na mwanao mpendwa na wa pekee Ruth,mkweo Eugene na wajukuu zako Emily na Ervin.
Pia unakumbukwa sana na Dada zako,Kaka zako,wadogo zako,wifi zako,wajukuu zako,shemeji zako,ndugu,jamaa na marafiki.Tulikupenda sana mama MUNGU alikupenda zaidi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Lihimidiwe. Amen!!!.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Rest in Peace!!
    The picture looks very familiar..is this Ruth Magessa's mom? wellEternal rest Grant to her oh Lord! Poleni wanandugu!

    ReplyDelete
  2. Dada angu mpendwa ni kweli sisi tulimpenda ila mungu kampenda zaidi.lililobaki ni sisi tumuombee kwa mungu azidi kumpa pumziko la milele.

    Love u so much my lovely sis,

    Jacqueline

    ReplyDelete
  3. Tunakukumbuka sana mama yetu Mkubwa kwa ukarimu,ucheshi na adabu uliyokuwa ukitufunza watoto wote wa familia.
    We really miss u.
    Otis Kimali

    ReplyDelete
  4. R.I.P Mom
    Tunamiss busara upendo na usimamizi wako mahiri kwenye sekta ya elimu, na maisha kwa ujumla, Mama tulikupenda zaidi lakini Mungu alikupenda zaidi hata akapendezwa akutwae ili ukashirikiane na malaika na wateule wote waliotangulia katika haki kumuimbia. Daima tutakuenzi kwa kufanya yale yote uliyokuwa unayawekea mkazo.

    Daima tutakukumbuka.


    MAZILA

    ReplyDelete
  5. we miss you mama Ruth
    Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Amen

    ReplyDelete
  6. Pole sana Ruth na Mungu aendelee kukutia nguvu na tumshukuru kwa kukupa mama mwenye upendo, hekima na busara tuendelee kumuombea ili apate pumziko la milele na aangazie mwanga wa milele na Mwenyezi Mungu

    ReplyDelete
  7. Dada siku ulipotutoka tulipatwa na simanzi nzito sana,tulitamani watoto wetu nao waishi nawewe kama tulivyozoea kupaita kwako chuo cha mafunzo.Familia ilifarijika sana kwani ulimwacha binti yako pekee lakini hivi sasa una watoto wawili na wajukuu wawili.
    miss u my dear dada
    merina massanja.

    ReplyDelete
  8. Nakumbuka ijumaa alfajiri(tarehe 29-11-1996) sentesi ya mwisho uliyonisemesha uliniuliza "Watoto wangu hawajambo?",sikujua kama ndio lilikua neno la mwisho la kuongea mimi na wewe,dada sikua najua kama Mungu angetutenganisha mapema hivyo,lakini nashukuru yote ni mapenzi yake,tulikupenda,tulikutegemea na tunakukumbuka hekima zako kwa familia pumzika kwa amani.Sitakusahau maishani mwangu,mpaka tutakapo kuja kuonana kwenye ulimwengu wa kiroho.Mdogo wako niliye kupenda sana Sarah Gellege

    ReplyDelete
  9. Rest in peace Emily.
    Daima tutakukumbuka kwa upendo uliokuwa nao juu ya famalia zote na ukoo wote wa Gelege

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...