Balozi nanii, Mdau wa libeneke lako akiwa Nashino stadium na mwanae a.k.a Kansope kuangalia jinsi ambavyo mnyama anaumiza mtu,goli 1-0. Kweli ushindi ni mtaamu sana- siku hiyo ilikuwa ushindi mara mbili Gunner nao walipiga mtu kipigo cha mbwa mwizi.
Mdau wa Ipinda Lusungo Kyela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kweli huyu baba ni mdau sana,jezi,bendera pamoja na mwanae.
    hope mtoto atakuwa kama baba yake.
    Nina differ nae kwa Simba tu,lakini tuko wote Gunners mie Yanga damuu kabisa toka enzi na enzi.
    Daud,NY.

    ReplyDelete
  2. arsenal,liverpool na chelsea wote yanga tutolee shombo uko.simba ni man utd ..vipi wewe???

    ReplyDelete
  3. Madu kama mh. Masha vile?naomba ufafanuzi,ndie au siye yaani kama yeye kabisa.
    Kumbe Masha ni Simba?

    ReplyDelete
  4. Hayo ni mawazo yako-yaani mtazamo wako man u sio simba.
    wewe ndio tutolee shombo la feri.

    ReplyDelete
  5. Hongera mdau umependeza sana na mwanao.kweli ushindi mtamuu.MIchuzi hapo kama amepigwa sindano ya ganzi=mr no comment.
    changia?????

    ReplyDelete
  6. LIVERPOOL NI KIDEDEA NA KIDEDEA NI SIMBA TAIFA KUBWA. WASHABIKI WA MAN UNITED SI WAMEANZA 91 tu HAPO. ILA TUWACHE KUHUSU TIMU ZA NJE MAMBO YOTE SIMBA TAIFA KUBWA. JUMBE.

    ReplyDelete
  7. Nakumbuka mwaka 1990 kipindi Simba inatesa ilikuwa inafananishwa na Liverpool ya kina JOHN BARNES,leo wanafananishwa na MAN U. Washabiki wa Simba vigeu geu.

    ReplyDelete
  8. Wadau hawawezi kuchekelea ushindi wa bongo bila kuingiza mambo ya mkoloni?

    ReplyDelete
  9. Nzuri sana mh. Masha kama ni yeye ,maana kweli wamefanana sana.
    Nitajitahidi nikutafuta mechi ya mtibwa kwani nipo bongo kwa sasa.still remember you mzee wa fitna a.k.a Dr Omary my former collegemate ,you was a very good VP of our student organization that time.vipi ndoto yako ya ubunge bado ingalipo???


    Boma D- aka Mochimochi

    ReplyDelete
  10. sio masha wala nini hawafanani kabisaaa. hongera unaonekana u baba mzuri unatoka na mwanao.

    ReplyDelete
  11. Napenda wababa wanaspend na watoto wao hata kidogo tu...hamna kitu kizuri kama hicho na ambacho mtoto atakikumbuka maishani...

    umnunulie mtoto wako expensive things namna gani kama huna one to one time with your baby is nothing

    ReplyDelete
  12. Kweli huyu anaonekana ni baba mzuri na bora,kwa hali iliyopo sasa sio wazazi wengi ambao wanapenda kwenda out na watoto wao- sababu ni nyingi.ningependa nipate contact za mdau huyu kama unazo kaka michuzi ili nimpongeze sio ,we ona mtoto yuko very happy nadahani huko shuleni kwake hadithi ilikuwa ni hiyo-hongera baba a.k.a Kansope.

    ReplyDelete
  13. arsenal nayo ugonjwa wa moyo tu,wanafunga watoto wakikutana na wakubwa kichapo.

    ReplyDelete
  14. Hongera ndugu yangu,mie niko hoi kwa kipigo hicho.Pian Gunner leo wamepiga mtu 4-1.
    rafikio - MPakistan.

    ReplyDelete
  15. Selina MushiNovember 08, 2009

    Nina swali naomba msaada wa majibu. Natanguliza shukrani.


    Naomba kujulishwa sheria ya Tanzania inasemaje kuhusu mwalimu wa sekondari anayempa mwanafunzi wake uja uzito. Nijuavyo mimi ni kuwa taifa linawaamini walimu wawalee vijana na kuwapa maadili kwa manufaa ya taifa. Mwalimu anapokiuka jukumu hilo na badala yake akawa preditor kwa wanafunzi walio chini ya uangalizi wake - naamini kuna sheria kali itamkabili. Naomba hasa majibu kwa maswali haya:

    1. Hilo kosa liko katika category gani ya makosai?

    2. Mshitaki ni nani?

    3. Mkosewa ni nani - ni wazazi wa binti au ni taifa?

    4. Taratibu za kufuata hiyo sheria zikoje?

    5. Adhabu yake ikoje - yaani inaweza kuwa ni nini?

    6. Je, kuna tofauti kama binti ana miaka 18 au zaidi?

    7. Kesi kama hizo zimeshawahi kutokea na kushughulikiwa kikamilifu kwa kufuata sheria? Kama ndiyo, kuna mifano yoyote? Kama hapana, ni kwanini?

    Natanguliza shukrani

    Selina Mushi
    Chicago
    =================

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...