zikiwa zimebakia wiki chache kabla ya sikukuu ya krisimasi, miti ijulikanayo kama mikrisimasi tayari imeshachanua maua yake mekundu na jiji la linapendeza. hapa ni barabara ya sokoine roa sehemu za posta ya zamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Wamachinga wanailia 'taimingi', muda ukikaribia zaidi, siku tutaamka tukute yoote imekwanyuliwa hiyo.. Bongo 'Twambarare'.
    Mdau, Groningen, NL.

    ReplyDelete
  2. OFISI YANGU ILIKUWA HAPO OPPOSITE KABLA SIJALA PIPA.

    ReplyDelete
  3. du kabla hujala pipa eeeh safi sana..sasa mkuu kabla hujala pipa sa hizi ofisi yako ipo kwa kizee/taahira gani au unabeba wapi box huko majuu mwenzetu....rudi home bwana..

    Mdau Bongo Tambarare

    ReplyDelete
  4. mitikrismass haina maua jamani ni green mwanzo mwisho

    ReplyDelete
  5. mkuu kabla sijala pipa..mkabala na hapo ni benki (maadili-sititaja)..je umeondoka hapo, umewaachia ofisi salama, salimini?..

    ReplyDelete
  6. we unayemtaka jamaa arudi bongo una ajira ya kumpa au mbwembwe tu..kama yeye anabeba box au analea kizee/taahira halafu analipwa fedha ya kumridhisha wewe inakuuma nini? kazi ni kazi tu.tena inaelekea wewe uliwahi kuishi ulaya ukapigwa bomba kwa kukosa viza sasa wivu tu ndo umekujaa..wabeba mabox hata bongo wapo,waangalizi wa vichaa au mataahira hata mirembe wapo.nishukuru kwa kukupiga msasa

    ReplyDelete
  7. Bongo tambarare wapi bwana. anaye piga box mwache apige box, kwanza nyie mnaosema mbeba box arudi akipiga box atakupa japo picha tuu kwenye frem nyie ndo mnaziiba, alafu mnakalia bongo tambarare what the ...

    ReplyDelete
  8. SICHAGUWI KAZI, KAZI NI KAZI NA KULA PIPA SI LAZIMA IWE UMEENDA ULAYA PENGINE NIKO MAPUTO JE AU BURUNDI, MSIWE NA MTAZAMO FINYU, KUWA PIPA BASI ULA AU AMERICA, KWA TAARIFA TU NIPO OMAN NAFUNDISHA KISWAHILI NA BEI NINAYOPATA NI KUBWA, MARA ZAIDI YA MIA NILICHOKUWA NAPATA HAPO NYUMBANI AND TAX FRE SILIPI KODI HATA KIDUCHU.

    ReplyDelete
  9. kama wewe uko oman sasa kwanini umshauri mwenzako arudi home? unajua yeye huko anakobeba box au kulea vizee/taahira analipwa kiasi gani? wewe ndio una fikra finyu unapodai bongo tambarare wakati mwenyewe uko oman..usiwe mvivu wa kufikiri wewe..mi ntaendelea kukuelimisha tu.mpiga box,mwalimu wa kiswahili,mlea vizee/taahira wote wanatafuta riziki bila kujali wapi wanakoishi

    ReplyDelete
  10. eti unauliza ofisi ya jamaa iko kwa kizee/taahira gani huko majuu.unaonyesha ni jinsi gani ulivyo fukala kimawazo kwa kufikiri kuwa kazi pekee ya watanzania walioko majuu ni kubeba box au kulea vizee/mataahira tu..kuna kazi nyingi tu na pia haijalishi wala haikuhusu mwenzako anafanya kazi gani,mind ya own f***ing bussines..kazi ni kazi tu.usiwaonee wivu walio majuu..wadau endeleeni kumpiga msasa mzalendo

    ReplyDelete
  11. WE MDAU BONGO TAMBARARE UNAMWAMBIA MWENZAKO ALIYEKULA PIPA ARUDI BONGO,UNA ISHU GANI YA KUMPA AKISHARUDI BONGO? NINI KILIKUSABABISHA UHISI OFISI YAKE IWE KWA KIZEE/TAAHIRA AU YEYE NI MBEBA BOX? NA UNAJUAJE KAMA HELA ANAYOLIPWA HUKO MAJUU NI MIYEYUSHO MPAKA UMSHAURI ARUDI BONGO?..ACHA MAKUZI WEWE OMAN UNATAFUTA MAISHA NA BONGO WANATAFUTA MAISHA NA MAJUU PIA WANATAFUTA MAISHA..KAMA UNAONA BONGO TAMBARARE BASI NA WEWE RUDI BONGO

    ReplyDelete
  12. dah we mdau unaedai uko oman unafundisha kiswahili miyeyusho kweli! mbona kiswahili chenyewe kinakushinda? pale unaposema ''bei'' unayolipwa ni mara mia....nadhani ungetumia neno mshahara/malipo badala ya ''bei''..nawasikitikia wanafunzi wako kama ni kweli wewe ni mwalimu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...