Miss Earth Tanzania 2009 Evelyne Amasi (pichani) amerejea leo nchini akitokea nchini Phillipines alipokuwa akishiriki mashindano ya Miss Earth 2009.
Fainali ya mashindano haya ilifanyika tarehe 22 mwezi huu Boracay nchini Phillipines. Ingawa Evelyne hakufanikiwa kuingia kwenye 16 bora(top 16) lakini amefanikiwa kupata tuzo ya Vazi bora la Taifa(National Costume) akiwapita warembo wengine takriban 80 kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Vazi la mrembo huyu ambalo ndilo lililomletea ushindi limebuniwa na mwanamitindo chipukizi kutoka mkoani Morogoro Diana Magese ambapo ametumia kamba kamba kutoka kwenye magome ya miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Are Ya'll feelin that Get Up!!

    ReplyDelete
  2. WHATS THE DIFFERENT BETWEEN MISS WORLD AND MISS EARTH! PLEASE NIJULISHENI

    ReplyDelete
  3. kamuulize lundenga na chipungahelo sijui mpunga wa leo.

    ReplyDelete
  4. Mtoto wa CoastNovember 28, 2009

    Michuzi tunakushukuru kwa kuturuhusu tufundishane hapa.

    Hata mimi hakika huwa sishabikii sana mambo ya umisss kila wakati maana kweli wadada wengi wanaweza kulemaa badala ya kuchuchumilia masomo kama ambavyo DRC watoto wengi wamekuwa wanawaza kuzungulusha au kuchalaza nyuzi kwa meno wakiwa na akina Koffi na wenzake huko Paris!

    Lakini pia sitovumilia hasilani baadhi ya watu wanaotaka kuharamia na kutukana URAIA wetu eti kwa vile tu wanaishi Canada au USA au Ulaya au popote nje ya nchi.

    Kama ni usodoma na ugomora je TZA ni zaidi ya USA, Canada & hata Ulaya?

    Ni huko mliko enyi waosha vinywa ambako si tu sera za vichupi zinapangwa na kuratibiwa bali kuna hata kwata (parade) za uchi wa mnyama, kwata za mashoga na wasagaji.
    Mnaongelea eti TBL, SERENGETI, ZAIN n,k ndio zaidi kuliko huko mliko? Mimi nina wasiwasi kama kweli mnaishi huko!


    Hivi kweli kuhusu maadili yanayokubalika ya ujumla (Universal Ethics)kati ya nchi yangu Tz na huko mliko, ni wapi kuna majumba ya Makumbusho ya ngono (Sex- Museum);

    Ni wapi watu wanapotoa fedha zao nyingi kwenda kuangalia si tu sinema za ngono bali mechi live ya ngono tena ya makundi (group sex);

    Ni wapi katika matangazo manne barabarani moja lazima liwe na picha ya mtu aliye nusu uchi;

    Ni wapi kuna kesi kibao zaidi leo hii za hata watumishi wa Mungu si tu kuzini bali kuwaingilia watoto wa kiume kinyume na maumbile;

    Ni wapi badala ya kujadili mambo ya maana mabunge yanapitisha miswada ya kutambua ndoa za jinsia moja;

    Ni wapi penye mvutano mkubwa juu ya ruhusa ya kutoa mimba, mtu anavyojisika (hata kama si kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama au kwa sababu za kitabibu);

    Ni wapi vijana wanaweza kwenda beach na kuanza kurushiana matusi ya nguoni huku wapiga picha na television vikirusha hewani matusi hayo hadi apatikane mshindi akazawadiwa;

    Ni wapi kuna televisions na au vipindi vingi hewani vya ngono (tena isiyo salama) vyenye majina kama vile:
    The Adult Channel- UK
    Adults Only Channel - Australia
    Adults Only Select - Australia
    AOV Adult Movie Channel - Canada
    Blue Juice Television - UK
    Fyre TV - USA
    HARDtv - Canada
    Hustler TV - Canada
    InXtc Tv Channel - Europe
    Maleflixxx Television - Canada
    Peephole.TV - United States
    Pink TV - US (known as Heat TV in Europe)
    Playboy TV - USA
    Playboy One - UK
    Red Hot TV - Canada
    Sex TV - Canada
    SexGay.TV - Italy
    Showcase - Canada
    Spice Network - USA
    TEN Networks - USA
    Television X - UK
    XXX Action Clips Channel - Canada
    REN TV - Russia
    Extasy - USA n.k

    ReplyDelete
  5. Mtoto wa CoastNovember 28, 2009

    Eti una uraia wa Canada so what?


    Ni wapi enye waosha, Taifa linasherehekea sherehe nyingi zenye mahusiano na uchawi na shetani na maonyesho ya giza kama halloween,Devil's Night,Walpurgis Night,Day of the Dead,Ghost Festival,Qarqe'an;

    Ni wapi ambapo machapisho na sinema za ngono na ya kishetani kama vile THE WONDERFUL WIZARD OF OZ, by Eric Shanower and Skottie Young na viabu 7 vya HARRY POTTER ambvyo yapata zadi ya nakala Millioni 400 za hadithi za kichawi-chawi vimeshauzwa na kinapotoka wananchi wanalala kwenye foleni ya duka la vitabu mithili yetu tulipokuwa tukijipanga usagishaji kwa ajili ya 'yanga' wakati wa njaa;

    Ni wapi kuna Jamii za kificho za giza nene (secret societies) ambazo jamii kubwa hakika haijui wanachokifanya kama vile wanaume wa Free-masonry;

    Ni wapi kuna unafiki wa kupiga marufuku ndondi za mbwa (dog fight)wakati wanaruhusu human cage-fight ambapo mtu anakupiga vyovyote na chochote hata kama ni kukungóa jino kwa goti. Ni huko huko mnakoshabikia na kuunda meleka ya kitoto ya kupanga na yenye majingambo uchwara na ambapo hakuna sheria maana hata refa anaweza pigwa na kiti na mpiganaji anaweza kuja na jeneza badaye likawa lake. n.k list ni ndefu sana.

    Yaani wanajifanya kumshangaa binti wa watu Semenya (aliyezaliwa hivyo na kulelewa kama binti) kushiriki mbio za akina mama wakati huko kwao wapo wanaoamua kubadili maumbo na wanasisitiza kuwa jinsi(a) ni uamuzi wa mtu anavyojisikia.

    Mnasema tunapenda mambo ya udanganyifu danganyifu nani kakwambia huko hakuna? Ninyi hamuishi huko waulizeni wanaoelewa njisi FIFA & UEFA inavyopambana na udanganyifu wa uzalendo wa kifisadi katika mechi kibao zilizopita.

    Baada ya Marion Jones (medali 5) na Andrew Agasi (bingwa mara 8) kutoka hadharani na kukubali kuwa walikuwa wanabwia viongeza nguvu sasa siamini kuwa watu wenu huko huwa wanatushinda kihalali. Yaani yeyote bingwa unayemwona sasa wa uko mpe tu muda tutakuja sikia kuwa alikuwa anabwia sukari fulani! Maskini pengine akina F.Bayi, Nyambui, Ikangaa n.k wangekuwa bado wana record zisizovunjwa! Ninaamini kuwa hata akima Matumla na Cheka wako juu ya hao watu wenu maana wa kwenu wakichunguzwa watakutwa ama wanabwia sukari au wanapanga matokeo na mshiko kugawiwa!

    Halafu katika kulea watoto, pamoja na matatizo yetu TZ, huko mnakoshabikia ni mkanganyiko mtupu. Maana haki za mtoto zinageuzwa kuwa kubwa kwa gharama za haki za mzazi na jamii kwa ujumla! Na hakuna mtu wa kumwambia mwenzake kitu ndiposa golikipa anajinyonga halafu baadaye kunakuwepo na mazishi ya heshima kubwa sana wakati hakika mtu huyo angepona angetakiwa kujibu mashitaka na hata hivyo pamoja na kufa hajapona adhabu ya milele inayowasubiri kundi la akina Yuda Iskariote!

    Mtatuambia nini enyi waosha hapa hakuna cha John Mashaka wala nani akae huko huko maana hatuna nafasi hata ya mwenyekiti wa mtaa ambaye anasubiri kupewa mfasiri au mkarimani wa Kiswahili kama mlemavu.
    Mkae huko huko ambako wakati sisi watu wanaweza kugate-crash kwa kuruka ukuta kuingia uwanjani ninyi huko ni hadi Ukulu; wakati sisi huku DC ndie wa mwisho juu kutuhumiwa ugoni ninyi huko ni rais na ikabidi akiri kwa kilio mbele ya screen!

    Msipende kudharau utu wala uraia wa mtu mkafikiri kuwa tutakaa kimya hapa. Ninyi ni watu hatari sana maana nia yenu ni kuchochea misimamo isiyo kiada (extremism) ya vuruigu watu wajichukie na kijidharau!

    Shetani toka hapa!

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu mtoto wa Pwani, umeongea falsafa nzito sana, ambapo kama waosha vinywa wa huku ughaibuni na watanzania kwa ujumla wataisoma kwa makini, watapata mazingatio makubwa. Inabidi upewe ukurasa kwenye gazeti la Mwananchi Jumapili, uwe unatuandikia chambuzi mbali mbali, kama wafanyavyo wakina Freddy Macha na Ndesanjo Macha. Keep it up.

    Mtu Mzima hapa.

    ReplyDelete
  7. we mtoto wa coast kama ulinyimwa viza kaa kimya na ishu zako za ni wapi ni wapi inahusu?? hata bongo mnatamani saana mambo haya sema tuu mnajidai wajahidina wakati ngono nje nje tena haya mambo mnayamaindi saana ebu nenda pale namnani kama utapata chumba we unadhani juu ya nini???? wameweka chaneli moja mahususi hivyo hata wakulukulu wanji wanajivicjari pale next time ukienda kuomba viza uende na vigezo vya kutosha utapata tuu acha donge
    mdau canada

    ReplyDelete
  8. Tatizo la mtoto wa pwani na watu wa aina yake ni kidomodomo,sasa unajidai na Tz yako kwa kuwa kiwango cha uhalifu ni kidogo kuliko hizo nchi unazoziponda ila hao wanaoongoza kwa uhalifu na uchafu wa kila aina wapo wapi leo kiamaendeleo na sisi waTz wenye kujali ubinadamu na kufata njia sahihi kimaadili tupo wapi leo kimaendeleo??

    Ungelijua hilo nadhani usingethubutu kusema hayo usemayo,tena kwa kuposti 2 times ka utalipwa vile,wenzako walianza siku nyingi na wakati wanaanza,hayo mauchafu yao hayakuwa kama yalivyo leo,we hujiulizi kwanini?
    Jibu ni rahisi,piga shule ndugu,hata sisi tungeanza shule kiukweli mapema kama wao basi mauchafu hayo yangekuwa kwetu na wala usingeona ka ni mauchafu na huenda ungekuwa ni mmoja wa wafanikishaji wa mauzauza hayo,kama unavyojiita eti mtoto wa Coast! Ndo nini sasa? Ni hiyo shule ingawaje ni ndogo kwako ndo imekufanya ujiite hilo jina,na kuweza pia kuchanganua na hatimaye kutoa ulinganifu kati ya Tz na Canada/Ulaya.

    Wenzako walisoma na wanasoma kwa uhakika na sio kama Tz watu wanagoma bila mpangilio,na wataalamu wanachekelea shahada zao badala ya kuzitumia kwa vitendo.Hao wacanada/wazungu unaowasakama wewe wamepiga shule na kunapokuwa na idadi kubwa ya wasomi hapo ndo maendeleo katika kila nyanja,idara na sekta mbalimbali yanapoanzia,watu wanafikiria namna ya kusonga mbele yani kutoa huduma bora na za kisasa zaidi na sio kukalia kushabikia umiss na uzinduzi wa bia usokuwa na manufaa kwa nchi,wenzako ni walevi but nchi yao huwezi kulinganisha na ya kwetu hata kwa thelusi moja,kwa kifupi ni kwamba kila mmoja katika nafasi yake ya kazi anakomaa ili awe bora zaidi ya awali.

    Wasanii kwa nafasi na aina zao wanajitahidi kufanya kazi zao ziwe bora zaidi,wanahabari ka Uncle Michuzi nao wanajitahidi kwa nafasi zao,wanajeshi na askari wa aina zote wanajitahidi kubuni njia za kupambana na uhalifu na namna ya kuwa na vyombo imara na vyenye nguvu huenda kushinda nchi nyingine,wanasayansi nao vivyohivyo wanasonga mbele na ndo maana wewe mtoto wa Pwani umeweza kutumia computer ya mcanada na wenzake kutuma hizo posti zako zisizokuwa na maana,madaktari,wanasiasa,walimu,wachungaji,wanahistoria na wengine wengi kwa aina zao wanasonga mbele kuhakikisha wanatoka na kitu roho inapenda.

    Sasa kama na wao wangekuwa kama wewe mTz AKA mtoto wa Pwani unaelala na kusubiri TBL azindue bia mpya ili uchekelee ukidhani hayo ndo maisha,au kuchekelea na kushabikia umiss ambao hakuna mafanikio yeyote ya kihistoria hadi leo hii,unadhani ungeweza kumtumia michuzi hizo posti zako za ajabuajabu? Unajua kimetokea nini hapo katikati mpaka wewe ukaweza kuandika hizo porojo zako na hatimaye Michuzi akazipata na kuziweka bulogini ili wadau nao waone ni jinsi gani usivyotulia na usivyomakini hata kwa uchangiaji maoni??!!Unadhani utaalamu huo unapatikana kwa kusubiri TBL azindue bia mpya ili wewe uchekelee au kushabikia umiss ambao umeanzia kwa hao wacanada/wazungu??
    Hamna siri hapo mtoto wa Pwani ni shule tu na hata huyo Harry Potter unadhani ni uchawi ndo unakufanya wewe umuone anavyojivinjari hewani na mbwembwe zote azifanyazo kwenye sinema yake? Shule,shule,shule..ohoo!

    Inaboa na inakera kuona mtu anajiandikia tu na kulaumu bila sababu ya msingi,wewe wahimize viongozi wako na waTz wazingatie elimu na tukishakuwa kama Canada/ulaya ndo useme hizo porojo zako,ufisadi na kuendekeza rushwa pamoja na kutaka maendeleo/utajiri au kutoka kirahisirahisi ndo kunafanya watu watoe maoni yasiyo kuwa na msingi na hatimaye kudhorotesha maendeleo kwa kusemasema na kupiga majungu na kidomodomo tuuu siku zote,kwanini sisi tushindwe hata kuchimba madini yetu au kuvua samaki wetu wenyewe au kuongoza na kuanzisha makampuni yetu wenyewe mpaka mcanada/mzungu aje? Tatizo ni shule na kama shule iliendeka basi tatizo ni kupata zero.

    Shule,shule,shule....shule jamani ohooo...

    Potz.
    (Mashariki ya mbali)

    ReplyDelete
  9. Mtoto wa CoastNovember 29, 2009

    Mtu mzima asante.

    Potz na wengine sijawahi kukurupika kuandika kiasi hicho. Hili lilikuwa jibu kwa wachache walio nje ambao wanaanza kushambulia Uraia wa Tz na kutamba oh sijui watoto wao wana uraia wa canada n.k. Niliweka comment zangu hapa makusudi maana palioanza haya malumbano kwenye posting ya Miss Tz 2008, palishapitwa na postings nyingine kibao na hii ikawa ndo angalau iko juu ili msome na kutafakari.

    Kwa taarifa, nje ya nchi ndo kanyaga kila wakati. Hardly nimekaa na passport miaka mitatu bila kubadili kutokana na kurasa kujaa sticker za visa na kugongwa mihuri.
    Ninatambua kuwa tuna changamoto kibao Tz za kiuchumi, kijamii na kisiasa na ninaandika sana ninapopata nafasi.

    Tunatakiwa kuisaidia nchi yetu kwa kutoa ushauri wa maana.
    KAMWE SITARUHUSU MTU YEYOTE ANITUKANIE URAIA WANGU AU KUNIAMBIA ETI KUWA TZ TUNAENDEKEZA UMALAYA AU UHUNI KULIKO NCHI NYINGINE! HII NI HUKUMU BATIRI!

    Hizo ni kauli ambazo hazijaenda shule. Namshukuru mtu mmoja hata ilibidi aseme kuwa wajanja hata kama wako nje hawapondi kihivyo nchi yao. Toa ushauri mzuri wa kuboresha demokrasia, matumizi ya nishati, kuinua uchumi, kuboresha elimu n.k lakini KAMWE KUTUKANA URAIA WANGU NITAKURUDI BILA BREKI!

    Na kama unafikiri kuwa Tz ni uhuni tu muulize Mh. Andrew Young na heshima zake amesema nini leo kwenye CNN Inside Africa.

    Tujitahidi kutumia elimu yetu kushauri juu ya maendeleo na sio kutamnba juu ya habari ya RPs za wana wetu na immigration status zetu popote tulipo!

    ReplyDelete
  10. nchi yetu ya tanzania ni nzuri sana ila viongozi wetu wametuangusha sana na bado wanaendelea ndo mana watu wanahasira kali na wengine wameamua hadi kuukana uraia wao ni poa tu manake wanatafuta maisha bora ambayo tuliahidiwa mpaka leo ni ndoto ndo kwanza umeme mgao maji mgao barabara kitendawili usafiri mh wakati kwa wenzetu hivi vyooote vipo tangu enzi maisha bora kwa kila mtu manake vitu vyote muhimu vipo sasa hii kitu inakatisha tamaa sana wandugu acheni tu watu wajiite wasomali wairaq wakandahar ni kutaka maisha bora elimu bora kwa vizazi vyetu tulivyovipata ughaibuni KAULI MBIU: TANZANIA BILA RUSHWA HAIWEZEKANI!!!!

    ReplyDelete
  11. Mtoto wa Coast, asante sana kwa maoni yako. Hakika umenisemea nami pia. Nilikereka sana (a few days a go) niliposoma maoni ya mtu mmoja kuwa watoto wake hawataikanyaga Tanzania kisa yeye ameukana uraia wa Tanzania. Angejua angenyamaza kimya. Tanzania yetu tunaipenda yeye na wanae waishie huko huko Canada hakuna anae wataka huku! Nasafiri sana kikazi (USA, UK, Asian countries) lakini sijawahi kutamani kuishi nje ya Tanzania. Kwa waosha wote waliojilipua ni kwamba tunawaonea huruma maana wengine mnashindwa hata kuwazika wazazi wenu. Loh! Poleni kwa utumwa wa kujitakia mliopa jina la KUTAFUTA MAISHA!

    ReplyDelete
  12. dah wee "mtoto wa coast" umenikuna ajabu apa macho yamentoka pima kwa uchambuzi yaonekana kweli wapenda nchi yako
    sio malimbukeni wanaotukana nchi walizozaliwa simply anapata dolar,dollar nn bwana???

    ata km nchi iko gizani haimaanishi Mungu alituumba kimakosa na nchi yetu...nyambaf na akili mbofu wote wanaotukana wa kwao wamelaanika!!

    ni ivi ata km tungekuwa tunaishi juu ya miembe ni maisha yetu na kivyetu,,,katu hatutafanana na uku tunakoishi na kung'ang'ania sijui upuuzi gani wa uraia!!

    acha kila mtu na fani yake mwataka wooote wawe ma-profesa???ovyoo

    ovyo sana

    ReplyDelete
  13. KAKA MICHUZI SPECIAL REQUEST!!


    Michuzi nakuomba tafadhali sana tena sana ebu copy na uweke maneno yote ya 'mtoto wa Coast' kama alivyochangia hapa. Ni mazito sana kaka Michuzi. Ebu tuyatafakari na kuyajadili kama mada inayojitegemea (new post).

    Waweza kuweka kichwa cha habari kuwa: MAISHA YA UADILIFU BONGO AU UGHAIBUNI?
    Halafu uyaanike anayoyasema, naamini wengi tutaguswa na uchambuzi wake.

    Naona alikuwa anawajibu wadau waliokuwa wanaponda Tz kuwa tunaendekeza umalaya au kwamba hatuna maadili kulinganisha na huko nje lakini yametuelimisha wengi katika yale tusiyoyajua.

    Tafadhali Michuzi najua wewe ni mtu ambaye una upeo mkubwa maneno hayo ya huyo jamaa hayawezi kupita tu kama maoni hebu tuyatafakari na kuwapa watu nafasi kuyajadili.
    Ndio maana ya kuwepo libeneke la jamii lililotukuka katika kujadiliana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...