



Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Bungeni: Richmond yalala doro
ReplyDeleteNa Mwandishi wetu
6th November 2009B
Sakata la mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, limelala doro tena.
Hiyo inatokana na ukweli kuwa Bunge litaahirishwa bila Serikali kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa maazimio 23 yaliyotolewa na chombo hicho.
Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za Bunge iliyotolewa leo asubuhi, kikao kilitarajiwa kuahirishwa leo na wala hakuna muda uliopangwa kwa ajili ya Serikali kutoa taarifa hiyo. Badala yake ratiba ilionyesha nafasi ya Waziri Mkuu , Mheshimiwa Mizengo Pinda kuahirisha Bunge.
Taarifa hiyo ya Serikali kuhusu Richmond, ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge wengi pamoja na wananchi kwa ujumla ili kujua nini kimefanyika kuhusiana na maazimio hayo 23.
Miongoni mwa maazimio hayo ni lile la kutaka Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), kutakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo ya mkataba tata.
Picha ya kwanza juu, naona mtasha wa kwanza kulia kauchapa usingizi kama vile kingunge wa bongo anasubiri muda wa posho tu...wizi mtupu
ReplyDeleteHuyu mama ni kichwa safi kwani tulipokuwa naye NY,NY enzi za balozi Mwakawago tuliona vitu vyake.Go mama Mulamula go.....?
ReplyDeleteHiyo ndio vakesheni ya mkuu wa nanihii huko burundi
ReplyDeletekila safari yake yeye ni vakesheni hasemi kama anaenda kupiga picha wakubwa na kuchukua habari ndio kibarua chake cha kumuweka mjini
yeye anasema vakesheni na fulana yake ya kichawi aliyopewa na mganga wake kama sindiko
haya mkuu wa nanihii weka wazi ajira yako ieleweke kwani unawapotosha jamii kwa kusema unaenda vakesheni na kumbe ni safari za kikazi.
Lakini kwenye kamkutano ka asasi za jamii kule finland mwaka fulani alijaza watu wa kasehemu kamoja tu na hata mzazi!
ReplyDeleteMmmh!! huyu Anonymous wa Sat Nov 07, 02:20:00 PM
ReplyDeleteInaonekana hizi vekesheni za mkuu wetu zinamkereketa kweli kweli....Anyway ndo binadam tulivyo!!
Mheshimiwa balozi kula vekesheni baba,na utuhabarishe zaidi na zaidi.
mkubwa ni kalonzo musyoka sio kalonzi musyoki.
ReplyDelete