MZEE ROBERT L. FERUZI
1946-2009

Ndugu, jamaa na marafiki, Tunasikitika kuwajulisha ya kuwa Mzee Robert L. Feruzi was Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumapili [Nov 15th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwake
98 Itasca St,
Mattapan, MA

Tunawaomba ndugu zetu mtusaidie kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi. Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili, Jeneza pamoja na gharama zingine ambazo kwa kawaida huja na haya matatizo.

Unaweza kusaidia kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:

Innocent E. Lugumamu
BANK OF AMERICA,
ROUTE NUMBER :011000138
ACCOUNT NUMBER:004628572563
Address: 12 Walker St, Lowell, MA 01854

IMPORTANT: Kwa wale waliopo nje ya state ya Massachusetts, Out of state deposit circle (zungushia) namba 77 , MA. Unapotuma pesa. (haya ni maelezo muhimu toka kwa bank of America)

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:
Innocent E. Lugumamu 978 996 7690
Steven Buberwa Mutasa 603 320 3220
Crispine Kahabuka 603 261 0802

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU.
Email-Address:-
au
stevebube@gmail.com




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Pole sana kwa msiba huu mzito, tuko pamoja nanyi kwenye hiki kipindi kigumu na tunawaombea kwa mwenyezi mungu ili uwatie nguvu.

    ReplyDelete
  2. Pole sana familia ya marehemu kwa msiba huu mzito, "inna lillah, wainailah Rajiun"

    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  3. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen

    ReplyDelete
  4. poleni Devota diva na Norbeta kwa kufiwa na baba yenu.

    ReplyDelete
  5. Ndugu zangu na haswa wahaya wenzangu naombeni tujitolee kwa hali na mali kuhakikisha tunaupeleka mwili wa bw robert feruzi nyumbani kwa mazishi popote mlipo
    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

    ReplyDelete
  6. Poleni sana jamani kwa msiba huu mzito!

    Namkumbuka huyu Mzee years back alipokuwa akija kumleta shule bintiye Marehemu Samiha pale Bunge Primary School.

    Mungu azilaze roho za marehemu wote waliotangulia mahali pema peponi amin.

    ReplyDelete
  7. Poleni Devotha na Robetha! Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  8. msiba ni wa wote wee boara apo juu acha ukabila, eti wahaya wenzangu! whaaat! usitenge watu kwa kigezo cha kikabila.

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wafiwa.
    Mungu awape faraja yake katika kipindi hiki kigumu.

    Wewe Anonymous wa Tarehe Tue Nov 17, 11:45:00 AM,
    unaposema "haswa wahaya wenzangu" unaanisha nini?Hii ni tabia chafu sana....usituletee ukabila wako...inamaana angekua Muha,Mdengereko,Mzaramu,msambaa,mchaga,mhehe,mgogo,mmatumbi au msukuma ingekuwaje?

    embu badilisha kauli yako..sisi wote ni waTanzania

    ReplyDelete
  10. POLE MUGA UMEBAKIWA MKIWA MDOGO WANGU KUONDOKEWA NA BABA YAKO,MUNGU AMLAZE PEMA MZEE FERUZI KAMA NAMUONA MIAKA HIYO AKIWA NA WATOTO WAKE MAREMU SAMIHA NA MUGA,MUGA MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO

    ReplyDelete
  11. POLE REBECCA FERUZI KWA KUONDOKEWA NA BABA....NDIO NIMEJUA LEO KUWA ROBERTA NA DEVOTHA NI NDUGU ZAKO WA BABA MMOJA POLENI SANA

    ReplyDelete
  12. POlen sana Roberta,Devota na Andrew kwa kuondokewa na baba,Mungu awatie nguvu.

    ReplyDelete
  13. Poleni Roberta,Devorta na Andrew kwa kuondokewa na baba,bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.

    ReplyDelete
  14. Wanaijeria wameshapata account number na routing number.. Tusubiri kusikiliza mtu kalizwa soon.

    Poleni sana wafiwa kwa msiba huu. Mungu ailaze pahala pema peponi roho ya marehemu.

    Ushauri wabure; Baada tu ya kumalizana na shughuli hii nakushauri mhusika ufunge hii akaunti. You know what I mean.

    ReplyDelete
  15. Robert, Devota na Andrew poleni sana. Nimeyapokea kwa masikitiko kuitwa kwa mzee wenu Feruzi ambaye alikuwa mwanafunzi mwenzangu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Though that was some 38 years back my memory still carries him as an always joyous man, capable of making even a funeral hilerious.

    Be cool, look on to God for real consolation and for the supply of all that is needed to lay his body in his temporary mansion pending resurrection.

    Samson M.E. LUHIGo

    ReplyDelete
  16. Poleni sana Roberta,Devota, Rebbeca na Andrew kwa kuondokewa na mpendwa baba yenu. Mungu awape nguvu ktk kipindi hiki kigumu cha majonzi.

    Mkunde.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...