Maalim Seif Shariff hamad

Jumuiya ya Wazanzibari waishio Uingereza(ZAWA-UK) inawapongeza Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kwa kukutana na kuazimia kuwaunganisha Wazanzibari ili kuhakikisha kuwa Visiwa vya Zanzibar vinakuwa na amani,mshikamano na kufungua milango zaidi ya maendeleo. Hatua hii waliyoichukua tunaamini itafungua ukarasa mpya
katika siasa za Zanzibar.
Ahsante,
(Abdulla A. Abdulla)

Mwenyekiti, ZAMA, UK Rais Karume

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. At last. Pongezi kwa viongozi na wadau wote wa mchakato huu. Kwa kweli zanzibar kama mtakuwa na nia njema ya kuungana ili kuleta maendeleo kisiwani na Tanzania kwa ujumla hongereni sana. Muwe na nia njema na msiwe wanafiki maana kwenye msafara wa mamba na kenge pia wamo. Mkifanilkiwa mtakuwa mfano wa kuigwa kwa upande wa Bara na afrika kwa ujumla.

    K.O.R.

    ReplyDelete
  2. nyie wapemba rudini Tz sasa acheni kubeba maboksi huko UK.pia mnatuletea magari mabovu na mafriji huko ni kuharibu mazingira.lete magari mapya sio ya kuokota.

    ReplyDelete
  3. Sasa inamaana kuazia sasa hivi kutakuwa na haki huko visiwani na watu hawatanyimwa tena hizo ZAN-ID na kujiandikisha kwa uchaguzi na kutakuwa na Tume Mpya na Huru ya uchaguzi? Mbona hatujasikia kauli hiyo kutoka kwa watawala? Na bila ya kusawazishwa hayo ni kweli kutapatikana amani na umoja?
    Hebu munaojua zaidi tuelimisheni,vyenginevyo badala ya hizi pongezi tutapeana tena pole wakati na baada ya uchaguzi.

    ReplyDelete
  4. Waunganisheni wa huko z'bar na tz kwanza wa huku wameshadata msijisumbue

    ReplyDelete
  5. ivi unaposema zanzibar na tanzania una maanisha nini??
    no wonder u dont develop stupid!!

    ReplyDelete
  6. Huyo mpumbavu haelewi, Eti Zanzibar na Tanzania!!!! Zanzibar iliungana na Tanganyika ndio maana ikaitwa Tanzania. Ukisema Tanzania inamaana ushaichanganya Zanzibar hapo. Kama unataka kuita majina mawili sema Huko Zanzibar na huko Tanganyika. Not zanzibar kisha Tanzania. Ulikuwa wapi wewe miaka yote hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...