Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, akipanda mti mwanzoni mwa wiki kuashiria kuzinduliwa kwa maadhimishi ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA) mnamo Julai 1984.Picha na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. HIVI KWELI JEMBE LIKISHIKWA KIMASIKHARA KIASI HIKI TUTAFIKA KWELI!!!!!......Kaka Michuzi ondoa hii picha.......mzee wa watu atatupiwa madongo mpaka kutakucha.......hao vijana wake wanaojiendesha kwa sera za migomo sijui wataandika nini humu leo.....Kha!

    ReplyDelete
  2. Hii ndio Kilimo ndio wa mgongo wa taifa la Tanzania,tulio wengi tunatokea vijijini (origin)na tunajua jinsi ya kutumia jembe la mkono,hapa waziri magembe anatoa fundisho gani kwa wananchi,ati anapanda mti,amewekewa kitambaa kwa magoti yake,its better asingetoa mfano,kama wakulima wakiona picha hii lazima wawe dispointed,au kukichukia kilimo kama kazi ya kitumwa,
    Ushauri wangu viongozi wanatakiwa kuvaa nguo zinazoendena na mazingira ya shambani,ili kuwashawishi wakulima,waione kazi hiyo hata viongozi wanaweza,kiongozi inabidi awe mfano,ENZI ZA MWALIMU ANGELAMBA ZAKE HAMSA WA HAMSINI,kwa wale watoto wa juzi,hamsa wa hamsini ni viboko 50,25*2 kwa kutumia mjeledi wa kikoloni,viongozi waige mfano wa mwalimu alikuwa anavaa gam boot anapofanya demo,sasa magembe analeta ubishoo,hata mimi nilitaka kwenda kulima siendi tena,tutabanana hapahapa Bongo!
    rgds
    Kisenga

    ReplyDelete
  3. Hivi hao waliomzunguka WANACHEKA NINI SASA?!! huyo ni prof, waziri wa ufundi sio kilimo na hatakiwi kuchafuka na kupindapinda mgongo!! aftaro buti zilikuwa hazipo coz alishtukizwa na tukio... anywayz kwa waosha vinywa waziri naye anasapoti kilimo kwanza.

    ReplyDelete
  4. Watu wa itifaki na maswala ya mavazi nisaidieni, kwani ilikuwa lazima kwa Profesa kuvaa suti wakati wa kupanda mti? Au aliombwa ghafla baada ya kufika SUA?

    ReplyDelete
  5. huyu kapiga magoti ana swali au anasali?

    jamaa tuache ubishoo...vinginevyo huku ni kuhubiri watu waache dhambi wakti mwenywe ndio Zero!

    ilibidi aonyeshe kwa vitendo jinsi ya kupanda mti..na sio kuchutama na kushika mpini wa ..jembe kichwa chini juu!

    ReplyDelete
  6. KWELI TZ TUNA KAZI... MMH NO COMMENT

    ReplyDelete
  7. Hii ndiyo shida yetu Watanzania, maana unapoangalia background ya huyu waziri wetu ni 'forestry' sasa kwa sababu ya utamu unaopatikana kwenye siasa angalia tu hata namna picha inavyojieleza. Tuna kila sababu ya kukubali kuwa bado tuko nyuma sana, na hii yote ni kwa sababu ya kukosa maono na hivyo kujiendea tu, nina shaka hata na ukuajia wa huo mti maana miti mingi inayopandwa kwa mbwewe zisizo na tija huishia kukauka tu, tubadilike watanzania wenzangu

    ReplyDelete
  8. duh haya majembe kumbe bado yapo? tunaingia karne ya 21 kwa kasi mpyaaaa

    ReplyDelete
  9. Sasa kama kiongozi wa umma anayetakiwa kuwa mfano wa kilimo kwanza ana-struggle na jembe kwa ajili ya kupanda mche tu tunawaonyesha nini wananchi wa kawaida.

    Mtu ambaye hayuko tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli kama hii hakupaswa kuwa mgeni rasmi. Hii ni fedheha sana kwa mkulima.

    ReplyDelete
  10. samahani michuzi, lakini penye ukweli lazima tuzungumze huyu waziri anatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  11. kumbe inawezekana kulima huku umepiga magoti kwenye kapeti sijui, now u r talking...sasa ntakuwa mkulima nimekua insipayadi sana, mimi ntaleta kochi kwa sababu sitaki kupiga magoti, ntakaa kwenye kochi huku nalima, nikichoka nalala, kidogo, pia pembeni ntakua na kifriji huku safari baridi ikiendelea kupoa, na stereo huku nikipata muziki kwa mbalii, na tv kwa pembeni, na ntapiga simu kwa mangi mchoma chips aniletee chips mayai na mbuzi wa kuchoma kando,,,

    ReplyDelete
  12. sioni tatizo hapo. baada ya kupanda huo mti Proffesor ana shughuli nyingine nyingi tu za kitaifa ambazo zinamlazimisha ahudhurie akiwa nadhifu.

    Proffesor Maghembe amewahi kuwa Mhadhiri Sokoine Univ, UD, na pia amefanya kazi za kitaalamu nchini Malawi na Nigeria.

    ReplyDelete
  13. Kwani mama Obama alipokuwa anapanda viazi na mboga ikulu ua marekani si ulimwona kavaa gloves. mbona hamkumlalamikia? Haya mambo yanafanyika au yanafanywa na viongozi ili kutoa mwongozo. Ulitaka aje na bukta akae hapo siku nzima?

    ReplyDelete
  14. What?????

    Ukisikia umeona kitu unatamani kutapika kwa hasira ndo vitu kama hivi....

    Ni waziri ok,,,,
    tena wa kilimo ok,,,
    on top ni professor..which means anaweza kuanalaize kuliko sisi
    anatoa mfano wa kulima kwa kuwekewa kitambaa kwenye magoti??
    Why????

    Kweli Tanzania iko gizani.

    ReplyDelete
  15. kumbe kilimo ni uchafu? maana isingekuwa uchafu asingetandika kitambaa chini! Najiandaa kuondoka hapa kijijini Masoko, Tukuyu. Acha tukabanane mjini, siku nikirudi likizo nitawaelimisha wanakijiji jinsi ya kutumia kitambaa ili magoti yao yasiharibike! Waziri katokota km siyo kuchemsha! Hii ni aibu kwa Taifa lenye ndoto ya kuendelea kupitia KILIMO! Waheshimiwa Mawaziri mtambue kuwa Taifa la Tz la Leo si landiyo mzee! Hivyo chochote mfanyacho mtafakari kwanza kwa makini kabla ya kuleta mbele ya wananchi wenye uchungu na Nchi yao.

    ReplyDelete
  16. yani nimechekaaaaa hahahahaaaa
    heee kweli hii ndio "kilimo kwanza" "kilimo uti wa mgongo"

    eee yani waenda kuzindua maswala ya kilimo umevaa frenchi suti na mokasini????ilhali waweza vaa vazi la shamba na ukitoka apo vaa hilo suti lako

    haaaahaha uwiiiiiiii nimeongeza siku ya kuishi

    ReplyDelete
  17. Ujumbe wa bw profesa na wasaidizi wake waliopiga na kutundika picha hii hadharani ni kwamba "haya mambo ya kushika jembe unajua hatukuyazoea, yanatupa shida sana!" jambo ambalo ni sifa chanya kwa wateule wetu wa bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...