Nguza Viking na wanawe watatu wakiwa kizimbani Januari 27, 2005 kusikiliza uamuzi wa Rufaa yao dhidi ya hukumu ya kifungo cha maisha waliyokata kutokana na kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wa shule, lakini Jaji Thomas Mihayo aliyekuwa anaisikiliza aliitupilia mbali.

Leo jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania (Wah. Natalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salim Massati) linakaa kusikiliza rufani ingine ambayo Babu Seya na wanawe wamekata wakiwa wanawakilishwa na Wakili Mabere Marando.

Wasanii hao walituhumiwa kutenda makosa kumi ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo.

Washitakiwa kwa pamoja walidaiwa kutenda makosa yao kati ya Aprili na Oktoba 2003 maeneo ya Sinza kwa Remmy jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. MIMI NAWASHAURI WATOTO WALIOFANYIWA VITENDO VIBAYA NA HAWA SASA WAKIWA WAMEKUA NAO WAFUNGUE KESI ZA MADAI DHIDI YA BABU SEYA NA WANAWE.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na anony wa kwanza kabisa. Ni kweli kwani hilo litasaidia kuclear some doubts kuwa wamebambikiziwa kesi na kigogo flani waliyetembea na demu wake.

    ReplyDelete
  3. ukweli mnaujua ninyi,mungu na hao watoto
    kama hamkufanya makosa mungu awe pamoja nanyi mrudi uraiani lkn kama ni kweli basi muendelee kula msoto wala siwahurumii

    ReplyDelete
  4. hawakubaka wala nini ni uzandiki fulani tuu ebu watolewe jela haiwezekani baba na wanawe woote wabake watoto haiingii akilini iko namna tu wanaokwenda jela sio wote wana hatia wengine wanakwenda kwa ishu za kupakaziwa GOD IS WATCHING!

    ReplyDelete
  5. IT IS VERY TRUE, IT DOESN'T MAKE SENSE AT ALL, FATHER AND HIS THREE SONS TO COMMIT THE SAME ACT, THIS MUST A SET UP. GOD WILL HELP THEM THIS TIME

    ReplyDelete
  6. Mie siamini kabisa eti baba na watoto wote washiriki kile kitendo kwa pamoja?, no no no haiwezekani lzm kuna issue behind, hukumu yao inasikitisha kweli, Mungu yu pamoja nao, na iko siku ukweli utajulikana tu, wamwamini Mungu na kumtumainia yeye pekee, hiyo rufaa tu ni dalili tu tosha za uwepo wake Mungu dhidi yao. nawakumbuka sana katika maombi. poleni wapendwa.

    ReplyDelete
  7. kwa kweli ni ngumu kuingia akilini. baba na watoto watatu wote kufuata vitoto hivyo hivyo! hata kama ni imani za kishirkina basi hizi zimezidi mipaka. kama mmesingiziwa, mwenyezi mungu atakua nanyi. na mhusika atalipwa kwa matendo yake. inauma sana!

    ReplyDelete
  8. NI KWA SABABU ZA KISHIRIKINA TU INAWEZEKANA THE UNTHINKABLE TO HAPPEN, MTU KU-SHARE SEXUAL EXPLOITS NA WATOTO WAKE AU NA WATU WENGINE, LAKINI KATIKA HALI YA KAWAIDA BADO ISSUE YA BABU SEYA NA WATOTO WAKE HAIINGII AKILINI.

    ReplyDelete
  9. Dunia ya sasa kila kitu kinawezekana.....binadamu wanaact kama wanyama.....ila bado sikubaliani na serikali kuwafunga maisha kama hawana ushahidi wa kutosha

    ReplyDelete
  10. Inawezekana kufanya vitendo hivi but hata hukumu isingeenda sawa kwani kama kweli walitenda basi kila mmoja angepewa hukumu tofauti kwa kuwa siaminikuw wote wametenda kosa sawa,pengine mmoja angeambiwa kasaidia,mwengine kafanya hivi but its impossible,huyo kigogo alikua amfunge huyo mwanamke wake na sio watu wa watu au kwa kuwa si watanzania halisi? huu ni uonevu na vipi wale walioua kwa kukusudia si walitolewa na kesi ikahairishwa hadi 2020 lakini mungu amehukumu kwa njia yake

    ReplyDelete
  11. Sasa hivi kuna kesi kama hii US
    mzee na watoto wake wamefanya mombo
    kama hayo , sasa wote wako jela
    kesi bado, you do not do these kind
    of things to children, I hope they rot in prison.

    ReplyDelete
  12. KAMA INAWEZEKANA MKE NA MUME KUSHIRIKIANA KUMBAKA MTOTO WAO WA KUMZAA KWA NINI HILI LISIWEZEKANE? KILA KITU KINAWEZEKANA KATIKA DUNIA YA SASA.

    ReplyDelete
  13. Jamani msiojua ukweli ni kwamba wakati babu Seya na wanawe wanatumbuiza pale Polisi Officers mess, walikuwa wakitembea na wake za wakubwa fulani pamoja na mahawara zao. Sasa, hao wakubwa ambao na wao ni mb mkononi walipoona hivyo wakashikwa na wivu wakaapa kulipa kisasi na kisasi ndiyo hicho jamaa wanasota Segerea kama siyo ukonga au keko. Hao wakubwa wengine ni makamanda wa polisi pia wanajulikana na kama sheria ikifuatwa jamaa watakuwa mtaani soon.

    ReplyDelete
  14. Tatizo Tanzania ya leo wanyonge ndio wanaenda jela lakini hatuoni matajiri na vigogo kukaa jela hata kama wametuhujumu weeeee bado tunacheka nao tunawaita "mkuu" tunapowaona na kwa akili zetu finyu tunaona hawa masikini ambao inawezekana kabisa wamebambikiwa kesi wakae tu huko jela mpaka kufa... Wizi Mtupu! Kama wewe na ufukara wako ungekuwa ktk viatu vya wakina Babu Seya ndio ungejua Tanzania zaidi ya uijuavyo. Ukiwa na uwezo whether ni pesa au nafasi basi full bata ndani ya bongo si unajua tena haya ni magonjwa tuliyoyalea wenyewe tunapenda sana shortcuts na kuogopana ishu kibao haziendi sawa sio hawa tu... Je wale polisi walioua kabisa na kupeleka maiti kituo cha polisi kusema wameua majambazi na bado wameshinda kesi! Hivi kweli unaua unapeleka polisi maiti tatu sijui eti hawa ni majambazi tumepambana nao halafu inakuja kujulikana wazi wale waliouawa ni wafanya biashara na wala hawakuwa na silaha zozote halafu wale waliowaua na walisema wenyewe kwa vichwa vyao na mkuu wao kutamba ktk TV eti wameachiwa huru jamani sijasoma sheria(law) lakini inabidi labda nikasome ili nijui jinsi ya kujiweka sawa pale janga litakapotokea na mimi nitumie hivyo vifungu vya sheria kutoka maana haiingii kabisa akilini...
    Sasa hivi tunaconcentrate na babu Seya weeee wakati haki zetu za msingi zinaenda na maji watanzania tubadilike... Hivi hakuna wanaume kama Nyerere? :-) Namzimia sana yule jamaa maana alikuwa anaona mbali kitu ambacho sasa hivi hakuna.

    ReplyDelete
  15. Anony Tue Dec 01, 09:11:00 AM udaku unaujua. Ila hukufuatilia ushahidi wa wale watoto wadogo around 9yrs wakisema "walituingiza madudu yao mdomoni na wakatuambia tumeze maziwa yanayotoka"

    Wale watoto ni wengi sana na wadogo kiasi kwamba hawawezi kutoogopa kusimama mahakamani kutoa ushahidi hata kama wamefundishwa na FBI ama KGB

    Acha ushabiki. Nchi haiendeshwi kisheria ila mizuka na mawazo ya watu kama ninyi.

    Vyombo vya sheria vimewekwa na mungu na tunaamini wanafanya haki na kama wanadanganya ama mtu amedanganya then atahukumiwa yeye.

    Kwa sasa tunahitaji adhabu kali kwa makosa kama haya ili kukomesha uovu. Mamia ya vijana wa kiume wamegeuzwa gays kwa kufanyiwa uharamia na watu wazima, ona mashuleni hakuna std 7 anayemaliza bikra kutokana na walimu kuwafanyia unyama, ona makazini mabosi wanavyowafanyia wake zetu

    Ukiwa huna mtoto na hujui mabaya then kuwa mtetea maovu

    ReplyDelete
  16. jamani cku ya mwisho wataenda wengi motoni, wamewapa watu wa watu kesi ya uongo, sasa wanajifanya kuwatoa kwa dhumuni ya kampeni hamna lolote wizi tu,

    N wa M

    ReplyDelete
  17. KAMA NI HIVYO ISOMWE ALIBADILI TUONE KITAANGUKIA WAPI FULL STOP!!

    ReplyDelete
  18. mIMI KAMA MAMA NAOGOPA KUTOKUAMINI KAMA KWELI HWAJAFANYA HAYO MAMBO, MAANA KAMA NI KWELI WALIWATENDEA WATOTO WADOGO MAMBO YA AJABU KWA USHIRIKINA AU LA, SITAJISIKIA VUZURI KUWA NIMEWAONEA HURUMA BURE BURE MAANA INGEWEZA KUWA HATA MTOTO WANGU.
    Na dunia ya siku hizi kuna mambo ya kila aina. Kuna wazazi wanabaka watoto wao wa kuwazaa na hii haikuanza jana wala juzi. Kuna watu wanashirikiana kubaka vitoto vya miezi sita, pia haikuanza jana wala juzi.
    Lakini pia haileti maana na ni ngumu kuamini kwamba baba na watoto wake wote watatu wanaweza kwenda wafanya vitu vya ajabu watoto wadogo.
    Kama wamefanya basi I pray to god waozee jela huko huko na magonjwa.
    Kama hawakufanya wamesingiziwa basi mungu awaepushie na lets hope waatacha kutembea na wake za watu. FUNDISHO.

    ReplyDelete
  19. NIMEIPENDA YA ALBADILI !

    ReplyDelete
  20. itakuwa ishasomwa albadil na ndo imeangukia huko kwamba wasote jela maisha. Ukweli Mung na wahusika wanao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...