Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Tandahimba, Mama Julia Kariati, akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shillingi 2.5m/- kwa ajili ya ununuzi wa madawati ya shule hiyo. Makabidhiano ya msaada huo kutoka benki ya NMB yalifanyika wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB Tandahimba mkoani Mtwara
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tandahimba, bibi Julia kariati, akiwa na wafanyakazi waNMB tawi la tandahimba katika picha ya pamoja baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya shillingi 2.5m/- kama msaada toka benki ya NMB kwa ajili ya ununuzi wa madawati ya shule hiyo


hizo hela zinunulie madawati kweli hakuna kukata panga ni za madawati tuuuu na hivi xmas inanyemelea hayo madawati hayo anyway
ReplyDeleteHela kama hizo zingepitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)zingeweza kudhibitiwa na wale TEA wangehakikisha madawadi yananunuliwa. Kuwapa shule hela moja kwa moja sio sawa kabisa pia NMB hawarudi tena kuhakikisha kama kweli hayo madawati yamenunuliwa. Hiyo kazi ingefanywa vizuri na Tanzania Education Authority (TEA).
ReplyDelete