wadau mnaolia ati bongo kuna foleni, je hii tuiiteje??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Chicago asubuhi na jioni foleni ni mtindo mmoja hivyo sishangai kabisa kuona hiyo foleni japo wapo organized. Je hiyo ni nchi gani tupeane mawazo?

    ReplyDelete
  2. Du hiyo nchi wanaadabu kwel kama nyuki vile,ingekua bongo ni soo daladala zingekula wing kama kawa au wanaita kutanua yaan ingukua vurugu tupu.

    ReplyDelete
  3. Unajua madereva wakiwamo wamiliki wa magari baadhi yao hawana subira wawapo barabarani. Mimi nionavyo foleni za Dar ni typical ya majiji yote duniani. Foleni haikwepeki mradi inamove. Foleni inakuwa kero pale ambapo magari yamekuwa yamesimama hayaendi. Otherwise foleni za dar magari yake yanatembea. No sweat man Kama hutaki foleni tembea kwa miguu.

    ReplyDelete
  4. Nafikiri hapo sio traffic jam ya kila siku. Inawezekana kuwa hii ni jam wakati watu wanakimbia New Orleans wakati wa Hurricane ya Katerina. Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. bongo inaitwa poleni kutokana na kutokwenda kwa hiyo foleni.lkn kimamtoni inaitwa foleni pamoja na kuwa na foleni lkn ngoma inogile yaani inakwenda.

    ReplyDelete
  6. hiyo siyo Mrorogoro road maeneo ya Kimara kwa msuguri ?? kweli bongo tambarare

    ReplyDelete
  7. hiyo inaitwa bumper to bumper,asubuhi na jioni ukitika mzigoni.train an trams oyeee.

    ReplyDelete
  8. tuite lifoleni

    ReplyDelete
  9. unajua kuna foleni ila gari zinatembea,
    sasa msituwekee tu picha bila maelezo
    je hizi zimesimama au zinatembea, bongo gari hazitembei bwana acheni utani kabisa. pili uliyeweka hii picha mbona iko advanced sana njia nane kasoro na inavyoonshe zinapishana yaani zimetengwa zinazokwenda na zinazorudi.
    in short naona haina uharisia na bongo!

    ReplyDelete
  10. hii hapo ni sumatra, indonesia. hii foleni imenizingua mpaka imenibidi nibadilishe kazi na waindonesia wengi wanasumbuliwa na foleni hii. In fact hii foleni imeshasababisha waziri wao wa miundombinu kujiuzuru kwa kushindwa kutafuta suluhisho la kudumu la hii foleni

    ReplyDelete
  11. kutuonesha foleni ya namna hiyo aina maani sisi ni afadhali.kwanza uwezi jua je kulikuwa na ajari au road maintenance hila mtazamo wangu mimi ni tofauti ni juu ya hiyo picture,ningesifia hiyo barabara ni first class laiti kama bongo ingekuwa kama hiyo nazani kusingekuwa na foleni

    ReplyDelete
  12. wee mdau wa chikago nilikuja chikago sijaona barabara mbovu kama za chikago hata hiyo traffic itakalia wapi?

    ReplyDelete
  13. Hiyo ni Reading...United Kingdom!!!

    ReplyDelete
  14. Mambo ya LA hayo sema hapo LA DK 30 Ishakwisha Eneo Moja Dar-es-salaam Hapa mtu unakaa Masaa mawili. Ndosi

    ReplyDelete
  15. Nchi ambayo ina barabara zake pana sana na mult lanes ni Marekani. Hata natural vegetation inaonyesha ni nchi ya marekani. New York State, New Jersey State, Maryland state, Illinois State na Califonia state foleni kama hii ni mtindo mmoja hasa kipindi cha Thanks Giving, X-mass na Mwaka mpya wanapoadhimisha kivyao.
    Nakumbuka siku niliendesha gari kwa saa tatu umbali wa maili 20 kwenye barabara ya Garden State parkway nikitokea kazini wakati watu wakiwahi kuungana na familia zao kula Thanks Giving holiday miaka mitano iliyopita

    ReplyDelete
  16. for the first time nimesikia hii thanksgiving day hapa china...ni nini hasa?nini kinafanyika kwa sababu gani?
    kuhusu lifoleni naona ni tatizo la kidunia....kila sehemu kuna foleni, na kila sehemu kwa portion yake...kwa magari machache ya dar na barabara mbaya na finyu za dar foleni ni sawa tu na hii....uzuri mwingine hii hakuna kutanua/kupita pembeni kama daladala za tz.

    ReplyDelete
  17. Hii picha si halisi kwa barabara kubwa namna hiyo huwezi kukuta foleni za namna moja kila upande! Najua waosha vinywa mtakataa lakini busara ya kawaida inaonyesha hivyo. Mmoja kasema asubuhi na jioni ni kweli lakini siyo pande zote. Mwingine anasema Katrina hiyo ingeeleweka sasa hapo hao wanaoelekea upande wa Katrina wanajitoa mhanga?

    ReplyDelete
  18. Thanksgiving day inajieleza. Ni siku ya kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa, marafiki, Mungu, nk.

    Ni siku inayo adhimishwa kwa kula Turkey (Bata mzinga).

    ReplyDelete
  19. hi wapendwa hii picha sio mbaya kama wenzangu waliotangulia kucomment kikubwa ni kwamba kwa sisi wabongo cha kujifunza pale ni kubadili bara bara zetu na kuwa za kisasa zaidi.kwani hata Uk tuna foleni lakin magari yanatembea sio kama bongo ndugu yangu, bongo magari sio meng kama ukifananisha na nchi nyingne zilizoendelea na zinazoendelea. Kikubwa kwetu tuige taswira hiyo kwa kupigania haki zetu serikalini so then wajenge barabara.
    yangu ndio hayo

    ReplyDelete
  20. UKITAKA ONA BARABARA PANA SAFI NENDA GERMANY NA CHINA, BARABARA NYINGI ZA NCHI ZA ULAYA NA AMRICA NI ZA MUDA MREFU NA NI MBOVU KWA MFANO ZA UK NI MBOVU AJABU KILA SIKU VILAKA TU NA SI LAINI NI MATUTATUTA TU UKO KWENYE GARI UNACHEZA SINDIMBA. HATA SAUDI ARABIA ZA KWAO NI BOMBA UKILINGANISHA NA UK. IT IS AN OLD COUNTRY WITH OLD FASHIONED ROADS.

    ReplyDelete
  21. angalieni vizuri kuna mshkaji anataka kuvuka barabara apo

    ReplyDelete
  22. Watu wajibu swali:

    Hii iitwe foleni ambapo magari yanasimama na kuondoka ndani ya muda mfupi.

    ReplyDelete
  23. hivi wadau msululu huu wa magari inakuwaje ukiharibikiwa na gari, sababu sioni hata hard shoulder.

    ReplyDelete
  24. Jamani tusijipe moyo kwa kujifananisha na hiyo foleni ki uongo uongo.
    1.inaonesha kuna msululu na sio foleni na physics yangu ndogo tells me gari ziko kwenye motion hapo.
    2.wenzetu wamejaribu kutafuta solution,at least barabara nyingi.sie hadi leo hatuna barabara yenye more than 4 ways.eti tupo kare ya 21
    3.ingekua kwetu hapo ungeona hiace imechomekea the wrong saiti,bajaji,magari yana-keep left
    na right at the same time
    Na mengineyo

    ReplyDelete
  25. hiyo ni copy and paste hiyo. cheki magari yanafanana ya mbele na nyuma yake kwa wingi. mtu huyu alitulia kuifanya kazi hii; lakini bongo ni orijino.

    ReplyDelete
  26. Aisee, bonge la foleni. . lakini hii picha mbona naona kama kuna sehemu mtu katuchezea akili ili tuone hali ni mbaya kuliko hali halisi ya huko??!! Look carefull ktk barabara ya juu upande wa kulia. Kuna lorry fulani na pembeni yake kuna sehemu identical!! Mambo ya cut n paste hayo. . . look at the details. . . si ya kweli hii picha.

    ReplyDelete
  27. Candid ScopeNovember 30, 2009

    Mheshimiwa sana Kaka Michuzi, nadhani tukiangalia sana suala la uhaba wa ardhi kwa nchi za ulaya ni ngumu kupanua barabara.Hata baadhi ya nchi za bara la asia zinaupungufu wa ardhi ya wazi kama China kwa vile sehemu kubwa kwenye lundo la mlima everest hakukaliki.
    Nchi ya Tanzania na ardhi kubwa isiyokaliwa bado na watu au kutumiwa kiwa shughuli za kilimo. Hali kadhalika Marekani huwezi amini kuona mapori mnakubwa yasiyotumika bado hivyo kuwa na uhuru mkubwa wa kutandika mkeka wa lami kama uonavyo.
    Nchi nyingi kama ulaya bado zinatumia round about ambapo mnarekani kila mji imewekwa round moja tu pembeni kabisa huko kwa ajili ya kumbukumbu ya mambo ya kale (musium). Ramp tu ndo zinaunganisha Highway hakuna traffic light Highway. Kujaribu kujenga bongo iwe tambarare hivyo sawa na kufata kunya kwa tembo.
    Muhimu bongo kuongeza barabara nyingi zaidi zinazopitika wakati wote hakutakuwa na folleni tunayofikiria kwani magari yako wapi?

    ReplyDelete
  28. utamu ni kuwa huku foleni huwa zinatembea siyo bongo mbuzi kagoma

    ReplyDelete
  29. HII PHOTO NI MAREKANI KWANI NDO INCHI PEKEE AMBAYO MAGARI YANA-KEEP RIGHT,NAUKIANGALIA KWA MAKINI VEGETATION INAONYESHA KWAMBA HII NI CALIFORNIA.CALIFORNIA INAONGOZA KWA INFRASTRUCTURE MAREKANI.WABONGO HII NDO INATWA FREE WAY,HAKUNA TRAFIC LIGHTS HUMO.MAMBO YA IN-RAMP NA EXIT RAMP TU

    ReplyDelete
  30. Gari ziko kwenye motion kivipi?? Foleni ni foleni tu jamani. Kuna wabongo hapa tumewahi kuwa nje ya TZ pia foleni huwa zipo... hasa asubuhi na jioni. Haijalishi zimesababishwa na matengenezo au la foleni ni foleni tu. Hata foleni ya hapa bongo nayo inasababishwa na vitu mbali mbali ina maana hivyo vitu vikipatiwa ufumbuzi foleni itapungua. Sasa watu hapa wana tetea foleni za huko nje... sijui inamaanisha nini. Swala ni yeyote mwenye nafasi ya kufanya mabadiliko hapa kwetu ajitahidi kuitumia nafasi hio vizuri kwa faida ya wote la sivyo tutabaki kutetea nchi zingine hata kwa vitu "-ve".

    ReplyDelete
  31. Ni parking kaka

    ReplyDelete
  32. hiyo ni yard ya kuuzia magari pale Sinza

    ReplyDelete
  33. Hapo ni Manzese ah no i mean Buguruni ahh yaani mbagala ndo kuna road ka hizo. hii si foleni bali kibaka kazuia road baada ya kumkwapulia mshikaji kamobitel kake.

    Bye
    Bp

    ReplyDelete
  34. Hiyo si picha halisi ni ya kutengeneza Mambo ya fhoto shop xgq200 Na alie itengeneza kakosea jambo moja gari za rangi ya bluu zimekuwa nyingi zaidi kiasi lazima kwa wataalam watajua tu kwamba ni image ya bandia. Mdau Majuto -USWIDI

    ReplyDelete
  35. Anon 07:08 PM anakahoja ka msingi ukiangalia kwa makini unagundua magari yanajirudia kufanana kwenye lanes tofauti....Huu mchezo wa kuigiza huu...watoto wa kiswahili huwa tunauita kanyaboya....

    ReplyDelete
  36. Misaada Raisi K unayoomba day and night tengeneza barabara bwana na siyo kujilimbikizia na barabara zimejaaa mshimo, magari hayaendi unasimaa for 2hrs sehemu ya kwenda 30minutes, pia madereva kuweni na adabu mambo ya kujipachika na kupiga bao acheni mnasababisha barabara kujaa mashimo na kukosa kutoka ukishajiegesha ubavu halaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...