Na Veronica Kazimoto
MAELEZO, ARUSHA.
Serikali inatarajia kujenga kituo kipya cha kimataifa cha mikutano mjini Arusha kinacho tarajia kugharimu kiasi ha shilingi bilioni 100.
Akitoa mada kwa maofisa habari, elimu na mawasiliano wa wizara, taasisi, idara zinazojitegemea na wakala wa serikali wanaoendelea na mkutano wao wa tano mjini Arusha mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) Elishilia Kaaya amesema mipango ya ujenzi wa kituo hicho iko mbioni na kufafanua kuwa hatua za awali zitakazowezesha ujenzi wa kituo hicho zimekwisha anza.
Bw. Kaaya amesema AICC imetenga eneo la wazi wanalomiliki eneo la Kijenge-Olorien Halmshauri ya Arusha mjini. Kaongezea kuwa Mwaka 2007 AICC ilifanya utafiti kuhusu uanzishwaji wa kituo kipya cha mikutano cha kimataifa kupitia kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Dar es saalam ambapo utafiti huo ulihusisha mikoa mitatu.
“katika utafiti huo ilipendekezwa miji mitatu ambayo ni Dar es salaam, Zanzibar na Arusha ambapo utafiti ulionesha kuwa mji unaopaswa kujengwa kituo cha mikutano cha kimataifa ni Arusha.” Amebainisha bwana Kaaya.
Bwana Kaaya amezitaja sababu zilizopelekea kuchaguliwa kwa mji wa Arusha kujengwa kituo hicho cha mikutano cha Kimataifa kuwa ni karibu na vivutio vingi vya utalii vyenye umaarufu mkubwa duniani visivyopungua saba.
Akivitaja vivutio hivyo amesema kuwa ni hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA), mbuga ya wanyama ya Arusha, mbuga ya wanyama ya Serengeti, mbuga ya wanyama ya Tarangire, mbuga ya wanyama Ngorongoro na ziwa Mnyara.
Sababu nyingine ni uzoefu wa AICC kuendesha mikutano mbalimbali ya kimataifa kwa muda mrefu kitu ambacho kimepelekea mji wa Arusha kuwa maarufu katika nchi mbalimbali duniani.
“AICC imekuwa kwenye biashara hii ya uendeshaji wa mikutano kwa miaka 31 sasa hivyo ina uzoefu wa kutosha katika kuendesha mikutano ya kimataifa kutoka nchi mbalimbali.” ameongeza bwana Kaaya.
Ujenzi wa kituo hicho kipya itapelekea Tanzania kuwa na vituo vikubwa viwili vy Mikutano vya kimataifa hii itaisaidia nchi hii kukabiliana na ushindani uliopo katika nchi za Afrika Mashariki.

KWA NINI WAJENGE ARUSHA TU, MTWARA JE????? NA NYINYI NTWARA NG'OO NTUTAKI NINI, WATANSANIA PIA, MAENDELEO JEEE!! NYINYI TU
ReplyDeleteMy friend Elishilia Kaaya naona mambo yako.
ReplyDeleteNaona jinsi unavyotumia elimu yako ya finance kuweka mambo sawa.
Karibu nitakuja huko kwa ajili ya vekesheni na nitapita AICC kukusalimu na kukupongeza kwa kazi nzuri unayofanya AICC.
HUU SI MGAWANYO WA RASILIMALI, KWA NINI WASIJENGE MTWARA AU LINDI?KAMA VIVUTIO VYA UTALII NI WANYAMA TU BASI TUNAYO SELOUS GAME RESERVE, LAKINI SI HIVYO TU MIKOA HII INA HISTORIA KUBWA INAYOWEZA KUWA VIVUTIO PIA TUSIWE WATU WA KUKARIRI TU ETI KILA KITU MOSHI NA ARUSHA!IPO KILWA,MISIKITI NA MAJENGO YA KALE, TUNA UWANJA WA NDEGE MTWARA UPO VIZURI TU, FUKWE NZURI ZILIZO SAFI NA HATA UMEME WETU WA BEI POA NA UHAKIKA (WA GESI) SASA HAYA MAMBO YA KUKARIRI KARIRI YANATOKA WAPI, MTAFITI GANI HUYU TOKA UDSM?.
ReplyDeleteMDAU MT
sasa wewe anonymous wa hapo juu unataka wajenge mtwara,mtwara kuna Hotel yoyote ya kitalii kwel? au unataka watu wafanye mkutano mtwara walale Dar,miundo mbinu mibovu,usafiri hakuna au unataka wakat ukiwapo mkutano huko mtwara magar ya kutembelea yasafirishwe kutoka Dar,hali ya hewa haieleweki shida tu.sanasana unaongeza matatizo juu ya matatizo.
ReplyDelete