Belinda Mlingwa alikuwa MC kwenye hafla hiyo maalumu kwa watoto na wazazi wao katika ukumbi wa Diamond hall jijini Dar wikiendi hii, ambapo wabuni mitindo wakubwa walipanda stejini na kuonesha vipaji vyao vya kusaka rhumba katika onesho la hisani kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu lililoandaliwa na Tanzania Mitindo House.
mbuni mitindo farha sultani alicheza midundo ya kihindi akiwa na madansa wa THT
mbuni mitindo zamda george akicheza na msanii hemedi na wana THT
ally rhemtullah alifunika kwa kujimwayamwaya kama fari ipupa kwa kibao cha 'makanja'
mbuni mitindo anayekuja juu francisca a.k.a franko (kulia) alitia fora sana na mchiriku
mustafa hassanali na khadija mwanamboka walitupeleka bollywood
mama wa mitindo asia idarous-khamsin alifanya kweli na ngoma ya 'bomu' toka zenji







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kudoz kwa wanamitindo na waandaaji!

    ReplyDelete
  2. mustaffa ametumia nini? mbona amepungua kiasi hicho? atuambie tunataka kupungu. hata hivyo mwambie inatosha. asipungue zaidi

    ReplyDelete
  3. Kweli, hivi Mustafa amekuwa na programu gani effective kiasi hicho kwa sababu muda ni mfupi sana kufikia hapo alipo. Michu, tunaomba jamaa atusaidie kujua alivyofanya siye tuliobakia. Mimi nafanya mazoezi kiasi asubuhi, nakula mlo mmoja kwa siku, nimepunguza sana ulaji wa sukari na sukari related foods lakini uzito haupungui wala kuongezeka. Nataka nipige chini 10 kilos at least.

    Ally kajitahidi sana kutoka kama Fari Ipupa natamani ningekuwepo nione huo mselebuko. Well done guys!!

    ReplyDelete
  4. Haha, those guys had fun. Sisi huku tunabeba maboxi tu, life is not fair.

    ReplyDelete
  5. itanichukua muda kuzoea umbo la Mustapha hasanali kwani kila nikiangalia picha hizi akiwa amepungua nasikia kulia jamani amepungua kupita kiasi napenda kupungua lakini hapana imezidi kama ana sumbuliwa na moyo au sukari kha!

    ReplyDelete
  6. Kudoz Tanzania Mitindo House! What you are doing for the kids is wonderful and I am sure they had a great time. Mwenyezi Mungu awazidishie muendelee na moyo huu na awaongezee pale mlipopungukiwa ili tuweze kuendelea kuwasaidia watoto wetu hawa. God Bless

    ReplyDelete
  7. Haiwezekani mtu apungue ghafla hivyo. Hiyo ni opereshen tu. Kajiona unene umezidi, akakwea pipa Sauz kufanyiwa opereshen.

    ReplyDelete
  8. Mh! Wewe Franko mchiriku toka lini ukaujua. Ila nakuaminia. Unakuja juu kwa kasi unanitisha! Kazi nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...