wananchi kijiji cha Mkata mkoani Tanga wakiangalia

basi la Meridian lililogongana na lori jioni hii sehemu hizo
Ankal Nanihii,
Mie ndo natoka vekesheni Roitoktok huko Kenya mpakani mwa Tanzania, nimepita njia ya Tarakea, yaani haifai. Baadaye kidogo ntakutumia taswira za huko.
Hapo juu ni ajali nimeikuta sehemu za Mkata mkoa wa Tanga ambapo basi la Meridian limegongana na lori. Dereva wa Meridian kajitahidi sana kuokoa maisha ya abiria kwani lori lilihama njia na dereva wa Meridian akasave kidogo kwa kuingia kwenye .
Hadi naondoka saa kumi leo hamna aliyekufa ila majeruhi walikuwa kibao na polisi walikuwa hawajafika.

Mdau Isaya Philip

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hivi Kaka Michuzi kwa nini kila MWISHO WA MWAKA kunakuwaga na MAAJALI ajali ya kuua watu kwa wingi namna hii jamani?

    Kuna mdau yoyote mwenye sababu ya kitaalamu alitolee ufafanuzi hili?

    Ndo mana me mwenzenu huwaga naogopaga sana kusafiri safiri mwishoni mwa mwaka namna hii

    ReplyDelete
  2. SABABU ZA KISAYANSI NI NGUMU KUZIPATA LAKINI KUNA SABABU ZA JADI NAZO NI KWAMBA MUNGU ANAVUNA MAZAO YAKE, PIA NI NATURE KUBALANCE IDADI YA WATU DUNIANI. DUNIA INAPOZUNGUKA KILA INAPOPITA INASABABU ZAKE KAMA VILE MVUA, JUA KALI, UPEPO, BARAFU, KUKAUSHA MITI WAKATI WA KIANGAZI/WINTER, I THINK THERE IS SOMETHING TO DO WITH EARTH RORATION/REVOLUTION.

    ReplyDelete
  3. MSHIRIKINA,10;47;00 Kama siku yako imefika,hata kama hutaki kusafiri utaangukiwa na dali la nyumba.
    Mimi,uk

    ReplyDelete
  4. Hivi kwanini bongo nao wasitengeneze barabara za kupita malori na za kupita mabasi ili kupunguza ajali??ni hayo tu asante

    ReplyDelete
  5. michuzi
    Nilikua huko jana ndo nimerudi hiyo barabara anayoisema mdau hapo ya kutoka tarakea hadi marangu ni kwa ujumla ni uzembe wa mkandarasi kuna sehemu tatu ambazo zinasumbua wananchi hizo sehemu zingejazwa kifusi zikashindiliwa wala kuzinge kua na tatizo sehemu zenyewe si zaidi ya meter 20 kila moja. Ila mkandarasi anapenda kuona watu wanataabika ila ukipita hizo sehemu njia yote ni mkeka tunashukuru mungu walau wa rombo tutapata lami mwakani christmas na mwaka mpya mambo mswano kuteleza hadi rombo. Mi nilipita saa 12.30 asubuhi hizo sehemu korofi nilikuta mabasi yamekwama lakini kwa kua gari yangu ndogo na ni front wheel drive ilikua kama kumsukuma mlevi

    Mdau Bongo forever

    ReplyDelete
  6. JAMANI SABABU NI KWAMBA WASAFIRI WANAKUWA WEEENGI KULIKO KIPINDO CHOCHOTE CHA MWAKA HIVYO HATA VIPOFU NAO WANAENDESHA SIO KINGINE

    ReplyDelete
  7. kweli bongo tambarare mijitu yote imefika hamna police.

    ReplyDelete
  8. @Anony - Tue Dec 29, 08:01:00 AM

    Wewe nani amekwambia kwamba FWD ndo kiboko ya matope na barabara mbovu?? Itakuwaje hizo tairi za mbele zikikwama? Wanna go for the Best? Get urself an AWD Subaru Forester with Turbo.
    Poleni Rombians...ongeeni fresh na mzee Pesa2 atengeneze hiyo barabara.

    ReplyDelete
  9. Mdau MlokoleDecember 29, 2009

    Ndugu zangu maelezo yanahitaji uwe na elimu ya mambo ya ulimwengu wa Roho. Kwenye ulimwengu huo kuna falme na mamlaka mbili. Moja ya Mungu (Nuru) na nyingine ya shetani au giza. Barabara hiyo imeshamwaga damu nyingi sana za watu kutokana na michezo ya kishirikina. Kutoka Chalinze kuelekea Segera halafu to tanga na to arusha, njia hiyo inayo misukulue mingi sana. Wanaoimiliki na wao wanajua huu ni mwisho wa mwaka. Kwa hiyo pamoja na sisi tunashereheka na mwisho wa mwaka na wao wanapenda misukule yao nayo isherehekee kwa kupata kinywaji cha damu. Hasa ukichukulia barabara hiyo wanapita watu wengi sana hata takribani laki moja. Niambie lita ngapi hizo za damu. Kwa hiyo kinachofanyika kila gari ikipita wao wanaipundua kwa kuisukuma au kutoboa tairi na ukucha. Katika ulimwegu wao wa roho wa giza macho yao ni tofauti na yetu. Gari wanaiona kama kibox cha kibiriti tu kwa hiyo kuipindua ni jambo rahisi sana.

    Ukitaka msafiri bila ya usumbufu mntakiwa mfanye maombi na muifunike hiyo gari yenu na nyinyi wenyewe na damu ya Yesu. Hapo mtapita salama. Ikatokea ndani ya basi lenu hilo halifanyika lakini kuna abiria ambao wameomba na wamejifunika na damu ya Yesu basi wao hupona.

    Kinachotakiwa na wachunagji wote na mapadri na wanmaombi wapite hiyo njia na waifanyie annointing ya damu ya Yesu hapo ndipo salama itapatikana. Short of that tutaendelea kuperish Ndugu zangu. Hiyo ndiyo habari yenyewe take it or leave it. Mimi nimesema.

    ReplyDelete
  10. mimi ni mkazi wa ROmbo jamani huwa tunapata taabu sana wakati wa mvua hiyo barabara wameitelekeza miaka nenda Rudi sijui hii sekrikali yetu inafanya nini. halafu jamani huko ulikosema sio Roitoktok bali ni Loitoktok.

    ReplyDelete
  11. pamoja na mwisho wa mwaka madereva wa malori ni full bangi huwa wanaspeed na wanakaa katikati naongelea malori ya mchanga na mafuso yani vichwa vya hao madereva ni full mjani hawajaligi kabisaa wana makusudi sana

    ReplyDelete
  12. Mji unaitwa Loitoktok sio Roitoktok!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...