Home
Unlabelled
bichi la wenzetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
KWa mfano china viongozi wanaopatikana wamefanya makosa ya rushwa/ufisadi adhabu zao ni kifo tu. Sasa Tanzania bila kuchukua mkondo huo tutaendelea kuangalia beach za wenzetu na mambo mengineyo mazuri ya wenzetu kama hivi tu! Hakuna kuoneana aibu kwenye ishu ya mapata au ufanisi wa kazi za serikali, full stop!
ReplyDeleteMimi nahesabu kuwa jiji la Dar ni kama tumeshaliharibu. Mkoloni inawezekana alikuwa mtu mbaya lakini angalau aliheshimu sheria za mipango miji tofauti na sis tulivyofanya.
ReplyDeleteNasema hivyo kwa sababu tumeweza kufuru kwa kugawa Beach Plots zote Dar kwa watu binafsi. Matokeo ni kwamba wana-Dar hawana Access to the Beach isipokuwa labda waende kwenye mahoteli ya kitalii au waende zile sehemu chache, kama Coco, ambazo ziliponyeshwa kwa kuweka barabara ya Toure kukinga kugeuzwa plots.
Cha kusikitisha ni kwamba sasa hivi hata sehemu zilizokuwa zimeokolewa, zinaharibiwa. Mfano ni pale kwenye ghati ya meli za kuenda Zanzibar. Kila kukicha unakuta inaoteshwa kajengo kaajabu ka kuuzia ticket za maboti - matokeo yake ni vigumu kwa mtu kuona bahari hata akiwa St Joseph, karibu kabisa na hapo.
Cha kufanya ni kuwawajibisha viongozi wote wasio waadilifu. Kwani hatuwajui?? Tunawajua ila tunaoneana haya. Tukipewa sukari tunasahau ubovu wote, matokeo tunasimama dede kuwakampenia ili wapate kula tena. Let us now be serious .... kwa kuchapa kazi kwa bidii na kwa uadilifu, tunaweza kufikia hali hii. tatizo hata wale wachache wenye upeo wa kufanya mazuri hatuwapi nafasi kwa kuwa hawana uwezo wa kifedha ili kupata nafasi katika nafasi za kuweza kuonyesha ujuzi wao. Mwekezaji Mtazania hapati nafasi kwa kuwa ana rangi tii. Asante Bro Mithupu kwa blog hii ya jamii maana tunaosha macho kuyaona ya watu huko kulikopambazuka mapema kwa uadilifu.
ReplyDeletesa mbona hiyo beach me naiona ya kawaida kabisa, sema tu iko ktk location nzuri na inaonekana ni mjini kabisa na inafanyiwa usafi tu, haina tofauti na beach ya kisiwa cha bongoyo Dar Es Salaam,,sa waTZ tufike mahali tuache lawama na otherwise tuwe tuna pendekeza zaidi nini kifanyike, kwani Tanzania si ya hao vigogo tu, ni ya wote hata wewe ambaye waweza kwa namna 1 au nyingine ukawa kiongozi au kigogo....ni haya tu...
ReplyDeleteyaani hapo hakuna masinia ya maandazi wala mihogo na samaki, very clean. tz ovyo
ReplyDeletemichuzi mi nafikiri ushauri wetu unaweza kuwa sawa na kumpigia mbuzi kitaa tu lkn ngoja mi nitoe unajua sheria za jiji au miji yetu tatizo kubwa azifuatwina jamii pia viongozi waliopewa mamlaka zaidi ni viongozi wa kisiasa hasa kwenye halmashauri zetu ni waheshimiwa madiwani na tatizo kubwa la hawa watu ni elimu tu sasa mi nashauri vijana tujitaidi tugombanie hata huo udiwani ingawa unaonekana sio dili sana ndio hizi beach,barabara,usafi,mipango miji nk vinaweza kuoneka hila tukiwaachia hawa non educated is very sensitive issue tutaendelea kuwa maskini wa mawazo tu kwavile hawa watu awaelewi hata kidogo unaweza ukawa na vision mzuri afisa mipango miji hila ukipeleka huko kwa hawa jamaa awakipitishi kwahiyo utaalamu wako uaishia hewani hila unalaumiwa tu mi sidhani kuwa maafisa mipango miji aliye ajiriwa kuanzia uhuru mpaka leo kwamba awapendi jiji letu liwe safi au linapendeza na madegree yao
ReplyDeletemi naomba sana vijana tuwe committed na nchi yetu
Rushwa,rushwa, rushwa na kutokuwa na Viongozi waadilifu ndio chanzo cha maozo yote.
ReplyDeleteNchi yetu hata Rais wetu viongozi wenzake hawamuogopi wala kumheshimu wanafanya wanavyojua wao.Kama tungekuwa na kiongozi kama Hayati Sokoine mapuuza kama hayo yasingekuwepo,Sheria singefatwa na jiji lingekuwa safi.Tatizo kila kiongozi yeye anajua kuliko sheria za nchi.Wenzetu hakuna kiongozi aliyejuu ya sheria, sheria ni moja na atakayepinda sheria ni mahakamani tu na sio kubembelezana huyu mtoto wa Rais,waziri nk ni ndani tu.
Law should be applied for each and everyone,no matter how big you are!
Mjusi
tusahau kitu kama hicho hapa kwetu TZ, viongozi wa kisiasa wameshajisahau sana. itachukua muda mrefu kuja kuona mabadiliko ya kweli, mpaka adabu itakapopatikana, na adabu haiji ivi ivi.... mpaka tuchapane na tutawanye kile tulichokikusanya ndipo watu watakapokuwa na heshima na mali za umma na viongozi kuwa ni watumishi wa wananchi... labda tutaweza kuona mandhari kama hizo..
ReplyDeletemameneja wakiwa wazungu tu lazima pawe namna hiyo pale coco bich panaweza kuwa hivyo lakini yule mzawa anayemiliki pale hajali mazingira ya pale pako lokoooooooo ovyo sana angepachukua mzungu mtashangaa !!! ndo hivyo watu wanajua kupiga tu kelele mali zetu wamepewa wazungu wakipewa ndo wanaua band kabisa acheni tu tubaki hukuhuku tuzoee ustaarabu
ReplyDeleteHii picha inanikumbusha Luanda, Angola ambako kwa sasa serikali ya Angola kwa ushirikiana na UNICEF inapanua kwa kumwaga vifusi vya mchanga. Kwa staili hiyo hiyo hata coco beach, ocean road na msasani tunaweza kufanywa hivyo, niviongozi tu kuandika proposal nzuri kwa haya mashirika...but i worried kidogo maana hata kwenye hizo fukwe haturuhusiwi kwenda (eg. kuliwekwa bango kabisa pale ocean road) hata ikipanuliwa nadhani itabaki kuwa fashion tu...Inashangaza mji wa Dar ambao hauna hata sehemu za kupumzika tunashindwa kufanya haya... tatizo viongozi wetu hawana wivu wa maendeleo, nadhani wao ni matumbo yao tu.
ReplyDeleteKwa nini usimuulize waziri wako wa miundo mbinu.....Go ask your minister of infrastructure development.
ReplyDeletephotoshop!
ReplyDeleteKuanzishwe idara ya beach patrol ama iwe chini ya Utalii au Mazingira kila mkoa wenye Bahari au Ziwa kubwa kuwe na ofisi na hawa kazi yao kubwa ni kuangali usalama wa beach na usafi kuwe na wafagiaji ambao kila siku asubuhi wawe wanafagia beach zote ziwe safi kuvutia watalii wa nje nchi na wa ndani nchi. Nyingi hufanya hivyo hufagia beach zao, mfano Thailand wanafanya hivyo na asilimia kubwa ya pesa ya kigeni hutokana na watalii, Visiwa vya Amerika ya kati hufanya hivyo, hata wakati mwingine wanatengeza beach bandia kwa kupiga greda na kujaza mchanga safi, beach zetu ni chafu jamani zifagiliwe na vijana watapata ajira pia, serikali ikishindwa ziuzwe kwa watu binafsi wazawa.
ReplyDeletehuyo anayemshauri mwenzake akamuulize waziri wa miundo mbinu anafahamu kuwa kumuona waziri bongo ni vigumu kama kuzungumza na queen wa uingereza?
ReplyDeleteyani tangu watu wajue neno photoshop sasa kila kitu ni photoshop ovyooooo!!!
ReplyDeleteAnony wa Dec 14 08:33 thumbs up not only waziri hivi kweli the highest authority wa nchi haoini hayo.Basi poleni sana.
ReplyDelete