Na Woinde Shizza,
Arusha
Timu ya mpira wa miguu ya shule ya sekondari ya Bishop Durning ya mkoani Arusha (pichani) inaondoka wiki jiayo kuelekea mombasa kushiriki mashindano ya vijana wa umri wa chini ya miaka 17 yajulikanayo kama Pwani cup

Mashindano hayo yatakayotiomua vumbi kuanzia tarehe 13 hadi 19 mwezi huu yatashirikisha timu za vijana na zile za taasisi na vyuo vya soka toka nchi za Kenya,Uganda,Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo,Rwanda na Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili mkuu wa shule ya sekondari ya Bishop Durning Sarubale Lendisa alisema wamepokea kwa mikono miwili mualiko huo na hivi sasa wako katika maandalizi makubwa kuhakikisha wanarejea na ubingwa wa michuano hiyo.

Lendisa aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji ishirini kiko kambini na matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa kwani wengi wa wachezaji wake wanashiriki katika ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Arusha na wanatumia ligi hiyo kama sehemu ya maandalizi

Akizungumzia kualikwa katika mashindano hayo ya Pwani cup, mwenyekiti wa timu hiyo Elisha Sironga alisema kuwa walipata mualiko huo kupitia kwa timu ya Mwenge ya Mombasa baada ya kuunda urafiki walipokutana katika mashindano ya vijana yanayoandaliwa na taasisi ya Rolingstone y mjini hapa ambayo hufanyika kila mwaka.

Sironga aliongeza kuwa hivi sasa wanafanya jitihada za kupata kiasi cha shilingi million tatu kwa ajili ya kugharamia ,usafiri, malazi na chakula watakachotumia katika kipindi chote cha mashindano na mikakati inakwenda vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. dah ama kweli..nimemalizia elimu yangu ya form 4 hapo mwaka 2007 na nilkuwa mchezaji wa timu hiyo ya shule ukirudi bishop we ulizia tuu mido ungenipata ..bado kuna wachezaji wawili nawajua hapo ambao nilikuwa nacheza nao amos mzamiru na baba gaucho....

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa mwalimu mkuu Bwana Lendisa. Ushauri wa bure ni kwamba wanafunzi hawa wasijitahidi tuu kwenye michezo lakini pia kwenye masomo kwani mwaka jana matokeo yao ya form four yalikuwa mabovu sana. Guys pull up your sox

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...