Watu watano wamefariki dunia leo, kati yao wanne papo hapo, baada ya gari la mashindano ya mbio za magari kuacha barabara na kuparamia umati wa watu waliojipanga kando kando ya njia eneo la Mikese Njia Nne , Wilaya ya Morogoro na kuwajehuri wengine 12 na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Gari hiyo yenye namba za usajili kutoka Kenya KAK 9208 aina ya Subaru likiwa miongoni mwa magari 16 yaliyoshiriki iliandikishwa namba sita ya katika mashindano ya mbio za umbali wa kilometa 380 yajulikayo kwa jina la Morogoro Pathfinder Rally 2009 na iliendeshwa na Dereva Dharam Pandya( 29).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ferdinaldi Mtui , alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo majira ya saa 4: 30 asubuhi eneo la Mikese Njia nne kwenye barabara ya vumbi baada ya gari yenye namba KAK 9208 aina ya Subaru lililokuwa likishiriki mashindani hayo kuacha njia ya kuwagonga watu pemebezoni mwa njia hiyo na kusababisha vifo wa watu wa nne papo hapo na kujeruhi wengine 12 ambao walikimbizwa Hospitali ya Mkoa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda hiyo wa Mkoa wa Morogoro, watu waliokufa kwenye ajali hiyo walitambuliwa kuwa ni watoto wenye umri kati ya miaka sita na kuendelea ambao walikuwa ni miongini mwa watu waliojitokeza kungalia mbio hizo za magari.
Alisema ajali hiyo katika barabara ya vumbi mara baada ya kufika Mikese Mizani , ambapo magari yayo yalitumia barabara ya kawaida na gari hilo lilipofika eneo lenye kona liliancha njia na kuwaparamia watu na kupinduka na hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo , kuwa kati ya maiti hizo nne ni mmoja ndiyo iliyotambuliwa kwa jina la Jacob Mashaka ( 6) ambaye ni mwanaafunzi wa Shule ya Awali katika Kijiji cha Mikese.
Naye Ofisa wa zamu wa siku ya tukio hilo katika Hosptitali ya Mkoa wa Morogoro, Judith Kagimbwa , alisema siku hiyo walipokea majeruhi 12 waliopata ajali wakati wa mashindano ya mbio za magari iliyotokea eneo la Mikese, Wilaya ya Morogoro.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa zamu, kwamba pamoja na kuwapokea majeruhu hao pia walipokea miili ya watu wa nne waliofariki dunia eneo la ajali hiyo na wakiwa katika harakati za kuwatibia majeruhi hao mmoja wao alifariki dunia akiwa wodini majira ya saa 7: 30 mchana ambaye ni Said Mohamed ( 40) mtanzania mwenye asili ya kiasia.
Hata hivyo Ofisa huyo wa zamu aliwataja majeruhi 11 waliolazwa kwa kupatiwa matibabu ni Pamera Ashumba ( 50), Mgema Deus ( 16), Mwanaidi Rajab (21), Iddi Hamis ( 40), Hadija Mwarabu ( 28), Mwamini Said ( 28), Juma Abdallah ( 33), Alex Mussa ( 14) Daniel Masanja (12) na Shukuru Roma (28) ambao baadhi yao ni wakazi wa Mikese na wengine nje ya Mikese.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa zamu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro siku ya tikio hilo, kuwa madaktari waliendelea na kazi za kuwatibia majeruhi hao.
Ofisa Uhusiano wa Mashindano hayo, Pankaj Valambia, alisema kuwa kufuatia ajali hiyo , wasimamizi wa mashindano hayo waliamua kusitisha mashindano hayo ili kushughulikia watu waliopatwa na ajali hiyo pamoja na taratibu kwa waliofiwa na ndugu zao.
“ Ni kweli ajali imetokea eneo la kona kali Mikese Njia nne na kufuatia ajali hiyo utawala na wasimamizi wa mashindano haya wamelazimika kuyasitisha kabisa kwa lengo la kuungana na ndugu na jamaa ambao wamefikwa sambamba na majeruhu” alisema Ofisa Uhusiano huyo
Hata hivyo alisema Utawala na wasimamizi wa mashindano hayo wameamua kushirikiana na ndugu hao kwa kila hali ili kuwezesha kufanikisha shughuli mbalimbali zinazohitajika kufuatia kutokea kwa ajali hiyo.
Mashindano hayo yaliyoanza juzi kwa mbio za kilometa 41 na jana kwa kilometa 380 yalishirikisha magari 16 kutoka Mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Morogoro na yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu jana kwenye viwanja vya Gymkana vya Mjini Morogoro.

Serikali ipige marufuku watu kukusanyika kwenye vitu kama hivi. Barabara zenyewe mbovu halafu watu wanakusanyika namna hiyo. Hii ni hatari. Nakumbuka wakati tunakaa Arusha, haya mashindano yalikuwa yanapita kule mianzini niliwahi kwenda mara moja tu nilivyoona nilijua ipo siku haya magari yatapitiliza kwa watu. Hii inaweza kuwa bahati ni watu wachache wameumia na kufariki ingeweza kuwa mbaya zaidi.
ReplyDeleteNingependa kutoa rambirambi kwa familia zote zilizoathirika na ajali hii.....pili ningesuggest hizi familia zingeungana na kutafuta mwanasheria mzuri kudeal na ishu nzima,wasideal na waandaaji direct,watawalalia,apart from the loss there is a lot of money to be made from the organizers [Law Suit]...Michuzi usiibanie hii,maana wiki hizi mbili unabania comment zangu sana!
ReplyDeleteMimi nashangaa saana huyu mtu ambae anazungumzia kuwa kuna pesa nyingi za kutengenezwa badala ya kuwapa pole na kuchangia jinsi ya kuwasaidia waliyoumia, hayo masuala ya madai baadae kama una uchungu saana funga safari nenda Mikese kawaone wafiwa wape ushauri mzuru ulioutoa unategemea mtu wa mikese akasoma uliypoandika katika mtandao. Yaliotokea ni accident na bahati mbaya sasa toa mchango wako ni kitu gani kitendeke ili ajali kama hii iepukwe isitokee tena.
ReplyDeleteI am sorry to say that this is just an accident just like other accidents....huyu alikuwa ktk mchezo kama tu football, so, sioni why apelekwe mahakamani. Fidia zitolewe ila huyu dereva asihukumiwe maana alikuwa ktk mchezo ambao umesajiliwa
ReplyDeleteIf you took time to read my comment [which i assume you didn't] i already said ,napenda kutoa rambirambi,halafu suala la kwenda Mikese hali-make sense,unataka kuniambia sisi wote hapa tufunge safari ya kwenda huko? maana ya barua pepe ni nini?...by the way Dunia ya sasa hivi BABU mambo ndio kama hivyo,unafikiri Insurance wanakata za nini? they know anything can happen,na hizo familia zina every right ya ku-SUE the individuals [organizers]...habari ndio hiyo!
ReplyDeleteKilichosangaza ni mwandishi alipoandika there is a lot of money to be made, hapo hakufa ngombe, aliekufa ni biniadamu hakuna thamani yeyote kipesa inaweza kuwa nyingi kwa mfiwa. Ungetumia maneno kama kupata mwanasheria kudai haki zenu kisheria.
ReplyDelete