MZEE KAWAWA AMETUTOKA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA TOKEA JANA BAADA YA KUPATA MATATIZO YA KIAFYA.
ALIZALIWA LIWALE MWAKA 1926 AMBAPO BAADA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI ALIKUWA WAZIRI MKUU KUANZIA JANUARI 22, 1962 HADI FEBRUARI 13, 1977 AKIFUATIWA NA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE. BAADAYE ALIKUWA KATIBU MKUU WA CCM KABLA YA KUSTAAFU.






Innah lillah wa innah lillah rajiun... Ametangulia mbele ya haki na tuliobaki tujiandae.
ReplyDeleteMh! Masaa yaliyobaki ni mengi saaaana kuuona mwaka mpya. Tuombe tupendelewe kuuona.
R.I.P Mzee Kawawa, kama vile ulijua ukaamua kuandika kitabu kuweka kumbukumbu ya fikra zako!
ReplyDeleteMahenge, W.
Ina lillahi wa inna illaiha rajioun
ReplyDeleteRIP Simba wa vita
INNA LILLAH WAINAIRAH RAJIOUN.YEYE AMETANGGULIA NA SISI NYUMA YAKE MWENYEZI MUNGU AMSAMEHE DHAMBI ZAKE.AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMIN
ReplyDeleteSisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi. Tutakukumbuka kwa mema mengi uliyowatendea wa Tanzania
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya mwarehemu mahali pema peponi - Amin. Wafiwa wa karibu sana mungu awape faraja. It should be put on History and probably a Public Day - Kawawa Day on 31st of every December!
ReplyDeleteSio kupenda sikukuu ni kumbukumbu za Kihistoria.
Du! Pole Rehema Mputa, Habiba, Zainab etal - RIP Simba wa vita. Tangulia simba! kale ugali na Julius.
ReplyDeletemzee kamwambie yote Nyerere kuhusu c cm na taifa usimfiche jambo
ReplyDeleteNchi imeingia kwenye msiba mkubwa sana. Poleni sana watanzania wenzangu.MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MZEE WETU.AMINA!
ReplyDeleteREST IN PEACE KIPENZI CHETU Umetangulia tuuu. Utuombe nchi iwe na Amani uchaguzi October 2010. Bila ya kuwepo kwako Mzee mwenye busara. Bite
ReplyDeleterip msalimie nyerere umweleze yote ya mafisadi
ReplyDeleteYou've done your good job
ReplyDeleteIt's time to rest Sir
May your soul rest in eternal peace
Amen
hakika ni majonzi makubwa kwa watanzania kututoka mtu muhomu sana hasa kipindi hichi kigumu kwa taifa likigubikwa na matatizo makubwa ya ufisadi na rushwa...nani atawapa hekima viongozi wetu wanaonuka uvundo wa kukosa uzalendo??? mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi Simba wa vita..Amen
ReplyDeleteMungu aiweke roho yake mahali pema peponi amina. Simba wa vita tuko nyuma yako baba
ReplyDeleteduh pole sana mzee wetu,inabidi sekhe yahya akamatwe sasa,maana kina anachokitabiri kinatokea kweli,maana 3days ago alisema kuanzia juzi hadi april atakufa kiongozi wa juu mstaafu.
ReplyDeleteRIP Simba wa Nyika
ReplyDeletePole kwa Familia
Inna lilahi waina illah rajoun, poleni watanzania wenzangu ni msiba mkubwa
ReplyDeleteInna lilahi wa Inna Ilaihi rajiuuuuun.
ReplyDeleteAmeishi muda mungu aliupanga kumuwezesha kuchuma amal njema.
Alikuwa ameishi simple na kutumikia taifa vizuri tangu akiwa Community Developent Officer, msanii mahiri wa filamu za maendele ya jamii (a.k.a) Muhogo Mchungu. Simba wa vita vya ukombozi kusini mwa Africa na hasa vita vya kumgoa nduli Iddi Amin.
Hakuwa fisadi na hata alipostaafu hakuwa na pension au hata akiba ya kuwa na makazi ya stahiki yake.
Kama ingekuwa tuzo ya Mo Ibrahim ingeweza kutolewa kwa hapa Tanzania angefaa atunukiwe.
Mzee huyu aliwalea watoto wake kama wananchi wa kawaida na hakuwa na haja ya kuwadekeza kwa kuwasomesha nje ya nchi.
Mara kadhaa alibebeshwa lawama za mapungufu ya serikali au makosa ya maamuzi ya cabinet na aliridhia ili kuwe na uamuzi wa pamoja na hadhi ya serikali ya wakati wake. hata baada ya kustaafu alitoa ushauri juu ya mambo kadhaa kila viongozi walipouhitaji. Hakuwa mtu wa makundi na hajawi kutumia nafasi yake kuwapendelea jamaa zake kwa kuwapa kazi, vyeo, nyumba, fedha au chochote kile.
Mungu amsamehe makosa yake, na waliomkosea wamsamehe kwa yale aliyowafanyia wakati wa uhai wake
na Mola amfutie dhambi zake na ampe radhi zake. Ameupushe na adhabu za kaburina na ampe daftari lake kwa mkono wa kulia
Mungu awape subira jamaa zake na hasa wale waliokaribu nae. Awakumbushe subira na sala na waitekeleze maana wanapopata msiba waweze kusema kwake Molla wetu tunatoka na kwake ndio tunarejea
Mkweli
INNALILAHI WAINA ILLAHI RAJIUUN.
ReplyDeleteUmekamilisha muda wako uliopewa hapa duniani nenda ukapumzike kwa amani baba yetu. Tutaendelea kukuombea Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi amin. Ameenda lakini ametuachia watanzania misingi mizuri ya uongozi katika enzi zake. Na familia iliyobaki muwe na moyo wa kusubiri Inshallah Mwenyezi Mungu atawapa maghfira.
Rest in Peace !!!!! yalibaki masaa kuoa mwaka mpya ila hakujaliwa!!!!! 2muombe mungu a2wezeshe kuuona mwaka mpya!!!!
ReplyDeleteMay God Rest his SOul in eternal Peace!!!!
RIP Simba wa Vita!
ReplyDeleteHivi kuna mtu anao waraka wa utabiri wa Sheikh Yahya kwa mambo mwaka 2009? Kama sikosei alitabiri kifo cha mtu muhimu sana ktk taifa hili ktk mwaka huu tunaoumaliza leo.
I am deeply saddened by the sudden death of our beloved son of our national, Mzee Rashid Kawawa. He was one of those true gentlemen and his quiet demeanor and thoughtful nature served him well. His wisdom came naturally from having made a long and careful journey in life and learning so much along the way that he was always willing to share with others. He always seemed to know the right thing to say and at exactly the right time. He truly exemplified all the best qualities that define his generation- hard working, honest, strong, and patriotism. RIP our hero and really true son of our national, Simba wa Vita, Rashid Mfaume Kawawa. Buriani. – Benjamin Ndaga
ReplyDeleteR.I.P SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA (MZEE BARAKA.
ReplyDeleteMTU MKUBWA ALIYEISHI MAISHA YA KAWAIDA MNO. ALIKUWA NA UWEZO WA KUCHUKUA CHOCHOTE KATIKA NCHII BILA KUULIZWA LAKINI ALIKUWA TAJIRI WA ROHO HAKUCHUKUA PUNJE YA CHOCHOTE. AKAKABEBESHWA U-BANGUSILO WALA ASILALAMIKE.
KWA MNAOKUMBUKA MWL NYERERE ALILIA PALE DIAMOND JUBILEE AKISEMA SIJUI NIKUPE NINI RASHID.
ZAWADI PEKEE WATANZANIA WENZANGU YA KUMPA MZEE WETU NI KUMUOMBEA DUA ILI MOLA AMSAMEHE NA AMUINGIZE FIR-DAUSI NA PILI TUFANYE ANGALAU ROBO TU YA MATENDO YAKE.
MOLA WETU. KWAKO TUMETOKA KWAKO TUNAITIKA NA KWAKO TUTAREJEA.
POLE RAIS WETU JK. WAZEE WAKO WALIOKULEA WANAONDOKA. MUNGU AKUPE NGUVU UKUMBUKE WALIYOKUUSIA.
Inna Lillah Wa Inna Ilayhi Rajiuun.
ReplyDeleteI salute , simba wa vita.
Pole kwa ndugu jamaa na watanzania kwa ujumla.
K.O.R.
Mungu alie hai apokee roho yako na kuipumzisha.
ReplyDeletemuadilifu wa mwisho umeondoka, GOD BLESS YOU.
ReplyDeleteWadau tuendelee kupeana pole ya msiba :( .
ReplyDeleteNaona tangazo lina mapungufu kidogo, Marehemu alikuwa waziri mkuu kuanzia tarehe 17 mwezi wa pili 1972 mpaka tarehe 13 mwezi wa pili 1977. na si kuanzia mwaka 1962.
Tanzania ilipokuwa jamhuri mwaka 1962, cheo cha uwaziri mkuu kilichokuwa kinashikiliwa na Waziri Mkuu Mwalimu Kambarage Nyerere kilifutwa. waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania/Tanganyika ikiwa Jamhuri ni Marehemu Simba wa Vita ambaye aliteuliwa 17 februari mwaka 1972.
Mdau Tandale kwa Mtogole,
Rest in peace baba yetu. Pole nyingi kwa my classmate Habiba, Nabu, my work mate at MOFEA Dada Sophia Kawawa. Mungu awape nguvu ktk kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteMUNGU ailaze roho yake Mahala pema peponi. AMINA
ReplyDeleteUliyeulizia juu ya utabiri Google ama angalia Hii linki http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4966
Wewe mtoa maoni wa Thu Dec 31, 01:12:00 PM. Angalia habari ya utabiri wa Shehe Yahya kama lilivyoripoti gazeti la HabariLeo.
ReplyDeletehttp://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4966
"Alisema hivi kutatokea kifo cha kiongozi wa zamani wa kitaifa kati ya sasa na Aprili mwakani, kabla ya uchaguzi"
Hata hivyo siwezi kulink hiki kifo na utabiri wake kwa sababu siamini mambo ya nyota.
Kama kweli Shehe Yahya mtabiri watanzania wasubiri kama kutakuwa na serikali ya mseto baada ya uchaguzi 2010.
ReplyDeleteHivi kuna mtanzania bado anaamini mambo ya Sheikh Yahya. Hivi kama mtu anaumwa yuko hospitali na unajua amezidiwa madaktari wenyewe wanajua hana siku nyingi za kuishi sasa Sheikh Yahya ujanja wake ni yeye ametabiri. Jamani hebu acheni mambo yakijinga sasa. Mwamwimbe akutabirie kifo chako anaatabiri chake akupe na tarehe kabisa ujiandae. Upuuzi mtupu hebu ondokeni na ujinga wa watabiri. Ndio hao hao wanawaambia mkaue Albino mtakua matajiri. Nonsense.
ReplyDeleteRIP MZEE KAWAWA
ReplyDeleteKIONGOZI SAFI WA MWISHO ALIYEKUWA AMEBAKIA AMEONDOKA.
ReplyDeleteRIP SIMBA WA VITA. WE WILL ALWAYS REMEMBER YOU, A GREAT MAN.
TANZANIANS, LIFE GOES ON .......!!
R.I.P. Simba wa Vita.
ReplyDeleteMichu umegonga msumari kichwani uliposema kwamba Kawawa alikuwa kiongozi wa kufanya mambo kwa mfano. Hata baada ya kustaafu alitekeleza yale aliyosimamia katika uongozi wake yaani kilimo kwa kuendeleza kilimo cha uyoga. Hakuishia hapo, akaeneza ujuzi huu kwa yeyote aliyetaka kufuatilia.
Nakulilia Mzee Kawawa. Nakulilia.
Mtu yeyote ukiona tu kiasi cha kujilimbikizia kilichofanywa na baadhi ya mawaziri wakuu waliofuatia ndio unaelewa kwamba Mzee Kawawa alijali zaidi maslahi ya wananchi kuliko ya kwake.
R.I.P.
Mungu naomba umpumzishe Mzee wetu kwa amani, Amina.
REST IN PEACE MR RASHID KAWAWA. YOU SURE WILL BE MISSED. PLEASE PRAY FOR US WHO ARE STILL ON THE JOURNEY. MAY YOUR SOUL BE LIFTED AND REST IN ETERNITY. AMEN.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya marehemu peponi.Kweli mzee Kawawa ametumikia nchi ya Tanzania kwa moyo wake wote. Na Tanzania inabidi impatie heshima zote. "aluta continua" mdau USA
ReplyDeleteTupo pamoja na ninyi wanafamilia ya Marehemu Mzee Rashidi Kawawa katika kipindi hiki kigumu, Tuanomba Mungu amlaze mahala pema peponi, Amen
ReplyDelete.
Rashidi Mfaume Kawawa (born 1929), Tanzanian political leader, devoted his career to policies designed to increase his fellow citizens' standard of living.
The son of an elephant hunter and the eldest of eight children, Rashidi Mfaume Kawawa was born in the Songea district of Tanganyika (now Tanzania) in eastern Africa. After primary schooling in Dar es Salaam, he finished his formal education at Tabora Government Secondary School (1951-1956), the alma mater of Julius Nyerere, leader in the fight for Tanganyika's independence. Kawawa refused the opportunity to continue his education at Uganda's Makerere College, thus enabling his father to use the family's limited resources to educate his siblings.
Early Career
Kawawa's first job was as a Public Works Department accounts clerk. This was a most difficult period for the young man. With the death of his father, he assumed the responsibility of supporting his younger brothers and sisters. In 1951 Kawawa realized a long-standing dream of becoming a social worker. He had actually inaugurated this career by organizing a literacy campaign for adults while a student in Dar es Salaam.
On his new job Kawawa joined a mobile film unit engaged in government literacy programs. When it was decided to use the unit for educational filming, he was chosen as the only Tanzanian leading actor. He also served as a scriptwriter and a producer. Perhaps the most important aspect of Kawawa's social worker career occurred when he was sent to central Tanzania (1953) to work among Kikuyu detainees held because of the Kenyan Mau Mau movement. He later described his successful work there as the "greatest challenge of my life."
Government Service
Kawawa joined the Tanganyika African Government Services Association, becoming its assistant general secretary in 1951 and its president in 1955. His main task was securing rights for government employees due them under Tanganyika's laws. Realizing the advantages of a nationwide organization, Kawawa helped found the Tanganyika Federation of Labor (TFL) and was elected its first general secretary in 1955.
The Tanganyikan independence movement was then underway, directed by Julius Nyerere of the Tanganyika African National Union (TANU). Kawawa's government employment prevented him from political participation, but his commitment to use the unions to further independence led to his resignation in February 1956 to devote his time and talents to labor and political organization. Joining TANU, he became a central committee member (1957) and vice president (1960). In the meantime Kawawa had been appointed to the Legislative Council (1957), remaining a member until 1960. In September 1960, following his first appointment to Cabinet rank, he resigned from the TFL to concentrate on politics.
When Prime Minister Nyerere of the now independent Tanganyika resigned for a brief period in 1962, Kawawa replaced him until his return to office. After 1964 Kawawa held the office of second vice president of Tanzania (formed from the union of Tanganyika and the island republic of Zanzibar), serving as Nyerere's principal assistant for mainland affairs and as leader of the National Assembly.
Nyerere resigned as Tanzania's president in 1985, and Kawawa left government service as well. However, he was seen once more in the political spotlight when he attended the seventy-fifth birthday celebration of former president Nyerere in early 1997.
MTOGOLE USISAHAU PIA KAWAWA ALIKUWA WAZIRI MKUU WA TANGANYIKA KUANZIA TAREHE 22 JANUARI MWAKA 1962 MPAKA TAREHE 9 DECEMBER MWAKA 1962 BAADA YA MWALIMU NYERERE KUJIUZURU KWENDA KUIMARISHA CHAMA.
ReplyDeleteTAREHE 9 DECEMBER MWAKA 1962 BAADA YA TANZANIA KUWA JAMUHURI WADHIFA WA UWAZIRI MKUU ULIFUTWA NA KURUDISHWA TENA TAREHE 17 FEBUARI MWAKA 1972 AMBAPO SIMBA WA VITA ALIRUDISHWA TENA KENDELEA NA UWAZIRI MKUU MPAKA TAREHE 13 MWEZI WA PILI MWAKA 1977 ALIPOBADILISHWA NA EDWARD MORINGE SOKOINE.
PAMOJA NA KUWA ALIONDOLEWA KWENYE WADHIFA ULE BADO ALIKUWA NA NGUVU NYINGI UKIZINGATIA ALIKUWA KATIBU MKUU WA CHAMA NA WAZIRI WA ULINZI MIAKA ILE CHAMA KILIKUWA KIMESHIKA HATAMU NA ILIKUWA VIGUMU SANA KUJUA NANI NI MKUBWA KATI YA WAZIRI MKUU NA KATIBU MKUU WA CHAMA SI KAMA SIKU HIZI KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI.
KWA MFANO KATIKA VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI MEZA KUBWA WALIKAA NYERERE, JUMBE NA SOKOINE LAKINI KATIKA VIKAO VYA CHAMA ALIKUWA NYERERE,JUMBE NA KAWAWA NA TUKUMBUKE MIAKA ILE VIKAO VYA CHAMA VILIKUWA VINGI MNO KUPITISHA MAAZIMIO MBALIMBALI NA MWONGOZO WA SERIKALI SI KAMA SIKU HIZI.
NYERERE ALIKUWA ANAMPENDA KAWAWA NA KAWAWA ALIKUWA ANAPENDA NYERERE, WALISHIBANA. KWA WALE WATU WASIKU NYINGI KIDOGO, MWANZO KAWAWA ALIKUWA AKIHUTUBIA KWA SAUTI ALIYOKUWA NAWEZA KUSEMA AMEZALIWA NAYO LAKINI SIKU ZILIVYOKUWA ZINAENDA IKABADILIKA NA KUWA ILE YA NYERERE, ALIKUWA MTU SAFI NA MCHAPA KAZI SANA HAKUNA MFANO NA SI MBINAFSI SI MWIZI NI MFANO WA KUIGWA
ReplyDeleteHivi vibabu viwili vilikuwa marafiki na kupenda kuvaa sare na kofia.
ReplyDeleteKaka Michuzi,madhehebu hayana wingi wala umoja.madhehebu ni madhehebu HAKUNA dhehebu la Ismailia wala WaShia.Kimsingi ni madhehebu ya Ismailia,WaShia,WaSunni.
ReplyDelete