Marehemu Dk. Lawrance Gama (pichani) ambaye alifariki dunia jana mchana katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake huko Songea siku ya Jumapili December 20, 2009 imefahamika.


Habari za kifamilia zinasema tayari maamndalizi yameanza kwa mazishi ya kiongozi huyu huko Songea, na jijini Dar watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwake kutoa rambirambi.


Dk. Gama atakumbukwa kwa utendaji kazi wake tokea akiwa Katibu Mkuu wa CCM, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Mkoa wa Dodma, Ruvuma na Tabora. Alipata pia kuwa Mbunge wa Songea Mjini kwa nyakati tofauti.

Gama aliwahi kuwa mbunge wa Songea Mjini tangu Oktoba 15, 2000 hadi Agosti 30, 2005 alipoangushwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Historia ya maisha yake inaonesha kwambha alizaliwa Januari 19, mwaka 1935 na alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1968 hadi 1969 na kutunukiwa cheti cha sheria.

Kati ya mwaka 1949 hadi 1950 alipata mafunzo ya Jeshi la Polisi katika Chuo cha Honden nchini Uingereza. Baada ya hapo alirudi tena nchini humo mwaka 1960 hadi 1961 ambako alipata mafunzo zaidi katika chuo cha Liverpool. Pia alijiunga na chuo cha mafunzo ya kijeshi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kozi mbalimbali.

Aidha, alihudhuria mafunzo ya juu nchini Marekani na mwaka 1985 hadi 1986 alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Berlin nchini Ujerumani. Mwaka 1987 hadi 1999 akiwa katika chuo hicho aliendelea na masomo na kufanikiwa kutunukiwa Shahada ya Udaktari (PhD).

Alipata kuwa mkuu wa mkoa kati ya 1997 hadi 2000 ambapo mwaka 1976 hadi 1982 alishika wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa nyakati taofauti katika mikoa ya Dodoma, Ruvuma na Tabora.

Pia mwaka 1972 hadi 1975 alikuwa Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa wakati mwaka 1970 hadi 1972 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Kati ya mwaka 1954 hadi alikuwa Ofisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa upande wa siasa, Gama alikuwa Katibu Mkuu wa CCM kati ya mwaka 1994 hadi 1996 na 1977 hadi 2002 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM. Mwaka 1975 hadi 1982 alikuwa katibu wa mkoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. DR.LAWRANCE MTAZAMA GAMA.

    KAPUMZIKE KWA AMANI BAMBO, NA MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA.

    Nditi - GESAMACHOWA

    ReplyDelete
  2. POLENI WAFIWA KWA MSIBA MZITO WA KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU.DAIMA NITAKUKUMBUKA KWA MCHANGO WAKO KATIKA NYANJA MBALI MBALI ZA SIASA NA MICHEZO.WENGI WALIKUSAHAU LAKINI UNA MCHANGO MKUBWA KWA SOKA LA TANZANIA.ULIANZISHA TIMU ZILIZOLETA USHINDANI LIGI KUU.MFANO MAJIMAJI.LIPULI NA MIRAMBO YA TABORA.
    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU GAMA MAHALI PEMA PEPONI.
    AMEN.

    ReplyDelete
  3. kwanza kabisa poleni wafiwa.
    pili mmh,wewe mtoa wasifu wa marehemu kidogo umenitatiza hapa:-
    1)alizaliwa 1935,na mwaka 1949-1950 akapata maafunzo ktk chuo cha polisi honden uingereza. sasa hapa naona alikuwa na miaka 14 alipoanza mafunzo ktk chuo cha polisi na alimaliza ana miaka 15. je hii imetulia kweli??
    sijui lkn mmh!!
    2)pia phD YAKE kasoma muda mrefu sana lkn hapa haina shida maana inategemea alisomaje pia, 1987-1999=12yr!!!

    ReplyDelete
  4. R.I.P dk.gamma.
    mwandishi wa wasifu vipi wasihu wa marehemu haujafuata mtiririko vizuri.tukufundishe kuandika nini? haya naanza:

    kuzaliwa-19 jan.1935.
    mafunzo ja jeshi la polisi honden wingereza 1949-1950.
    afisa wa polisi 1954-x
    mafunzoni liverpool 1960-1961.
    chuokikuu mlimani(sheria)1960-1968.
    mkuu wa jeshi la kujenga taifa JKT 1970-1972.
    mkugenzi mkuu idara ya usalama wa taifa 1972-1975.
    mkuu wa mkoa wa dodoma,ruvuma,tabora 1976-1982.
    shahada ya uzamili chuo kikuu berlin 1985-1986.
    phD ktk... chuokikuu berlin 1987-1999.
    mkuu wa mkoa wa... 1997-2000.
    mbunge wa songea 2000-2005.
    kisiasa,marehemu alipata pia kuwa:
    mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM 1975-1982.
    katibu mkuu wa CCM(ngazi ya..)1994-1996.
    MAREHEMU ALIHUDHURIA MAUNZO TOFAUTI nchini marekani,...,....,
    alifariki trh.....na kuzikwa ni trh....

    nadhani unaona mtiririko unaofaa kuandika wasifu mkuu au sio?

    ReplyDelete
  5. Binafsi nimesikitika sana kutokana na kifo cha mzee wetu Dr. Lawrence Mtazama GAMA. Alikuwa ni kiongozi shupavu sana wakati wa uhai wake. sisi watu wa Songea tutamkumbuka zaidi kwani ni katika kipindi cha utawala wake ndipo tulipoweza kufanya mambo mengi ya maendeleo. Nakumbuka kauli mbiu kama agizo la Mlale.
    Natumaini ataenda kuzikwa kijijini kwake alikokupenda sana kule Amani Makoro.
    Pumzika kwa amani Nduna wetu Dr. Lawrence Mtazama GAMA

    ReplyDelete
  6. Wafiwa poleni sana.Anna Gama pole sana.
    IFM student 1998.

    ReplyDelete
  7. Jamani rest in peace. I used to go his house wakati nasoma tabora.

    ReplyDelete
  8. Chilingi ChumuniDecember 18, 2009

    Poleni wafiwa woote.
    Hii PhD yake aliisotea kwa miaka 12!!!!?? Nadhani hapo waandishi mmekosea kidogo hebu rekebisheni ili tuelewe vizuri.
    Ooh!! Lakini inawezekana kwa sababu zamani ukienda ulaya kimasomo ilikuwa unjifelisha ili usirudi nyumbani haraka na uendelee kula maisha ya kuku kwa mrija.
    Pia msisahau kuwa alikwenda huko akiwa tayari ni kachero wa ngazi ya juu.
    Mwanga wa milele umwangazie eeh Bwana.

    ReplyDelete
  9. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
    Wapenzi wa soka tutakumbuka mchango wake. Uwanja wa Majimaji, timu ya Mirambo.

    ReplyDelete
  10. Wafiwa Poleni Sana na Msiba..Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.


    Wewe uliyeandika huu wasifu wa Marehemu umeniydhi sana....yaani baada ya kuandika hata wewe mwenye hukuona kama kuna haja ya kuisoma kama unatoa ujumbe unaoeleweka..!!!???

    Watanzania tumezoea kulipua kila jambo tunalofanya...aggrrrr

    ReplyDelete
  11. PETER NALITOLELADecember 18, 2009

    MICHUZI MIMI SINA SHARI LAKINI NAULIZA KWA NINI TUNA WAPA POLE WAFIWA WAKATI TUKIJUA FIKA WOTE TUNA ELEKEA HUKO HUKO TUTAKUFA ONE DAY OR LATER? MIMI SIONI HAJA YA KUOMBEANA WALA KUPEANA POLE KWA SABABU MBILI KWANZA TUNAIMANI HUKO WAENDAKO WAFU NI POA KULIKO MAISHA HAYA YA DUNIANI PILI KILA MTU ANA SIKU YAKE SASA CHA MSINGI NI KUJIANDAA TIME IKIFIKA WATU WANAKUAGA KAMA TUNAVYO AGANA MGENI AKIJA KUKUTEMBELEA... I MEAN UNASEMA HONGERA NENDA KALE GOOD TIME TUTAKUTANA SIKU MOJA TUTA KULA NA KUCHEZA, SIONI HAJA YA KULIA WAKATI MGENI ANAONDOKA BAADA YA KUKUTEMBELEA? HII TABIA INABIDI IKOME! MIMI NILIKUWA MTUNDU SANA MUZUMBE CHUO KIKUU NILIKUWA NI MTU WA DEEP THINKING MPAKA NIKAPEWA JINA LA KAMUZU BANDA, I AM SMART AND DEEP THINKER. NAWAKILISHA...........!

    ReplyDelete
  12. Kapumzike kwa amani baba mzee Gama, you are already missed.Thanks for everything.
    Miss E.

    ReplyDelete
  13. RIP mzee Gama,Anna Gama pole sana pamoja na familia yenu yote.Nalitolela Nalitolela unaboa

    ReplyDelete
  14. WE MISS YOU ALREADY!

    Here goes one of the few tanzanians who really worked for our country.

    What moves through us is a silence, a quiet sadness, a longing for one more day...we may not understand why you left before we were ready to say good-bye.
    Little by little we begin to accept not that you have gone but that you lived and that your life gave us memories too beautiful to forget.

    Your good deeds honors your family and friends.

    RIP Lawrence
    Old friend (Old is Gold)

    ReplyDelete
  15. Poleni sana Florah,mwl Mary Gama Morogoro na wafiwa wote,nimepokea kwa hudhuni taarifa ya MSIBA WA BABA GAMA,Mungu alitoa na Mungu ametwaa.
    Ni mimi,
    Anna Gama,
    London.

    ReplyDelete
  16. RIP Baba.. Anna na May Gama tupo pamoja katika sala

    ReplyDelete
  17. huyu Anna Gama alisoma Zoo Iringa?poleni

    ReplyDelete
  18. PLEASE WRITE CHRONOLOGICALLY, DONT JUST MIX THINGS, NO ONE WOULD UNDERSTAND WHAT YOU WANTED TO CONVEY, PhD FOR TWELVE YEARS IS NOT NEW THING, IT IS OBVIOUSLY POSSIBLE THERE ARE SO MANT PEOPLE IN THIS WORLD WHO HAVE DONE PhD FOR SO MANY YEARS, SO IT IS NOT SOMETHIG UNUSUAL, ALSO YOU HAVE FORGOTTEN TO MENTIONED THAT HE WAS A BROTHER IN LAW TO NYERERE = ALIWOWA DADA YAKE NYERERE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...