Home
Unlabelled
gari la umma kazini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mdau ni heri mmeyaona wenyewe kwani wengine tukisema tunaambiwa tuna wivu. Hii hali isipotazamwa na hawa zecomedy wetu sijui kama kweli tutatoka katika umasikini huu. Hapo angalia yanatumika mafuta ya serikali si ya mtu binafsi, mimi nashangaa unakuta hata mke wa boss naye anapelekwa kazini na kurudishwa, magari hayo hayo yakachote maji na hatimaye nyasi na mbolea za shamba.
ReplyDeleteHaya bwana hii ndo bongo lala kweli.mwambieni makamba atetee tena hii dharau kwa umma.
NINA HASIRA NA HAWA VIBOSIRE UCHWARA. WE ACHA TU IPO SIKU YAO WATASAGA MAWE KWA MENO
Maskini! Kwa bei ya haraka haraka Gari hiyo inaenda mpaka 65,000 USD Halafu inaishia kubeba nyasi! Tatizo si la huyo bosi, tatizo ni la serikari unampa gari ya bei hiyo mfanyakazi unayemlipa mshahara wa laki 5 kwa mwezi, ndoto ya kumiliki gari hiyo hana maisha yake yote, Hawezi thamini wala hawezi itunza. By the way kwanini serikali inatumia pesa nying namna hiyo kununua magari ya gharama kiasi hicho? Yaani serikali zetu hizi sijui hamana anayefikiri, they alwayas think of roofing instead of buliding foundations. Hiyo pesa inaweza boresha mishahara ya Walimu wangapi ambao watazalisha wanafunzi bora wangapi amabao watalitumikia taifa kupitia taaluma zao!
ReplyDeleteDo, Waziri mkuu ameipata hii?
ReplyDeleteMajani ni ya boss au ni ya ngombe wa dereva? au limekodishwa?
Nidhamu hapa kidogo inautata!
Nafikiri, kwa vile reg. number zaweza kutambua hilo gari ni la wizara gani na liko chini ya nani, basi hakuna haja ya kuunda tume!
Mhusika angeachia ngazi mara moja kupunguza gharama za kumfukuzisha kazi
Bongo tambarareeeeeeee banaaaaaa.
ReplyDeleteNaomba serikali ifanyie kazi hili suala mana ni rahisi now kutrack na kujua nani ndo muhusika huu ni utumiaji wa mali ya umma kwa manufaa binafsi na inatubidi kubadilika kwa kweli kwa maendeleo ya nchi yetu sio kila siku kutupiana maneno yasiyo na manufaa.
ReplyDeleteMmmmhhh! kazi tunayo.
ReplyDeleteTatizo kubwa la watanzania, hatuna utaratibu wa kulipa kodi. Kaka kweli tungekuwa tunalipa kodi ipasavyo basi tungekuwa na jeuri ya kukemea uovu huu.
Utakemeaje uovu wakati mwenyewe hauko sawa? Waingereza wanase, EQUITY PREVAILS UNLESS YOU HAVE CLEAN HANDS.
Na hilo gari inaonyesha ni la kiongozi mkubwa tu serikalini, kwani namba zake ni za kubandika ili muhusika mwenyewe akiwepo basi namba halisi zionekane. Possibly a minister W KV (Mfano, WAZIRI KUKU NA VIFARANGA)
fuata maisha yako, subiri na wewe uingie ofisini tuone upafekti wako
ReplyDeletetena ni kwa nini wafuge ng'ombe mjini?? ni uchafuzi wa mazingira kuharibia majirani zenu hali ya hewa mna kera sana yani magari ya vibosile hawa yakiwa yanatoka dodoma utachoka na roho yako yanashindiliwa magunia ya mkaa huku wanajidai kupiga stop utumiaji wa maliasili wakati wao ndo wavunja sheria namba moja oneni mnavyoumbuka ingekuwa ni cruizer lako usingebeba majani humo ndani meno ya mwenzio kutafunia mchanga ni poa sana kweli cha mtu mavi viongozi wetu acheni umimi msiharibu mali za umma kwa makusudi wengine wakija watatumia nini?? au ndo yakanunuliwe mengine mapya muwe na huruma enyi mafisadi sugu!!
ReplyDeletemdau canada
vichwa vyetu sijui. NITATUKANA BURE.Hebu angalieni Rwanda jamani
ReplyDelete!"$^*¬?+=*£|^)9~>%$*N&+kudadadadada-leki
Tatizo huyu anaweza chukuliwa hatua ila kuna wengi tu wanayofanya haya na mengineyo kwa kutumia mali za serikali na bado wanapeta labda wawekwe hadharani. Watu hawana discipline na kazi zao kabisa. TANZANIA KWELI TAMBARARE.
ReplyDeleteWewe umejuaje ni ng'ombe wa bosi? Wabongo... Mimi msure kabla hajastaafu alikuwa kibosile fulani na mara nyingi huko mitaani nilikuwa nakuta dereva wake amebeba nyasi wakati sisi tulikuwa hatuna ng'ombe nyumbani. Kwa kuwa naye alikuwa anatupeleka tunakotaka bila msure kujua nilikuwa namkaushia na sijawahi kumwambia mdingi. Kwa hiyo msijenge chuki bila kujua tatizo ni nani na ni wapi. Kesho mtasikia huyo dereva ambaye mshahara wake haufiki laki moja amefukuzwa kazi na bosi anaendelea. Hata kama ng'ombe ni wa bosi atakayekuwa matatati ni dereva. Fikirini kwanza kabla ya kutoa umbea wenu.. Hii bongo bana...
ReplyDeleteMbaya zaidi,pale unapokuta kwamba hata hayo majani si ya dereva,familia ya bosi au wizara...bali ni ya kimada,au ndugu yake kimada...sema bana,bongo ni tambarare,unabisha?
ReplyDeleteMara nyengine tunakuomba mpigaji wa picha ujitahidi kutumia kamera yenye "time stamp" ili tuwe na ushahidi mzuri wa kumchukulia hatua anayehusika. Maelezo yako ya siku (tarehe) wakati , sehemu gari ilipokuwepo na muhimu sana.
ReplyDeleteNakupongeza kwa kazi nzuri , shika uzi huo huo katika ujenzi wa Taifa.
Bibi: Mwanangu naomba msaada wa kamzigo kangu haka ng'ombe wangu hawajala siku ya tatu hii.
ReplyDeleteDevera: Mama hili gari ni ya wenyewe haturuhusiwi kubeba mizigo ya watu.
Bibi: Naomba basi shilingi hamsini niweze angalau kuongezea kwenye nauli.
Dereva: Yaani hata shilingi hamsini huna sasa huku ulikuja kufanya nini?
Bibi: Mume wangu amefariki juzi na bado hatujapata hela za kumsafirisha na ng'ombe ndiyo siku ya tatu hawajala ndiyo maana nimeamua kuja huku mwenyewe.
Dereva: Pole mama kwa matatizo, nitakusaidia kwa leo tu. Zilete basi hizo nyasi.
Njiani.
Mbea: Hehehe kamera yangu iko wapi hawa mafisadi wamezidi lazima niwaweke kwa michuzi.
Mshkaji:Mamaa tena kweli CCM wamezidi.
Bibi: Mwanangu nahisi kuna mtu atakuletea matatizo kwenye kibarua chako lakini atamfuata mume wangu hivi karibuni.
Dereva: Mmmmmh Mola niepushe na balaa hili.
Kwanza ninampongeza mlipakodi aliyepiga picha hii. Kama walipakodi tulio na uchungu na kodi zetu tukianza kupiga picha kama hizi na kuzitundika mtandaoni, mafisadi wataanza kujiuliza mara mbili kabla ya kutenda ufisadi.
ReplyDeleteLakini kuhusu picha hii mimi ninaona hizo si nyasi za ng'ombe. Ni kama mboga za majani hivi (mchicha au sukumawiki). Jamani, sasa hamtaki hata vigogo wawatafutie chakula bora familia zao?
mjukuu wa makamba
Daaaaaaaaaaaaaaah Mshanifukuzisha kazi Ila Shemeji yangu yupo pale kiti chaj uu sitofukuzwaaaaa hayooooooooo hahaaha. X to X
ReplyDeletethis is nothing new...tangu enzi za Nyerere, serekali does not want us to move forward...I guarantee 50 YEARs from today, sisi tutabaki hivo hivo bila maendeleo....sorry to see hali yetu but that is the truth...omba...omba...omba is what we all take pride in including top officials
ReplyDeleteNIMECHOKA NAO HAO, WANA MSEMO WAO HAO, NI KWAMBA UKIWA KATIKA NAFASI YA KUIBA IBA, NA UKIWA KATIKA NAFASI YA KUTUMIA MALI YA UMMA UTAKAVYO TUMIA, NDO MAANA WANAIBA SANA NA WANATUMIA OVYO MALI ZETU/ZA UMMA. HAMNA MZURI HATA MMOJA TOKA JUU HADI CHINI WAKO KAMA TAI WAMEONA MZOGA WANAGOMBANIANA TU KAMA MAFISI KILA MTU ANAIBA KWA MTINDO WAKE KWANI WANASEMA MBUZI ULA REFU WA KAMBA YAKE, MAMBUGA YOTE YA WANYAMA NI YAO NA WAMEJENGA MAHOTEL YA KUTISHA KWA KUTUMIA MAJINA YA WABIA WAO, HATUTAFKA NA TUTAKUWA HIVI HIVI UMASIKINI HADI KIUNONI LABDA MIAKA ELFU IJAYO WAKATI KIZAZI HIKI BALAA KITAKAPO KWISHA.
ReplyDeleteah!baraa gani tena?kumbe wale vichaa wa ngoma afrika walioyaimba yapo? gari ya umma mtu anaandika jina lake
ReplyDeleteYaani ni aibu tupu na inasikitisha sana watu kutumia madaraka yao vibaya!ndiyo maana watu wanagombania vyeo ili waweze kutumia vibaya mali ya umma na madaraka yao,na huyo si mmoja tu anayootumia mali ya serikali vibaya,wapo wengi tu!Je Mh.Rais wa Tanzania hayaone hayo?kweli nchi yetu itaendelea lini?wenzetu nchi zilizoendelea za Ulaya, mawaziri na wabunge wao wanapanda baiskeli kuendea kazini!na sisi nchi yetu ya kimaskini mawaziri na wabunge wetu wanapanda Land cruser na kufuja mali ya serikali,kila siku tutabaki hivi hivi bila ya maendeleo na kusubiri misaada itoke nje ili wanunulie magari yao yenye bei ya gharama na kutanuli na kufuja mali ya umma!
ReplyDeleteyale tusiyoyaona ndio balaa kabisa
ReplyDeleteWadau, hii serikali ya wabinafsi wanachojali ni maslai yao, Tujiulize kwanini kwa mfano mwanasiasa anunue kura?? ili aingie serikalini anyonye jasho la walalahoi walipa kodi, mamilioni ya watanzania tunalipa kodi na hayo ni baadhi ya matumizi ya kodi zetu! Lakini swali la msingi la kujiuliza kwanini wanatununua?? La pili viongozi wengi walio madarakani wanamaovu yao na kwa namna moja au nyingine wanajuana na ndio maana swala la kukomesha matumizi mabaya ya mali za umma au kukemea ufisadi inawawia ngumu sanaaaaa! Tunaposema serikali iangalie tukumbuke huyo mwenye hiyo gari ni sehemu ya hilo serikali then unategemea nn???? Viongozi wetu wengu wapo ktk nafasi hizo kwa maslai binafsi na wengi wao ni wachafu pia ndio maaana hawawezi kukemeana. Tufanyeje???? Kwanza tusikubali kununuliwa, tuwewaadirifu katika sehemu zetu za kazi, tuweke maslai ya taifa mbele then tuwakose kwa nguvu zote hawa wala jasho la walalahoi.
ReplyDeleteMim sijaona kama kuna ubaya hapo hilo gari sawa ni la serikali na ni la umma hakuna ubaya ukimkuta bib yako njiani na mizigo yake uogope kumsaidia eti utapigwa picha,acheni ushamba wadau mnaopinga hili gari ni kitu kidogo sana hakuna ubaya wowote kutumia gari la serikali kutoa lift kwa watanzania na mizigo yao manake wao ndio walipa kodi na ndio waliosababisha kuwepo hilo gari pia nampogeza sana huyo bosi/Dereva aliyebeba hayo majani kama ni ya mama,baba,mke au yake mwenyewe ni vizuri na anaonyesha kujali na uzalendo usikatishwe tamaaa na wanga.
ReplyDeleteJAMANI HIVI MNAFAHAMU KUNA KITU WANASEMA KUTOA KAFARA? ANGALIA HII PICHA ITAKAVYMFUKUZISHA KAZI DEREVA KWA MATUMIZI MABAYA YA GARI
ReplyDeleteYAANI MI NIKIANGALIA MAMBO YANAYOENDELEA HAPA KWETU NASHINDWA KUELEWA KABISA, HIVI MGANGA ALIYETUROGA KAFA??!!! 2010 MI NAMPIGIA KURA KAGAME AJE KUWA NANIHII WETU..... KURA ZISIPOTOSHA NAHAMIA RWANDAAAAAAAAA
ReplyDeletechiggs, deslam
Mdau Marium Khalid, hilo gari siyo la Wizara... ni either la Ikulu au la Usalama wa Taifa ndo maana lina namba mbili. hiyo inayoonekana imebandikwa kwa hiyo mipira miwili myeusi... habari ndo hiyo
ReplyDeleteAngalia vizuri hiyo plate namba imekua planted,dreva huyu atakua more SMART kuliko mlipa kodi wetu aliefotoa hii picha.
ReplyDeletemh...nyie vipi???
ReplyDeleteacheni umbea huo,kwani mkisafiri na magari ya ofisi nyie hambebi mikaa na magunia ya viazi,vitunguu nk njiani???
acheni zenu
Hapa mmeona kiduchu tu
ReplyDeleteMngeona sinema yenyewe mbona mngekoma.
Linchi limeoza hili ndio maana kila mtu anafanya anavyotaka
Hata ukipost picha hii, kuna nani wa kufuatilia wakati wahusika wote wako likizo?
WACHA WABEBE HATA MAVI...SASA HIVI MNAJIFANYA KUSEMA WAKATI WAKURA MKIPEWA OFA YA SODA AU KANGA MNASAHAU NA KURUKWA NA AKILI....WAACHENI WABEBE CHOCHOTE..WANAJUWA KAMA MTAWAPA KURA ZENU TENA...NA MARA INGINE TENA HAWACHUKUI MAJANI WATACHUKUWA WATOTO ZETU NA MAMA ZETU. AMKENI NA TUTHAMINI KURA NA TUSIBABAISHWE NA UTUNZO WA MASHAIRI ZA SHEREHE ZINAZOTOLEWA KILA KUKICHA. UKITAKA KUJUA MTU KAMA MSAFI AU SIO...MWANGALIE YEYE KWANZA YUKOJE NDIO UTAJUWA YANAYOTOKA MDOMONI YA UKWELI AU LAA...
ReplyDeleteWAACHENI WABEBE CHOCHOTE..WANAJUWA KAMA MTAWAPA KURA ZENU TENA...NA MARA INGINE TENA HAWACHUKUI MAJANI WATACHUKUWA WATOTO ZETU NA MAMA ZETU. AMKENI NA TUTHAMINI KURA NA TUSIBABAISHWE NA UTUNZO WA MASHAIRI ZA SHEREHE ZINAZOTOLEWA KILA KUKICHA. UKITAKA KUJUA MTU KAMA MSAFI AU SIO...MWANGALIE YEYE KWANZA YUKOJE NDIO UTAJUWA YANAYOTOKA MDOMONI YA UKWELI AU LAA...
ReplyDeleteNI KWELI SENTNCES ZA HUYO JAMAA HAPO JUU BW.SAID KWA HAKIKA SISI WATANZANIA TUMEPUMBAZWA NA HAWA VIGOGO NDIYO MAANA YAOTE HAYA YANAKUWA,ONA MFANO BURUNDI HAKUNA MCHEZO HUU, WAZIRI ANAPEWA GARI YA KAZI KI-CORROLA NA SIYO MASHANGINGI KAMA HAPA KWETU TZ MKUU WA MKUU WA WILAYA ANAPEWA SHANGINGI SASA HAPA WEWE UNATEGEMEA NINI ?????????????LAZIMA WANANCHI MUANGALIE KURA ZENU SIYO MRADI TU UNATUPA KURA YAKO BILA MPANGO.