ZIMEBAKIA SIKU CHACHE ILI NCHI WASHIRIKI KUFIKIA MUAFAKA WA
KUPUNGUZA GESI YA CARBON DIOXIDE HUKO CAPENHAGEN.NAPENDA
KUELEZEA KUWA WATANZANIA PIA TULIANZA ZAMANI KUELIMISHA JAMII
KUHUSU MADHARA YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA ONGEZEKO LA
JOTO DUNIANI.INGIA KWENYE WEBSITE HAPO CHINI NA BONYEZA ,
"RESEARCH AND EDUCATION " HALAFU BONYEZA "CONTINUE".UTAPATA
MAELEZO JINZI GANI TUNATAKIWA KUFANYA NA TUJIANDAE VIPI KUWEZA
KUZOEA HII BADILIKO LA HALI YA HEWA NA ONGEZEKO LA JOTO DUNIANI.
www.ireq-tanzania.com

The Institute Of Research And
Environmental Quality[IREQ]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tutie hamasa kwa kutudokolea kidogo kilichomo ndani ya webusaiti yenu.

    Maana masuala ya Copenhagen Denmark ktk televisheni wameeleza hoja lukuki mpaka tusha kinai.

    Hivyo turahisishie mambo kwa kutupa dondoo hata ktk bullet-form tuone kama una hoja tofauti mfano:

    -kuyeyuka na kupotea kwa Barafu Greenland (Artic na Antica)kutasababisha Darisalama kufunikwa na barafu ili ku-balansi mazingira-asili ya sayari ya dunia.

    Mdau
    Kakamiye

    ReplyDelete
  2. haya mambo ya mazingira kwa nchi zetu masikini wanatusingizia tu, madhara tunayoya aona sasa hayakuletwa nkuchoma mkaa, kupika kwa kuni au watu kujisaidia kwenyye vyanzo vya mito,hata wao wanajua kuwa mapinduzi ya viwanda pamoja na matumizi ya silaha kali za kivita ndiyo yaliyotufikisha hapa, kwa hiyo badala yakupoteza muda na kula posho kilafi waambieni nchi zilizoendelea wafanye kile kinachotakiwa kuokoa mazingira, wanajua nini kinatakiwa kifanyike, kwa sababu hata hawa wattlamu wetu wa mazingira sehemu kubwa ya maarifa yao wameipata kutoka katika nchi zilizoendelea kiviwanda, kuwa kusomea huko au kutumia vitabu na majarida mbalimbali kutoka kwao. tuokoeni visenti vyetu kwa kuboresha mahospitali yate na kutengeneza mazingira mazuri ya watoto wetu kupata elimu

    ReplyDelete
  3. KUHUSU HILI SWALA LA GLOBAL WARMING NI KWAMBA KILA MTU DUNIANI ANACHANGIA KUONGEZEKA KWA JOTO KWA NAMNA YEYOTE ILE.KWA MFANO KIDENDO CHA KUCHOMA [MAKAA MAWE,BIOMAS,PETROL.HAYO YOTE NI KUONGEZA CARBON DIOXIDE.Hata kitendo cha wati kwenda huko capehangen ni tayari wameongeza carbon dioxide .kwa nini ni kwamba wametumia usafiri unaotumia mafuta.

    ReplyDelete
  4. haya mambo watu wanasomea na wana vifaa,sasa uje na wasiliana na mmoja wa ofisa wetu ili akuonyeshe jinsi gani uchomaji wa misitu unasababisha global warming.tuna vifaa njoo Hananasif karibu na kituo cha polisi Uliza hiki chama chetu IREQ.ILI UJUE.NA KUPATA KUELEWA.

    ReplyDelete
  5. Ndugu zangu wa IREQ tafuteni watu wenye utaalamu wa kweli wa haya mambo badala ya kutaka kupotosha watu. Mataifa ya magharibi yanachoma dizeli na petroli si kawaida, huwezi kulinganisha na uchomaji wetu wa kuni tunazookota chini mwituni. Ukifanya carbon balance ya vijiji vyetu utabaini kwamba hewa ya kaboni wanayoitoa inarejelezwa kwenye miti na kuendeleza mzunguko. Kazi ipo kwa mataifa ya magharibi yanayounguza petroli, makaa ya mawe, dizeli nk.
    Tusibebe mzigo usiokuwa wa kwetu. IREQ, rekebisheni hilo.

    ReplyDelete
  6. carbon Emissions of 15 saloon car in third world is equal to one Industry in developed country.We are part of adding carbon dioxide.By burning so as to clean our shambas and ride away bad insect and animals.Most of our national parks are always burn dry grasses so as to let the new to grow up.BANK OF CARBON IS [MAKAA YA MAWE,FOREST,PETROLI,DEZELI].Once you burn them you let out.And when comes up and mix with oxygen we call them "carbon dioxide].

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...