RAIS JAKAYA KIKWETE AKITANGAZA RASMI KIFO CHA SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA LEO IKULU JIJINI DAR
WANAHABARI WAKIMSIKILIZA AIS JAKAYA KIKWETE AKITANGAZA RASMI LEO KUHUSU KIFO CHA SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA MUDA MFUPI ULIOPITA IKULU, DAR. JK AMETANGAZA PIA SIKU SABA ZA MAOMBOLEZO KITAIFA AMBAPO BENDERA ZITAPEPEA NUSU MLINGOTI NCHI NZIMA. MAANDALIZI YA MAZIKO YANAENDELEA NA JK KAOMBA SUBIRA NA ITATANGAZWA WAKATI WOWOTE MAMBO YAKISHAKAMILIKA
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGEA NA MWANASIASA MKONGWE MZEE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU BAAD A YA KUTANGAZA RASMI KIFO CHA SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA LEO IKULU JIJINI DAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. inna lillah waina illah rajoon.mola ailaze mahali pema.aliekuwa kiongozi katika viongozi.aliekuwa mchapa kazi katika kambi ya wachapa kazi.

    -Aballah Mohammed Oman

    ReplyDelete
  2. inalillah waina illah.ni masikitiko makubwa. twamwombea roho yake mahali pema. mchapa kazi kati ya wachapakazi.aliekuwa kiongozi kati ya viongozi

    ReplyDelete
  3. INNALILLAH WAINNA ILAYHI RAJI'UN.

    Salamu za rambi rambi kwa Familia ya marehemu na TAIFA kwa ujumla, nimezipokea kwa hozuni taarifa za kifo cha mpendwa wetu Mzee KAWAWA, MAY GOD forgivbe him. Kamwe sitosahau jitihada zako

    REST IN PEACE SIMBA WA VITA.

    JUNIOR OF HYDERABAD.

    ReplyDelete
  4. Mzee michuzi anza kwa 'demo' ya speech ya JK kuhusu huo msiba uweke ktk video urushe ktk 'youtube' tuanze mwaka mpya

    ReplyDelete
  5. MH! This is shocking! Jana kwenye taarifa ya habari ITV walisema alikuwa anaendelea vizuri na aliongea hata na akina Kingunge, in fact na Kingunge mwenyewe alisisitiza! Picha zilizoonyeshwa pia zilidhihirisha kwamba hali yake ilikuwa under control. Nafikiri imefika wakati viongozi wa Tanzania wawe wakweli, call a spade a spade. Kama wanaijeria, raisi ana hali mbaya wanataka kieleweke, nani anaachiwa madaraka, sio kupamba hali nzuri wakati mtu kafikia death bed.

    Mzee Kawawa asante kwa uliyoyafanya Tanzania itakukumbuka daima. Rest in Peace.

    ReplyDelete
  6. NI HABARI ZA KUSTUSHA SANA.RIP SIMBA WA VITA.

    Bongosamurai

    ReplyDelete
  7. Rest in Peace.

    So ina maana hizo siku saba watu hawaendi makazini?

    ReplyDelete
  8. R.I.P MZEE KAWAWA
    TAIFA LINAVUJA MACHOZI. POLE JK NA WATANZANIA WOTE. TUIOMBEE FAMILIA YA MZEE KAWAWA MUNGU AIPE NGUVU NA MOYO WA SUBIRA.

    ReplyDelete
  9. Ooh! Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi,kwani hiyo ni njia ya kila mmoja wetu.Mwenyezi Mungu awape nguvu na ujasiri familia zima ya mzee Kawawa.

    mdau
    scandinavia

    ReplyDelete
  10. kwa hiyo na kazi hakuna kwa siku saba au ??

    ReplyDelete
  11. Nyerere yupoo Nyerere yupo ukiona kundi la siasa Nyerere yupoo, Kawawa yupoo Kawawa yupo ukiona kundi la siasa Kawawa yupoo na Jumbe yupoo na Jumbe yupo ukiona kundi la siasa na Jumbe yupoo,aaahhh!!! Nyimbo kama hizo zinanikumbusha mbaaali enzi hizooo. Mwenyezi Mungu ndo mpangaji wa yote kapumzike mahala pema peponi mzee wetu.

    ReplyDelete
  12. Pole Mhe. Rais. Huu ni msiba mkubwa wa Taifa. Msiba wetu wote. Mungu ailaze pahali pema peponi roho yake.
    Swali. Je hivi huyo mpiganaji hapo nyuma sharti awepo kila pahali? Si angekaa kando tu?

    ReplyDelete
  13. Utabiri wangu wa jana Mkuu naona sasa unaanza kufanya kazi!Mungu amlaze mahala pema Simba wa Vita!
    Ila naendelea kutabiri, Bwana Michuzi tutakupigia debe pale Mlimani ili upate doctorate yako!Au wadau munasemaje?
    Utabiri unaendelea kuwa Mvua kubwa itanyesha maeneo ya nyanda za juu na kuleta maafa makubwa.Pia kutakuwepo na mabalaa ya hapa na pale kwenye mkesha wa mwaka mpya, Hivyo ni vyema watu wakavaa nguo za Kijani au Buluu Bahari ili kujilindana pepo wachafu usiku wa mkesha
    Chuo cha Uganga
    Ugirikini

    ReplyDelete
  14. RIP Simba wa Vita. Ulifanya yale uliyoweza kufuatana na wakati na hapana shaka sura yako katika kitabu cha historia ya taifa haina ubishi.
    hoja ya kiuzushi: nami ninaungana na mdau kuuliza je huo utamaduni wa mlinzi wa rais kwenye uniform ya jeshi anayesimama nyuma yake kila aendapo, hatuwezi kuachana nao na ukatumika ulinzi na usalama wa kisasa zaidi!!!

    ReplyDelete
  15. Mourning period ni siku saba kwa bendera kupepea nusu mlingoti. Siyo siku saba kutokufanya kazi. Hapana. Tutaenda kazini kama kawaida huku tukiwa bado kwenye majonzi ya kifo cha Mzee wetu.

    ReplyDelete
  16. "INNA LILLAH WAINNA ILLAHYI RAJ`UN"

    Salaam za rambi rambi kwa familia ya mzee wetu kwa huu msiba wa Taifa zima.
    Mzee Kawawa ni baba na babu wa watanzania wote ni mmojawapo wa wazee wetu walioiweka misingi ya siasa ya umoja na amani katika nchi yetu tukufu.
    Pamoja na siku saba zilizotangazwa na mheshimiwa rasi Kikwete,kuwepo na matayarisho ya mazishi ya kitaifa.
    Tungekuomba mkuu wa blogu yetu ya jamii kutundika maelezo ya tangazo la mhs raisi kikwete na mazishi ya mzee Kawawa katika kijidirisha cha "You Tube" kama changamoto ya ukurasa mpya blogu ya jamii.
    Picha zinatupa kumbukumbu na kijidirisha cha "YOU TUBE" kitatuunganisha katika msafara wa mazishi ya kumuaga mzee wetu kijamii na kitaifa.

    Mickey Jones-Denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...