JK akiweka shada la maua katika makaburi ya watu kumi na nne wa familia moja ya Shumbi walofariki dunia kutokana na maporomokoa ya udongo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Mamba Miamba,wilayani Same,Mkoa wa Kilimanjaro mwezi uliopita.Rais kikwete alifanya ziara maalumu kijijini hapo ili kuwafariji wafiwa na kujionea uharibifu wa mali uliotokana na mvua hiyo. JK akiwahutubia jana wananchi wa Kijiji cha Mamba Miamba wilayani Same wakati wa ziara maalumu ya kuwafariji kufuatia mvua kubwa iliyoleta maafa na kuharibika kwa mali.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nakushukuru Mheshimiwa Rais kwa kujali. Asante sana kutufariji. Mungu akuzidishie mema.

    ReplyDelete
  2. Mhe, Rais anaendeleza moyo wa uzalendo ambao ulianza toka enzi za mwalimu.
    Hili ni jambo jema sana kwa Watanzania wote.
    Watanzania tunafahamika kwa umoja tulionao, bila kujali ukabila, dini na itikadi zetu za kisiasa, mara zote tumekuwa msatari wa mbele kusaidiana majanga yanapo tupata.
    Ushauri ulio mwema kwa serikali, ni kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya kueleka inasambaa kila kona ya nchi yetu.
    Huko Mamba Myamba alikoenda Mhe, Raisi, barabara zilichimbwa na wananchi kwa kujitolea, kile ambacho serikali ingewasaidia kwa kutambua juhudi za wananchi hao ni kuifanya barabara ya kwenda huko iweze kupitika kipindi chote cha mwaka, ili hata kama mvua kama hizo zilizo sababisha maafa zikitokea misaada iweze wafikia kwa haraka.
    shukurani.

    mdau wa ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...