Na Mwandishi Maalum, Havana, Cuba
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Havana, Cuba, kuanza ziara rasmi ya siku tatu nchini Cuba kwa mwaliko wa Rais Raul Castro Ruz.
Ndege iliyombeba Rais Kikwete na ujumbe wake imewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jose Marti, mjini Havana, kiasi cha saa tisa na nusu mchana (sawa na saa tano unusu mchana kwa saa za Afrika Mashariki), ikitokea Trinidad na Tobago.
Rais Kikwete na ujumbe wake umekuwa katika Trinidad na Tobago tokea Alhamisi iliyopita, Novemba 26, 2009, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi za Jumuia ya Madola uliofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, wa Port of Spain. Mkutano huo umemalizika jana, Jumapili, Novemba 29, 2009.
Kwenye uwanja wa Jose Marti, Rais Kikwete na ujumbe wake wamelakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mama Ana Teresita Gonzalez, Balozi wa Cuba katika Tanzania Ernesto Gomez, na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba Hector Igarza.
Wengine waliompokea Rais Kikwete ni Balozi wa Tanzania katika Cuba Balozi Peter Kallaghe ambaye ana makazi yake nchini Canada, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Sultan Mugheiry.
Pamoja na kwamba Rais Kikwete na ujumbe wake ambao ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amewasili Cuba leo, sherehe za mapokezi yake rasmi zitafanyika kesho, Jumanne, Desemba Mosi, 2009, kwenye Kasri ya Mapinduzi (Palace of the Revolution).
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo rasmi, Mhe. Rais Kikwete kesho ataanza ziara yake kwa kuweka shada la maua kwenye kumbukumbu ya Shujaa wa Kitaifa wa Cuba, Jose Marti kwenye Bustani ya Mapinduzi na kutembelea Jumba la Maonyesho la Shujaa huyo.
Baadaye, Rais Kikwete atatembelea kiwanda cha dawa cha Labiofam kabla ya kwenda Kasri ya Mapinduzi kwa ajili ya mapokezi rasmi na kufanya mazungumzo ya Kiserikali na Rais Jenerali Raul Castro Ruz.
Jioni ya kesho, Jenerali Raul Castro Ruz, atamwandalia chakula rasmi cha usiku cha makaribisho. Keshokutwa, Jumatano, Desemba 2, 2009, Rais Kikwete atakwenda Jimbo la Santiago de Cuba, ambako yalianzia Mapinduzi ya Cuba ya mwaka 1959.
Mhe. Rais Kikwete aliwasili katika eneo la nchi za Caribbean tokea Jumatatu, Novemba 23, 2009, kuanza ziara rasmi ya Kiserikali yenye mafaniko makubwa katika Jamaica kabla ya kuelekea Trinida na Tobago.

Ndugu uliyeandika hii habari ya ziara ya Kikwete,ungefaa ufafanue mafanikio makubwa ya ziara ya mheshimiwa huko Jamaica.Hivi kweli kuna kitu tunategemea kupata kutoka Jamaica? Mkuu wetu aangalie priorities, halafu kweli mkuu wa nchi anapokelewaje na naibu waziri wa mambo ya nje? Hii sio sawa, inaonyesha kuwa hao mabwana wana kazi nyingi hawana muda wa kupoteza kupokea watanzania wanaozurura nej kila kukicha.Bunge liangalie sasa ziara za mheshimiwa kupima kama kweli zina tija kwa walala hoi wa tz
ReplyDeletena huyo anayesema saa tisa na nusu mchana ya cuba ni sawa na saa tano na nusu mchana east african time its so wrong....
ReplyDeleteAnony ziara ya Jamaica ilikuwa na mafanikio sana kwani aliwaomba "wawekezaji" wa kijamaica waje waweze tz so siku si nyingi tutarajie walima ndizi wa jamaica waikimiminika nchini. Lakini pia wajenzi wa bembea huenda wakaja kwani wanahisi soko huku si baya sana.
ReplyDeleteIpo siku mtu atapokelewa na Mwenyekiti wa mtaa wa WallStreet.
ReplyDeleteJUMATANO 2 DESEMBA TUTAANDALIWA CHAKULA CHA USIKU, KARIBUNI.
ReplyDeletemh alishafanya ziara BIHARAMULO au ndo anatafuta wanadredi wakalime MINDIZI KAGERA
ReplyDeletetuna matumaini anao madaktari wake katika msafara huo maana hiyo mizunguko inaweza kuleta balaa! ni bora akazungikia the carribeans kuimarisha urafiki na diplomasia kuliko kwa 'wenzetu' ambako ni kuwa ombaomba!
ReplyDeleteHAKO KA-JET KA MUHESHIMIWA JK KANAKULA AIRMILES,BAADA YA 2015 KATAUZWA KWA TSH 100 TEH TEH TEH
ReplyDeleteUsikose kupita Venezuela kwa Chaves. Ziara ya Cuba, hapo ni bomba. Vijana wetu wakajifunze ushushu. Usikose kumuona Fidel na kupata busara zake.
ReplyDeleteHivi kwa Nini Raisi Wetu atulii Nyumbani na Kuendeleza Nchi...Coz Nchi Ujengwa na wenye Nchi.....Hakuna Mgeni atakae leta changez Tz..Kama sio sisi wenyewe....
ReplyDeleteMbona Mh. Kikwete katika ratiba yake hasemi kama atakutana na watanzania waishio huku, hususan wanafunzi?Na mheshimiwa Membe ni mwenyeji sana wa huko Cuba wakati akiwa ubalozini Canada, au ndiye aliyemshauri Rais asiwaone wanafunzi???? Eh! Jamani hebu angalieni basi hata Cuba rais anapokelewa na NAIBU waziri,nyinyi TZ waimba nyimbo tu wanapokelea na viongozi wakubwa.Mjomba katika muda umeshemsha, saa tisa na nusu mchana ya Cuba ni sawa na saa tano na nusu ya usiku Tanzania.Tunaomba Mh. rais na ujumbe wake wakirudi nyumbani watuelezee walichokiona huko Cuba na walichojifunza, maana sisi tunaambiwa tu kuwa ni masikini wana shida na wakomunisti, lakini wanatupatia misaada kama madaktari na mainjinia sasa wanatokea wapi?mbona wanatengeneza madawa mengi tu wao wenyewe na vifo vya watoto viko chini sana huko?Mh. ukirudi hebu tuelezeeni kulikono huko.
ReplyDeleteNyie mnaosema mimi mwenyeji CUBA ni waongo, mimi nilikuwa nashughulikia Canada tu huko uswazi nilikuwa sijawahi kufika ndo mara ya kwanza.
ReplyDeleteTukitoka huku tunaelekea Mexico then German afu Tunisia, Tutauwa dar February mwanzoni. wasalimieni wote. Membe
jaman naomben kuuliza kuna jambo ambalo sijalielewa vizur,hiv ni sawa rais wa nchi ukaenda katika nchi ya mwenzako ukapokelewa na Naibu Waziri naona kama kunakasoro kidogo hapo?
ReplyDeletewewe anonymous wa 01.36 pm, ni hivi Rais wa nchi kupokelewa na ,tena, naibu waziri siyo kuna kasoro kidogo, ni KASORO KUBWA SANA, yaani hapo ni aibu tu, maana inaonekana hakuwa na umuhimu saaaaana wa kuwepo hapo, yaani kwenda au kutokwenda Cuba ni sawa tu kwa waCuba.Hebu labda jaribu kunifahamisha Hivi TZ inaweza kuwasaidia nini Cuba?au ni Cuba kutusaidia sisi.Jamani viongozi wetu hamjifunzi tu!!
ReplyDelete